Nilikuwa Kipofu, Sasa Ninaona – Haleluya!

Walishika msahafu wakatuuza kama watumwa huku wakiwatafuna dada zetu
Walishika biblia wakatutesa kwa viboko na wakaiba rasilimali zetu
Walishika msahafu lakini sio msahafu uliotenda maovu hayo. Waliotenda hayo ni watu wenye mioyo mibovu, waliopotosha ujumbe wa Biblia. Dini ya kweli haifundishi utumwa, unyonyaji, au unyanyasaji, bali upendo, haki, na heshima kwa binadamu wote.
 
Ubarikiwe wewe na kizazi chako.nimezini leo,nahisi hatia ndani yangu...
 
We badoo kipofuu.
Mara nyingi, ukipoteza kitu ndio unajua thamani yake! Huwezi kujua sana thamani ya macho yako mpaka uwe kipofu kwanza.

Ukipoteza uono, yaani macho yako yasipoweza kuona kwa muda mrefu, kisha ghafla ukaanza kuona tena, ni kama dunia inasherehekea nawe! Nuru inakuingia kwa nguvu, rangi zinacheza mbele ya macho yako kama siku ya tamasha kubwa. Kila kitu kinakuwa kipya kana kwamba kimeumbwa kwa ajili yako tu.

Ni hisia inayoweza kukufanya ulie na kucheka kwa wakati mmoja, kwa sababu safari ya kutoka gizani hadi kwenye mwanga ni tukio la kushangaza. Huo ndio uzuri wa kuona baada ya kutokuona kwa muda mrefu. Ni furaha isiyoelezeka kwa urahisi, na shukrani isiyo na kikomo.

Mimi sio wa kwanza kupitia mabadiliko haya makubwa. Katika Biblia kuna habari ya mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. Mtu huyo aliponywa na Yesu kwa muujiza. Kwa furaha na mshangao, akasema: “Nilikuwa kipofu, sasa ninaona” (Yohana 9:25). Tofauti yake na mimi ni kwamba, yeye alikuwa kipofu wa kimwili, lakini mimi nilikuwa kipofu wa rohoni, fikra zangu zilikuwa zimepofushwa na ibilisi.

Kwa sababu ya upofu wa rohoni, matusi, chuki, kusema uongo, vyote hivyo sikuona ubaya wake. Maisha ya uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo sikuona hatari yake, hadi Yesu aliponiondolea upofu wa rohoni. Hiyo ilitokea miaka kadhaa iliyopita, katika mkutano wa Injili. Siku hiyo Yesu alinigusa, akanipa macho mapya ya rohoni. Sasa ninaona nuru yake ang’avu. Natambua waziwazi dhambi ni nini na mshahara wa dhambi naujua. Hiyo ndiyo hali anayokutana nayo kila mtu aliyekuwa dhambini kisha akaokoka.

Yesu alipoingia ndani ya moyo wangu alileta badiliko halisi la maisha. Ukinikasirisha, mimi nacheka tu. Ukinichukia, mimi nakupenda tu. Ukinidharau, mimi nakuhurumia. Ukinitupia mawe, mimi namshukuru Yesu. Haya ndiyo maisha ya kila mtu aliyeokolewa kwelikweli na Yesu.

Asante Yesu kwa kuniokoa. Asante Yesu kwa kuwa sasa ninao uhakika wa kuingia mbinguni.
 
Macho Yako yanaona mazuri ni dini yko tuh.
Huna upendo kwa wengine kma yesu alivofundisha
Unasema unamuamini Ila mabandiko yko yanaonyesha una chuki na watu wasio na msimamo kma wako
Ukijifunza hilo utakua kma unavyojinadi ila ukishupaza shingo
Bhc upofu utakutawala
Yesu hakubagua dini wala kabila
Ndio maana aliingia kwa wayahudi na kwa waislam pia kwenye sinagogi zao

