nilihisi haniamini sasa Simuamini yeye | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nilihisi haniamini sasa Simuamini yeye

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Elia, Sep 20, 2012.

 1. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  amekuwa anapeku sana simu yangu
  anapekua mikoba yangu
  anapekua nguo zangu
  kila anachotaka najitahidi kumpatia hata nikishindwa huwa nimejitahidi sana
  hapendi kusikia nimemsaidia mtu.. anadai sisi wanaume hatujui kutunza hela...

  KILICHONIFANYA niandike hii thread leo ni hiki:

  MOJA ya masharti au msimamo wangu ni kwamba sitaki kusikia jambo la ndani ya nyumba (tatizo) limepelekwa sehemu nyingine yeyote, tukishindwa kulitatua sisi wawili huko itakuwa ni kujichoresha tu. Hili nililiweka clear kwake naye akaliafiki na kuunga mkono..
  MBILI sipendi kufichana fichana kama kunakitu kinafichwa basi sio kizuri, nalo lilikuwa clear na lilieleweka

  Wiki iliyopita katika kupitia pitia simu yangu amekuta meseji alizoona zinautata akanipigia simu. akihitaji maelezo alikuwa MKALI sana...nilimpa maelezo ilikuwa ni hizi meseji za utani ambazo huwa tunatumiana. nilimueleza undani wa hizo meseji... niliona tatizo kwake ilikuwa imeandikwa na mwanamke.. nilimfafanulia ikiwa ni pamoja na kumpigia simu huyo muhusika mwisho nilimsifu kwa kitendo chake cha kuuliza kwangu ili apate ufafanuzi, nikimsihi asije peleka matatizo yake nje alinithibitishia kwamba hawezi kupeleka jambo kama hilo nje ovyo ilhali yeye ni mtu mzima sasa...

  siku moja ikapita nikaitwa na mama mchungaji nikaona siwezi kwenda peke yangu nika mwambia anisindikize maana alikuwepo tu nyumbani. tulifika kwa mchungaji tukaongea sana baadae tukaishia kula chakula na juisi then nikaaga nikitegemea ataanzisha alichoniitia lakini sikupata kitu.. nikamuuliza una neno ulilo niitia? akasema basi tu niliwamiss,

  tukaondoka nyumbani nika mwambie mwenzangu kwakweli mimi sijaipenda hii safari yetu nimeacha mambo yangu mengine nikidhani kuna la muhimu kama nilivyo itwa kumbe kuuza sura tu... akaniambia usichukie hata kusalimia ni jambo jema yakaishia hapo..

  jana nilitumia simu yake kutuma meseji kwa mdogo wangu ikafeli na kujisevu(auto) kwenye draft.. nilipoweka vocha nikaenda kuitafuta kwenye draft ndipo nika kuta meseji mbili zilizo nikosesha usingizi usiku wa leo

  1. .....naomba usimwambie habari ya zile meseji maana naona hali huku sio nzuri nitarekebisha mwenyewe.
  2.......hiyo hela iliyobaki nitakumalizia mwezi wa kumi na moja

  Nilipo angalia ile meseji ya kwanza ilikuwa ni siku nilipoitwa kwa mchungaji na ilitumwa kwa mama mchungaji.
  Hii ya pili sikuielewa ikanibidi nizame kwenye mkoba wake (sio kawaida yangu) nikakuta mkataba wa manunuzi kwa jina lake akiwa amelipa milioni sita na laki nne zimebaki milioni moja na laki sita, nilishituka sana maana hana kipato kingine zaidi ya kunitegemea mimi

  MWISHO nilihisi haniamini nikawa najitahidi kumfanyia kila anacho taka ikiwa ni pamoja na kumpeleka shule na kumpa nafasi ya kusimamia vibiashara ninavyofungua 80% vilikuwa vinakufa.. kwakweli nimekosa imani naye kabisa na usiku nimewaza mambo mengi sana
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Kwanza kabisa muulize
  labda kuna majibu ya kuridhisha

  mengineyo yoote yafuate baada ya kumuuliza
  hata ushauri wa humu hauna maana kama hujasikia utetezi wake
   
 3. Kamanda Moshi

  Kamanda Moshi JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,419
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  pole mkuu hebu uliza kwanza, lakin cha ziada alikopata hizo pesa za kununulia hicho kiwanja ni wapi?hapo lazima uwe serious sana, na kwa haraka huyu mkeo hakuamini wewe, kwa nin anunue kiwanja kwa siri?ana lengo gan?hayo yote uulize kabisa na umbane upate clear answers.
   
