Uchaguzi 2020 Nilikuwa siamini, sasa nimeamini uchaguzi huu ni muhimu sana

Thomas10

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
841
2,268
Tangu juzi kulikuwa na tetesi za kwamba mitandao ya kijamii itazimwa kuanzia leo tarehe 27/10. Binafsi sikuamini kabisa habari hii kwa sababu moja tu

Hakuna athari itakayotokea kuharibu uchaguzi kwa watu kuendelea kutumia mitandao hii. Sasa imefungwa, bila taarifa kwa umma au yawezekana mimi ndio sikubahatika kupata taarifa. Naumia mno, nasononeka sana ukizingatia mahali nilipo sina namna nyingine ya kupata habari kwa haraka zaidi ya kupitia twitter, whatsapp, insta au FB.

Kwa sababu hii, naamini kuwa uchaguzi huu ni muhimu pengine mwingine wowote uliowahi kufanywa hapo awali. Kweli JPM hana tumaini la kumshinda Tundu Lissu, na njia pekee ni kutumia ubadhilifu, naelekea kuamini hivyo japo awali sikuwa na imani hiyo.

Nina swali dogo tu, kungetokea nini kama mitandao hii ingeendelea kuwa active? Nini kimekusudiwa kufichwa ambacho hakitafumbuliwa hata siku wakiiwasha tena?

JPM na serikali yake wanalenga kufanya nini?
 
Mitandao ya kijamii ndio njia kuu ya kupashana habari, japo wamevibana vyombo vingine vya habari kwa kuvifungia ili visitangaze habari za upinzani, lakini mitandao ya kijamii kama twitter, fb, na instagram imewezesha kwa kiasi kikubwa sana kusaidia kampeni za Lissu.

CCM wanaiogopa hii mitandao kwasababu wanajua ndio itatumika kwa kiasi kikubwa kwenye kusambaza habari wakati wa uchaguzi, mfano, kutangaza mshindi kwenye kituo fulani au jimbo fulani pale ambapo majumuisho ya kura yatakuwa tayari yameshafanyika.

Ndio maana unasikia sasa hivi wanapiga marufuku mawakala wa vyama kuingia na simu kwenye vyumba vya kuhesabia kura, hii ni njia mojawapo ya kihuni inayotumiea na CCM kwenye kuiba kura kwa kuzuia jamii isipate matokeo halali kwa wakati.
 
Hii yote ni kuzuia wapumbavu wachache kusambaza propaganda za kizushi! Watanzania linapokuja suala la uzushi mitandaoni tuko vizuri sana!

Sasa katika kipindi hiki cha kumzuia Amsterdam ni muhimu sana kuzuia wajinga wasilete ngebe mitandaoni
 
Back
Top Bottom