Aisifuye mvua imemnyea!
Huna upendo kwa wengine kma yesu alivofundisha
Ningekuwa sina upendo nisingehangaika kukueleza habari njema za Yesu. Ningesema: "shauri yako, utajiju"
Unasema unamuamini Ila mabandiko yko yanaonyesha una chuki na watu wasio na msimamo kma wako
Hayo ni mawazo yako. Yesu aliniondolea chuki miaka mingi iliyopita. Maandiko yananiambia: "Ikiwa mtu atasema, “Nampenda Mungu,” lakini anamchukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa maana kila mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, atampendaje Mungu asiyemwona? (1 Yohana 4:20)
Yesu hakubagua dini wala kabila
Ndio maana aliingia kwa wayahudi na kwa waislam pia kwenye sinagogi zao
Inaonekana somo la historia ulilikwepa. Yesu alipokuwa duniani, Uislamu haukuwepo. Uislamu ulianzishwa karne ya 7 BK na Mtume Muhammad, ilhali Yesu aliishi karne ya 1 BK. Kwa hiyo, Yesu hakuingia kwenye sinagogi za Waislamu kwa sababu hakukuwa na Waislamu wakati huo.
 
Ndugu yangu Mangwea1900, inaonekana hujajua kwamba kuna dini safi na dini nzuri. Wanaotumia dini kama silaha ya kuwamaliza wanadamu maskini ili kujitajirisha, waliishatajwa zamani katika 1 Timotheo 6:5. Hao hawakubaliki mbele za Mungu kwa sababu hawana dini safi.
Yakobo 1:27 inafafanua kwamba dini safi ni kumsaidia yatima na mjane, na kujilinda na uchafu wa dunia. Hiyo ni kinyume kabisa na silaha ya kuwamaliza wanadamu maskini.
Kumbe mungu ana dini
 
Mbona vipofu ni wengi duniani ina maana hawaijui hiyo tiba yako
 
Asante zumbemkuu
I profoundly appreciate your felicitations; indeed, the illumination of my inner being has been nothing short of a transcendent awakening
Imebidi nisome mara kadhaa, hii misamiati.
Hongera sana kwa hatua hiyo. Binafsi nachukia sana uongo, na nikilazimika kuongea uongo huwa najiskia vibaya sana.
Mengine yanavumilika, kazi ngumu kuacha PCs
 
Aisifuye mvua imemnyea!

Ningekuwa sina upendo nisingehangaika kukueleza habari njema za Yesu. Ningesema: "shauri yako, utajiju"

Hayo ni mawazo yako. Yesu aliniondolea chuki miaka mingi iliyopita. Maandiko yananiambia: "Ikiwa mtu atasema, “Nampenda Mungu,” lakini anamchukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa maana kila mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, atampendaje Mungu asiyemwona? (1 Yohana 4:20)

Inaonekana somo la historia ulilikwepa. Yesu alipokuwa duniani, Uislamu haukuwepo. Uislamu ulianzishwa karne ya 7 BK na Mtume Muhammad, ilhali Yesu aliishi karne ya 1 BK. Kwa hiyo, Yesu hakuingia kwenye sinagogi za Waislamu kwa sababu hakukuwa na Waislamu wakati huo.
Uislam ulikuepooooo kbla ya yesu na yesu ajaleta ukristo.
Wala hajui nn maana ya kanisa maana hakuacha kanisa
Tena siku akirudi akaona misalaba mtamfanya apate mawazo mnoo maana aliteswa kwenye msalaba 😁
Dini yenu ukitumia common sense utajua ni ya kuunga unga
 
Weka basi ushahidi wa hayo uliyosema
 
Imebidi nisome mara kadhaa, hii misamiati.
Daah, jina lako linaashiria umetokea eneo lenye wasomi sana. Imekuwaje tena hiyo imekuwa misamiati ya kusoma mara kadhaa? 🙂
Hongera sana kwa hatua hiyo. Binafsi nachukia sana uongo, na nikilazimika kuongea uongo huwa najiskia vibaya sana.
Mengine yanavumilika, kazi ngumu kuacha PCs
Kama huwa unalazimika kuongea uongo, nafikiri hujajua kwamba waongo hawataurithi ufalme wa Mungu. Tubu mapema dhambi hiyo na usiirudie kabisa.
Ufunuo 21:8
“Bali waoga, wasioamini, wachukizao, wauaji, wazinzi, wachawi, hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti; hii ndiyo mauti ya pili.”
 
Back
Top Bottom