 4. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  hayo maswala yakupelekana kwa mama mchungaji sijui ni sawa na wote mnatembea uchi kumbukeni wale ni bindamu na wana mapungufu yao.
  swali:
  huyo ni mkeo halali au mchumba?
   
 5. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Swala la pesa sijamuu liza ila kuhusu kutoa mambo ya ndani nje alikataa katakata ni hiyo meseji tu ndio iliyonipa jibu kinyume na alivyo sema yeye @Amstadam nimeshazaanae watoto wawili ni mke. kamanda moshi hilo la pesa limenichanganya mkuu nitamuuliza
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,222
  Trophy Points: 280
  ndo maana biashara zimekufa, jibu ushapata!

  Zungumza nae, kuhusu msg, kwanza heri kamwambia mama mchungaji kuliko angewaambia mashosti zake!

  Halafu nyie mnaishi kwa kuviziana, hebu kuweni huru mwambiane mipango yenu na mshirikiane
   
 7. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  mkuu mbona na wewe umekiuka makubaliano yenu ya awali ya kuto-toa siri za ndani nje???...

  Kwanini umeyaleta hapa jf?..kupata ushauri sio?...the same to her..alipeleka kwa mama mchungaji kupata ushauri... na kwann umeshamuhukumu kuwa 80% ya vijibiashara vyako huwa vinakufa chini ya usimamizi wake?...huoni kama unatoa hukumu kwa kosa ambalo hujalidhibitisha....

  Utajisikiaje kama atakuambia hiyo pesa aliyonunulia kitu ni mchezo anacheza na wenzake kwa kile kiasi kidogo cha pesa ulichokuwa ukimpatia toka umuwowe na mpate watoto wawili?..

  naomba uwe mwanaume wa shoka na usimamie maamuzi yako...hapa umekurupuka kuleta mada jf kabla hujaichunguza na pia umekiuka maamuzi yako ya kuto-toa siri nje ya familia... Pole sana mkuu.
   
 8. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  hizi simu hizi...

  mpaka watoto wajae mitaani tukose pa kupitisha magari ndio tutajuwa madhara ya kupekuana
  na kutafutana tumeweka nn kwenye misimu yetu..simu ni personal and private life ieleweke hivyooo.

  Ona sasa wewe ukivunja ndowa tatizo ni lako kupekuwa simu ya mkewo...ukimchunguza bata hutoweza kumla kwa uchafu alokuwa naooo.
   
 9. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Hiki kizungumkuti..hebu ongea naye kwanza kwa namna ya uanaume.......unatakiwa kutumia skills ya hali juu, Usije ukakosa mke na pesa zako
   
 10. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Mi naona usimuulize wala nini, hapo umegundua kiwanja tuu ndo hukijui, ukichunguza unaweza kukuta ANA MIJUMBA MIWILI na wewe huijui, sasa ukimuuliza kuhusu hicho kiwanja ataomba msamaha kwa kukuficha kiwanja afu yataisha hivo ambavo hujavibamba ndo hutovijua kamwe!!!
  Kama unataka kutatua tatizo hilo lazima uwe mjanja! Kuwa mtoto wa Mjini Usimwambie nimeona meseji hiii blah! blah! blah! We muweke mtu kati mwambie bwana nina USHAHIDI wa kujitosheleza bila shaka yoyote, kuwa wewe UNAIVEST KISIRI, sasa kabla sijatoa maamuzi ya mwisho, na hitimisho, ukiwa kama Mke wangu kwa huu muda uliosalia nakupa LAST CHANCE ya kunieleza kwa KINA kila kitu ulichoficha, na KWANINI huniamini mumeo? Kutokana na habari nilizonazo nikilinganisha na utayosema, nikakuta ufichaji fichaji hauendelei WE MAY HAVE A CHANCE YA KUTUNZA NDOA! Ila kama kufichana na kudanganyana kunaendelea heri tuachane manake tutawekeana SUMU.
  Kwanza atapanic ushahidi gani ulio nao!! Nani kauza CD? Atababaika huyo kama kama amekutwa akiwang usiku, maneno yatakuwa yanakatikia kooni
  Hapo atatiririka na kufunguka A to Z @ Wifi yangu, ila  ndo YOU SHOULD EXPECT THE UNEXPECTED!!!!! Unywe dawa za kutuliza pressure mapemaaa usije kututoka!!!
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  mna siri za nini.
   
