Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Ujumbe alioupost leo Zitto kabwe kwenye account yake ya FaceBook ni tusi kwa Magufuli.
" wapumbavu wakubwa Rudini kazini mara moja! Nilidhani mnataka mle kama mameneja wenu kumbe mnataka nao wawe kama ninyi? Nilidhani mnataka nanyi mpande juu...."
Haya ni maneno ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine kwa Wafanyakazi wa TAZARA mwaka 1983 alipokwenda kuzungumza nao kufuatia mgomo wao. Moja ya madai yao yalikuwa ni kwamba wao wafanyakazi wanakula chakula kibaya kwenye kantini yao ilhali mabosi wanakula chakula kizuri kwenye kantini ya mabosi iliyo juu. Kwamba wafanyakazi walikuwa wanakunywa chai ya rangi na kipande cha mkate bila siagi ( wakati huo uhujumu uchumi umenuka na hali ya nchi mbaya sana hata mkate ilikuwa ufahari), mameneja walikuwa wanakunywa chai ya rangi na mikate ya siagi na mapochopocho mengine.
Waziri Mkuu Sokoine akawauliza. Maoni yenu nini? Tufanyeje? Wakamjibu " hao nao washuke wale kama sisi' Sokoine akafura kwa hasira. Akaagiza FFU kuzima mgomo na asisikie tena fyoko. Moringe alitaraji kuwa wafanyakazi wangetaka nao wale kama mabosi wao wanavyokula.
Bahati mbaya sana Watanzania wengi hawapo hivyo. Wengi hufurahia maumivu ya wengine ( saddism). Inaitwa HUSDA.
Source: Zitto Kabwe - " wapumbavu wakubwa Rudini kazini mara moja!... | Facebook