Nilifikiri ni kwa wanawake tu!!!!

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Nilipita sehemu na kupewa flyer ya barber shop moja yenye kutoa huduma zifuatazo:

Classic Barber ShopTunatoa huduma zifuatazo:
  • kunyoa mitindo ya aina zote na Easy wave
  • scrubbing, mask, kuosha nywele na super black
  • kutinda nyusi, ndevu magic na kupamba maharusi wa kiume

Wasiliana nasi kwa namba 0654 948 790

Tupo karibu na hospitali ya ... na duka la vocha la jumla. Karibu upate huduma bora na za uhakika.

My opinion: kwa nini wasiite Unisex salon kwani huduma nyingine ni kwa wanawake au na wale wa Cameron?! Mwanaume unatinda vipi nyusi? mwanaume unaosha vipi nywele jamani?! na mask ndio nini ehe?!!
 
kutinda NYUSI ndio noma, lakini kuosha nywele kwa wale wenye afro si mbaya
 
haha haha haha haha haha , hayo ndio wanaita mambo ya mjini, kama ya kaisari muachie kaisari, ya ngoswe muachie ngoswe, pia ya hawa masaharobaro tuwaachie wenyewe masharobaro, teh teh the kwi kwi
 
Kwa maoni yangu UMETUMWA KUTANGAZA BIASHARA HIYO JF.

Kama ni suala la kushangaa tu, ulikuwa na umuhimu gani wa kukariri namba ya simu na kuja kuiweka hapa?

Naamini mtu akipiga hiyo namba utapokea wewe. Huna haja ya kujifanyisha fanyisha na kuikandia biashara yenu ili tu uitangaze. JF ina majukwaa mengi bana, hii biashara yako kaweke kwenye matangazo madogo madogo
 
Sasa ukishamaliza kukata nywele uinazurura nazo ukidondosha kila mahali?
Hawapaki kucha rangi na hina, manake wakaka siku hizi full kubanana!
 
Back
Top Bottom