 12. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Mi naona usimuulize wala nini, hapo umegundua kiwanja tuu ndo hukijui, ukichunguza unaweza kukuta ANA MIJUMBA MIWILI na wewe huijui, sasa ukimuuliza kuhusu hicho kiwanja ataomba msamaha kwa kukuficha kiwanja afu yataisha hivo ambavo hujavibamba ndo hutovijua kamwe!!!

  Kama unataka kutatua tatizo hilo lazima uwe mjanja! Kuwa mtoto wa Mjini Usimwambie nimeona meseji hiii blah! blah! blah! We muweke mtu kati mwambie bwana nina USHAHIDI wa kujitosheleza bila shaka yoyote, kuwa wewe UNAIVEST KISIRI, sasa kabla sijatoa maamuzi ya mwisho, na hitimisho, ukiwa kama Mke wangu kwa huu muda uliosalia nakupa LAST CHANCE ya kunieleza kwa KINA kila kitu ulichoficha, na KWANINI huniamini mumeo? Kutokana na habari nilizonazo nikilinganisha na utayosema, nikakuta ufichaji fichaji hauendelei WE MAY HAVE A CHANCE YA KUTUNZA NDOA! Ila kama kufichana na kudanganyana kunaendelea heri tuachane manake tutawekeana SUMU.

  Kwanza atapanic ushahidi gani ulio nao!! Nani kauza CD? Atababaika huyo kama kama amekutwa akiwang usiku, maneno yatakuwa yanakatikia kooni

  Hapo atatiririka na kufunguka A to Z @ Wifi yangu, ila ndo YOU SHOULD EXPECT THE UNEXPECTED!!!!! Unywe dawa za kutuliza pressure mapemaaa usije kututoka!!!
   
 13. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kama wewe idadi ya kumi hamfiki duniani hapa! Em mulize kwa utaratibu, reaction ya kwanza,itakupa majibu.
   
 14. W

  WISER WISE Member

  #14
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 20, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  every thng hapen 4 a reson...juct talk to her in critical way as a head of da family yawezekana kuna sababu ilimpelekea kukuficha.....na je hizo biashara zinaingiza kiac gani kwa cku kama ni kipato cha kawaida hapo pana mashaka wap katoa mijihela yote hiyo
   
 15. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  TEMA mate TUMCHAPE
   
 16. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Elia wakati mwingine unaweza kutafuta kushauriwa kwa jambo ambalo kama ungekuwa na subira ungelitatua bila matatizo. Nashauri kama alivyosema The Boss anza kupata details kwa mkeo kwanza halaf mengine ndo yafuate. Sanasana hapa tutakupakaza asali tu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,025
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  .


  Ukiona manyoya jua keshaliwa. Huyo mwanamke wako ni mwizi, sio mwaminifu ila nachelea kusema kuwa ni Malaya.

  Ni mawazo ya Bazazi tu, usiyape umuhimu mkubwa.

  Ndimi Bazazi!
   
 18. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #18
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ushauri humu ni mwing sana utapata lakini kumbuka ukimuona mtu hamwamini sana mwenzake ujue yeye mwenyewe ana matatizo sana,kumbuka mtenda uhalifu huwa anakuwa makini sana kuzuia uhalifu usimtokee yeye na hilo ndio tatizo hapo.kuhusu kulifikisha shauri hapa ni sahihi ila ulijihisi una akili na uwezo mkubwa sana wa kutatuwa shida zako bila kujiuliza ni kwanini mungu aliwaumba binaadamu wengi.mlijiwekea ukuta wenyewe na mkeo.halafu naliona tatizo kubwa mbele yako na bahati nbaya mama mchungaji naye anaonekana sio mwema sana ni shoga yake na sio mshauri wake wa kiroho kama unavyomchukulia.tumia busara sana kuamua hili jambo lakini shtuka kaka!
   
 19. b

  beib New Member

  #19
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuwa kimya kwanza na mfuatilie kwa makini,hakikisha una uhakika na mambo anayofanya,baada ya hapo unaweza kuongea nae tena with evidence atafunguka.
   
 20. p

  pretty n JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 21, 2012
  Messages: 299
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanawake shida wanaume shida khaaaaaaaaaaaaah???? Talk 2 yo wife first reaction ndo itakupa majibu n nothng else.
   
Loading...