Nilichoshuhudia kimenishangaza

Nilichoshuhudia kimenishangaza

Ndomana wengine hawapendi kukaribisha watu majumbani mwao kukwepa wafyetele wa namna hii!
 
WanaMMU
Nilikuwa safarini katika mkoa mmoja hapa Tz. Kwa kuwa ilikuwa safari ya kikazi nilipanga kufikia hotelini lakini kwenye huo mkoa nina rafiki ambaye sasa amekuwa kama ndugu na alinisihi nifikie kwake. Baada ya kuona shemeji naye anasisitiza nifikie hapo basi nikaona acha nifanye savings ya hela ya accomodation ili walau nirudi home na zawadi kwa wife.
Matukio.
Tukio la kwanza ni la shemeji kuja na jamaa ambaye alinitambulisha kama "staff mwenzangu".Hakutegemea kunikuta nyumbani muda huo kwani asubuhi nilitoka kwenda kuangalia ofisi ambayo nilikwenda kufanya kazi mkoani hapo. Hawa walikuwa wapenzi maana nilipokuwa natoka chumba cha mgeni nilisikia miguno ya kimahaba na walipotoka wakati nikiwa sebuleni ndipo nilipotambulishwa kuwa kuwa huyo jamaa ni staff mwenzake.
Huyu jamaa tunafahamiana na tulipowasiliana alinieleza kuwa huyu dada ni mtu wake kitambo na bado wanaendelea.
Tukio la pili
Siku moja kabla sijaondoka kurudi Dar,nikiwa napanga vitu vyangu usiku nikakumbuka kuwa nimeacha charger yangu sebuleni. Shemeji alikuwa amesafiri kwenda mkoa mwingine kwa shughuli ambayo siwezi kuitaja hapa. Niliporudi sebuleni ili kuchukua charger ndipo nilimuona rafiki yangu na housegirl wanafanya deep kissing kwenye kijieneo cha "dinning".
Walishtuka mi nikachukua charger na kurudi chumbani.
Hawa wana ndoa changa lakini inaonyesha wazi bado hawajawa tayari kuishi maisha ya uaminifu.
Vijana heshimuni viapo ndoa.
Vipi ile figisux2 za kumpa mke wa binamu yako mimba ilishaje? Na issue ya kumpa mke wa mtu lift mpaka akawa anakusema vizuri kila wakati ilishaji?
 
Yaani hiyo ndoa ni kama vile aliyeuza cheni bandia nae kalipwa pesa bandia..safi sana
 
WanaMMU
Nilikuwa safarini katika mkoa mmoja hapa Tz. Kwa kuwa ilikuwa safari ya kikazi nilipanga kufikia hotelini lakini kwenye huo mkoa nina rafiki ambaye sasa amekuwa kama ndugu na alinisihi nifikie kwake. Baada ya kuona shemeji naye anasisitiza nifikie hapo basi nikaona acha nifanye savings ya hela ya accomodation ili walau nirudi home na zawadi kwa wife.
Matukio.
Tukio la kwanza ni la shemeji kuja na jamaa ambaye alinitambulisha kama "staff mwenzangu".Hakutegemea kunikuta nyumbani muda huo kwani asubuhi nilitoka kwenda kuangalia ofisi ambayo nilikwenda kufanya kazi mkoani hapo. Hawa walikuwa wapenzi maana nilipokuwa natoka chumba cha mgeni nilisikia miguno ya kimahaba na walipotoka wakati nikiwa sebuleni ndipo nilipotambulishwa kuwa kuwa huyo jamaa ni staff mwenzake.
Huyu jamaa tunafahamiana na tulipowasiliana alinieleza kuwa huyu dada ni mtu wake kitambo na bado wanaendelea.
Tukio la pili
Siku moja kabla sijaondoka kurudi Dar,nikiwa napanga vitu vyangu usiku nikakumbuka kuwa nimeacha charger yangu sebuleni. Shemeji alikuwa amesafiri kwenda mkoa mwingine kwa shughuli ambayo siwezi kuitaja hapa. Niliporudi sebuleni ili kuchukua charger ndipo nilimuona rafiki yangu na housegirl wanafanya deep kissing kwenye kijieneo cha "dinning".
Walishtuka mi nikachukua charger na kurudi chumbani.
Hawa wana ndoa changa lakini inaonyesha wazi bado hawajawa tayari kuishi maisha ya uaminifu.
Vijana heshimuni viapo ndoa.
Hayakuhusu fuata mambo yako!
 
Virusi vya HPV hufanya wanaume na wanawake wapatwe na vipele vigumu, kutia ndani vipele vinavyotokea kwenye viungo vya uzazi. Kwa kawaida, vipele hivyo havina kansa. Ingawa kuna aina za virusi vya HPV zaidi ya 150, ni chache sana kati yazo ambazo husababisha kansa.
Mtu hupata saratani ya shingo ya kizazi ikiwa tu aina fulani ya virusi hivyo vinakaa kwa muda mrefu. Kwa upande mwingine, maambukizo mengi ya virusi hivyo hupona yenyewe baada ya kushindwa nguvu na mfumo wa kinga wa mwili.

Ni kina nani wanaweza kuambukizwa?

Wale hasa wanaoweza kuambukizwa ni wanawake wanaoanza kufanya ngono wakiwa na umri mdogo, wale walio na wapenzi wengi wanaume, au wale wanaofanya ngono na mwanaume ambaye ana wapenzi wengi wanawake.

Mara nyingi, mwanamume asiye na dalili zozote zinazoonekana za ugonjwa huo ndiye humwambukiza mwenzi wake.
 
hukuona kile kibao kilichoandikwa "ya hapa yaache hapa hapa umbea nyumbani kwako" hukuona?
 
Back
Top Bottom