Nilichomshauri DK WILBROAD SLAA nilipokutana nae

Kwa nini hao 30%-40% wanaojitokeza wasichague CDM waichague CCM? Kikulacho ki nguoni mwako!!!!!!!!!!!!!!!
 

Waliboreshe basi wasipige chenga kama unaona hakutakuwa na madhara yoyote...
 
Kwa nini hao 30%-40% wanaojitokeza wasichague CDM waichague CCM? Kikulacho ki nguoni mwako!!!!!!!!!!!!!!!

Kwa sababu CHADEMA imepata nguvu sana baada ya uchaguzi 2010,wengi wa wanao support CDM nu vijana walio kwenye hilo rika lililotajwa kama nimemuelewa vizuri mtoa mada.
 
Ochutz,
Kwa bahati mbaya huna ujasiri wa kuandika jina lako la kweli, hivyo siwezi kujua Kama kweli ulinipa ushauri au umetunga tu. Ebu jiulize katika akili ya kawaida, Mimi na wewe ( au Chadema) nani angelimshauri mwenzake, wake moja Kati ya lengo la OPeration Pamoja Daima ni kuishinikiza Serikali kuboresha Daftari Hilo. Hayo yamesemwa na Mbowe, Lisu na Slaa! Kati yako wewe na Slaa ni nani Hana uelewa au nani ampe ushauri mwenzake. Ni vema tusifanye ushabiki katika mambo mazito.

Kama kweli ukielewa na una nia njema, badala ya kutuma ujumbe kwa Slaa, ungeandika kwenye Gazeti ili uishinikize Serikali kwa kuwa kazi ya kuboresha daftari ni ya Serikali na NEC yake. Aidha ungelikuwa na ujasiri wa kupostiwa kwa ID yako ningelijua Kama tuliongea la, kwa sasa hoja yako haina maana yeyote,
 

Ni vyema Mheshimiwa umetoa kauli,Natumai ujumbe umefika...
 

vuguvuvu la mabadiliko ndo kiswahili chake mdau.
 
sasa kama watu now hawajitokezi kupiga kura daftari likiboreshwa ndio watajitokeza kupiga kura !?
 
Dr Slaa, kwanza niseme hoja ya Ochutz ina maana sana kwa wakati huu. Kama mliongea au la hilo soi hoja, hoja iliyopo ni mantiki ya hoja yake.

Ninakumbuka Mzee Mwanakijiji aliandika kuhoji upigaji wa kura Mbeya vijijini ambao ulikuwa ni asilimia 30.

Mwemyekiti wa NEC aliulizwa na hakuwa na jibu kwanini watu wajiandikishe asilimia 70 halafu wapige kura asilimia 30.

Huko nyuma kulikuwa na ushahidi wa ununuzi wa shahada za kupiga kura ambao uliisha kimya kimya bila ninyi wapinzani kufutailia.

Hoja ya Otchuz ni kuwa inawezekana kabisa kampeni zenu ni effective lakini mnashindwa 'technically'.

Unakumbuka baada ya kuanza kulinda vituo wizi ulibadili sura ya matokeo kwa kiasi kikubwa.
Je, mumeangalia kwa undani nini kinaendelea na asilimia ndogo ya wapiga kura?

Sidhani kama Otchuz kuandika katika gazeti kungeweza kuwa na impact kuliko ninyi wapinzani rasmi kulizungumzia suala hilo, hivyo ni muhimu ukaiona hoja yake bila kumjua au kuwa na prejudice dhidi yake

Utakumbuka kuwa tuliwahi kuwa na mjadala na hapa tena namnukuu Mwanakijiji kwa kusema kuwa vyama viwe na madaftari ya wapiga kura wao sambamba na la wapiga kura la NEC.
Je, mnajua wanachama wenu wangapi wanakwenda kupiga kura?

Laiti mngekuwa na daftari pengine mngekuwa na ushahidi mzuri sana wa kutahmini wapi tatizo lilipo.Hivyo ndivyo wanavyofanya wenzenu katika vyama vingine huko duniani. Hakuna kosa la kisheria kuandikisha wanachama wako na kuwafahamu.

Ni muhimu ukakubali kuangalia hoja bila kutanguliza hoja za nani anajua nani hajui.

Ahsante
 
Last edited by a moderator:
Swala la kuboresha daftari la kupiga la mpiga kura ni muhimu ila swala la elimu ya uraia na Sera ni muhimu sana. Cmd inabidi iuze Sera zake kwa rika zote sio kutegemea kundi la vijana tu
 
Kwa sababu CHADEMA imepata nguvu sana baada ya uchaguzi 2010,wengi wa wanao support CDM nu vijana walio kwenye hilo rika lililotajwa kama nimemuelewa vizuri mtoa mada.
Therefore they are fighting the wrong battle!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ushauri mzuri muhimu ni elimu ya uraia watu waone ni haki ya msingi kujiandikisha na kupiga kura
 
Hayo yote anayajua, asichokijua ni kuwa ubaguzi ndani ya chama ndo THREAT kubwa. Kitila angekuwepo angefanya utafiti na kujua wapi wamekosea, lakini waliobaki wote ni propaganda uchumia tumbo.
Kwa ushauri huo unamaanisha kuwa watu wakizeeka wanaichukia CDM na kuipenda CCM, ambacho kwa mtazamo usio rasimi ni kuwa watu wanapoongezeka umri wanajitambua na kuanza kuona mbali na kutodanganyika.
Kwa mtazamo huo na ushauri CDM imepoteza dira, maana huwezi aminisha watu kuwa waliokufa, waliopoteza viparata vya kupigia kura, wagonjwa wasioweza kufika kupiga kura, wazee na vikongwe wasioweza kufika vituoni kupiga kura wote ni CDM.
Kwa kuwa waliobaki hawawezi kujitafakari, imekula CDM:wave:


 
Wewe usichoelewa nini? Ujumbe umemfikia ndio maana ametoa kauli...
Umeanza lini kuandika mitandaoni?Kujieleza kidogo tu kunakupa kazi.Ungemwambia "ujumbe umemfikia",unaposema ujumbe umefika ni kama una acknowledge kwa upande wako...kwamba ujumbe umekufikia.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…