LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 19,977
- 37,879
Huu wimbo Solo Thang uitwao Miss Tanzania, nilipousikiliza kwa mara ya kwanza, nilifikiri ana mdiss Wema Sepetu au Rashida Wanjara. But nilipousikiliza kwa makini nikagundua alikuwa anaizungumzia Tanzania.

Baadhi ya punch kali zinazo patikana kwenye hili song ni :
· Baba ake alikuwa mkoloni kipindi huyu binti mwali,
Mchonga alikata utepe lakini hakuvinjari,
Sababu alikuwa bize kumlinda na geti kali,
Kumbe wenzake wanabinjuka kushtuka kakaaa mbali,
Hapa Solo Thang, anasema, Tanzania ilikuwa chini ya wakoloni wakati bado rasilimali zake haziajaanza kufujwa na wajanja. Mwalimu ndo akawa Rais wa kwanza wa nchi lakini hata hivyo yeye binafsi hakunufaika na rasilimali za taifa hili kwa sababu nia yake ilikuwa ni kulinda rasilimali za taifa kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Hata hivyo, Mwalimu alikuwa peke yake, kwani wenzake walikuwa kinyume chake, wakati yeye akimlinda binti huyu, watu alio wapa majukumu ya kusaidiana naye katika kumlinda, walikuwa wanatumia fuja rasilimali zake, Mwalimu alipokuja kushtuka, tayari akawa nje ya mfumo( Ameshan'gatuka )
· Demu alikuwa na heshima kabla hajatangazwa ruksa,
Chukua chako mapema ukimkonyeza tu ume gusa
Solothang anasema, Tanzania ilikuwa na heshima kabla ya utawala wa Mwinyi, na heshima ya nchi ilishuka baada ya Mwinyi kuingia madarakani.
· Ana sura ya dhabahu inayoita kama amezaliwa Geita,
Tatizo ndo kicheche kila mwanaume amepita
Hata Benja hakutoka kapa huyu demu hajatulia..
Solo Thang anasea, Hata Rais wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa hakuacha kuzitumia vyema rasilimali za Tanzania wakati wa utawala wake.
· Sitochoka kuwakilisha jinsi anavyo niacha hoi,
Juzi juzi katoka kuopolewa tu na Handsome Boy
Juzi juzi tu katoka kumilikishwa kwa Jakaya Kikwete.
BIG UP SOLOTHANG. HIZI NDO NYIMBO ZINAZO STAHILI TUZO, SIO NATAKA KULEWA
http://www.youtube.com/watch?v=plDLceKKPco&desktop_uri=%2Fwatch%3Fv%3DplDLceKKPco&nomobile=1