Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,217
- 1,705
Mk 8:27 SUV
[27] Akatoka Yesu na wanafunzi wake, wakaenda kwenye vijiji vya Kaisaria-Filipi; na njiani akawauliza wanafunzi wake, akasema, Watu huninena mimi kuwa ni nani?
Swali hili waliloulizwa wanafunzi linatuhusu mimi na wewe leo, kwa sababu tunaweza tukawa tunasema tumeokoka ila tukawa na mtazamo tofauti juu ya Yesu.
Kila mwamini akiulizwa swali hili anaweza akawa na majibu yake tofauti, tena majibu mengine yanaweza kukushangaza kabisa.
Utashangaa kile kitajibiwa na mtu ambaye unamwamini ni muumini wa siku, alafu akitoa majibu ambayo hukutegemea.
Sijui unamwonaje Yesu au unaufahamu kiasi gani juu ya Yesu, vile unamwona Yesu ndivyo mambo yatakavyotokea kwako.
Ukiwa unaufahamu kwa kiasi kidogo juu ya Yesu, atakuwa kwa kiwango kile kile katika maisha yako.
Ukimwona Yesu hawezi kukusaidia jambo fulani, ndivyo itakavyokuwa kwako, hawezi kufanya nje na imani yako.
Ikiwa umwona Yesu kwa viwango vya juu, ndivyo itakavyokuwa kwako, vipo vitu vitakuwa kwako vya viwango vya juu.
Eneo tunalomweka Yesu ndivyo itakavyokuwa katika maisha yetu, jambo ambalo linaweza likawa jema au lenye upungufu fulani.
Unaweza kuona ni jinsi gani ilivyo muhimu kukazana kuongeza kiwango chako cha imani yako, ili uanze kumwona Yesu katika ukubwa.
Soma biblia kwa mtazamo mpana, usisome kwa ajili ya kuhubiri au kufundisha au kumshinda shetani tu, soma kwa malengo mapema ya ufalme wa Mungu.
Maisha yako yanaweza kubadilishwa moja kwa moja na Yesu, watu wanaokufahamu wakaachwa midomo wazi kwa yale wanayoyaona yakiendelea kwenye maisha yako.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana