Nilichomshauri DK WILBROAD SLAA nilipokutana nae

Dr Slaa, kwanza niseme hoja ya Ochutz ina maana sana kwa wakati huu. Kama mliongea au la hilo soi hoja, hoja iliyopo ni mantiki ya hoja yake.

Ninakumbuka Mzee Mwanakijiji aliandika kuhoji upigaji wa kura Mbeya vijijini ambao ulikuwa ni asilimia 30.

Mwemyekiti wa NEC aliulizwa na hakuwa na jibu kwanini watu wajiandikishe asilimia 70 halafu wapige kura asilimia 30.

Huko nyuma kulikuwa na ushahidi wa ununuzi wa shahada za kupiga kura ambao uliisha kimya kimya bila ninyi wapinzani kufutailia.

Hoja ya Otchuz ni kuwa inawezekana kabisa kampeni zenu ni effective lakini mnashindwa 'technically'.

Unakumbuka baada ya kuanza kulinda vituo wizi ulibadili sura ya matokeo kwa kiasi kikubwa.
Je, mumeangalia kwa undani nini kinaendelea na asilimia ndogo ya wapiga kura?

Sidhani kama Otchuz kuandika katika gazeti kungeweza kuwa na impact kuliko ninyi wapinzani rasmi kulizungumzia suala hilo, hivyo ni muhimu ukaiona hoja yake bila kumjua au kuwa na prejudice dhidi yake

Utakumbuka kuwa tuliwahi kuwa na mjadala na hapa tena namnukuu Mwanakijiji kwa kusema kuwa vyama viwe na madaftari ya wapiga kura wao sambamba na la wapiga kura la NEC.
Je, mnajua wanachama wenu wangapi wanakwenda kupiga kura?

Laiti mngekuwa na daftari pengine mngekuwa na ushahidi mzuri sana wa kutahmini wapi tatizo lilipo.Hivyo ndivyo wanavyofanya wenzenu katika vyama vingine huko duniani. Hakuna kosa la kisheria kuandikisha wanachama wako na kuwafahamu.

Ni muhimu ukakubali kuangalia hoja bila kutanguliza hoja za nani anajua nani hajui.

Ahsante

Well said brother.. tatizo viongozi wa CHADEMA hawapendi kukosolewa. ukiwakosoa tu,unaonekana mpinzani. Kumbe wakati mwingine mtu unakuwa na nia nzuri tu.
 
Last edited by a moderator:
Mbowe amemharibu sana Dr Slaa hakua hivyo nyuma

"Serikali ya CCM inajenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Ulaya"-Dr Slaa
 
Ochutz,
Kwa bahati mbaya huna ujasiri wa kuandika jina lako la kweli, hivyo siwezi kujua Kama kweli ulinipa ushauri au umetunga tu. Ebu jiulize katika akili ya kawaida, Mimi na wewe ( au Chadema) nani angelimshauri mwenzake, wake moja Kati ya lengo la OPeration Pamoja Daima ni kuishinikiza Serikali kuboresha Daftari Hilo. Hayo yamesemwa na Mbowe, Lisu na Slaa! Kati yako wewe na Slaa ni nani Hana uelewa au nani ampe ushauri mwenzake. Ni vema tusifanye ushabiki katika mambo mazito.

Kama kweli ukielewa na una nia njema, badala ya kutuma ujumbe kwa Slaa, ungeandika kwenye Gazeti ili uishinikize Serikali kwa kuwa kazi ya kuboresha daftari ni ya Serikali na NEC yake. Aidha ungelikuwa na ujasiri wa kupostiwa kwa ID yako ningelijua Kama tuliongea la, kwa sasa hoja yako haina maana yeyote,
Duh, hii ni kali.

Kwanza, kwa mtu anayefuatilia kwa karibu sauti ya kimaandishi ya Dr. Slaa hawezi kuamini kama hii sauti niya kwake mwenyewe.

Pili, Kama kweli aliyeandika ni Dr. Slaa basi ninadhani anahitaji time for political reflection nje ya siasa hata kwa mwezi mmoja ili apate muda wa kuzijongea fikra, hekima na busara katika kukabiliana na misukosuko ya kisiasa nchini. You seem to be angry for no reason!.

Sijaona kosa la mleta mada hata kidogo hasa ikichukuliwa kuwa ushauri wa kisiasa ni jukumu la wanachama wote wa chama kwa chama chao kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ambapo Dr. Slaa ndiye mtendaji Mkuu wa CHADEMA. Hoja hapa ni ushauri kwa faida ya chama na siyo jina la mleta ushauri hasa ikichukuliwa kuwa, mleta mada aliishatoa ushauri kupitia njia mbadala za chama kikatiba.

Kiongozi mzuri ni yule anayesikiliza kwa makini watu wake wanasema nini lakini siyo lazima ayafanyie kazi yale yote anayoambiwa na watu wake linapofikia swala la implementation.

Kwa mtaji huu, ninashawishika kusema mnajenga mazingira ambayo yatawafanya wanachama wenu wawaogope hata kuwanyoshea vidole kulingana na Katiba kama ilivyoainishwa katika taratibu, kanuni, itifaki na miongozo ya chama. Kama ushauri kwa chama tu unakumbana na majibu yenye mlengo huu, itakuwaje kama ikiwa ni personal criticism. Kufukuzwa uanachama!

Yangu macho na masikio.
 
Hivi chadema wana ofisi au jamii forums ndio ofisi yao?

du hili nalo neno aiseeeeeeeeee.......ngoja kurugenzi ya habari ije hapa uone majibu yao marefu mwisho ni kuomba waunde tume....na wengine wawajibishwe sasa hapa cjui nani awajibike..............ingekuwa serekali imegaragazwa hv sasa hv matamko ya kutaka mtoto wa mkulipa kuchapa lapa tungeyasikia.............lakini kibabu haguswi japo chama kinaporomoka mikononi mwake aiseeeeeeeeeeeeeee...chopa 3...................kata 3.......bado jamaa anastahili kuwa mtendaji mkuu wa chama cha ukombozi na ukombozi umetabiliwa next year!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
sela za cdm ndo mbovu watu wamestuka. Sela za ubaguz na umimi haziwezi kunusuru chama. Wajipange kisela tu

Watu wapi?suala hapa ni kuboresha daftari la wapiga kura na si bla bla nyingine.ccm wanalijua hilo na ndio maana hawataki kwa makusudi kuruhusu tume kuliboresha ili kuingiza kizazi kipya na watu wenye uelewa kuhusu madhambi ya ccm na ubakaji wa demokrasia nchini.
Badala yake inafurahia watu kama wewe unayeshindwa hata kujua neno sera na badala yake unaita sela
 
Ukweli Dr slaa ni miongoni mwa wanasiasa ambao mimi nawakubali sana hapa Tz pamoja na Tundu Lissu. Dr slaa anajua kujenga hoja, pia anatetea maslahi ya wanyonge kwa dhati. Kuhusu kushindwa uchaguzi mdogo wa udiwani, kuna mambo mengi yamechangia na ambayo yako nje ya uwezo wa Dr na chadema kwa ujumla. Suala la daftari la wapiga kura ni dosari ambayo chadema walisha ilalamikia toka mwanzo. Kuhusu polisi kutumika kutisha wapiga kura ni kawaida ya chama tawala uliza Mh.Wenje, Hiness kama sio nguvu ya umma ubunge wasinge upata. Pia kuna haja ya chadema kuweka nguvu vijijini ambako ndio ngome kuu ya ccm. Dr slaa ajipange tuna mtegemea sana wataka mabadiliko, asichoke kamanda wetu.
 
Duh, hii ni kali.

Kwanza, kwa mtu anayefuatilia kwa karibu sauti ya kimaandishi ya Dr. Slaa hawezi kuamini kama hii sauti niya kwake mwenyewe.

Pili, Kama kweli aliyeandika ni Dr. Slaa basi ninadhani anahitaji time for political reflection nje ya siasa hata kwa mwezi mmoja ili apate muda wa kuzijongea fikra, hekima na busara katika kukabiliana na misukosuko ya kisiasa nchini. You seem to be angry for no reason!.

Sijaona kosa la mleta mada hata kidogo hasa ikichukuliwa kuwa ushauri wa kisiasa ni jukumu la wanachama wote wa chama kwa chama chao kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ambapo Dr. Slaa ndiye mtendaji Mkuu wa CHADEMA. Hoja hapa ni ushauri kwa faida ya chama na siyo jina la mleta ushauri hasa ikichukuliwa kuwa, mleta mada aliishatoa ushauri kupitia njia mbadala za chama kikatiba.

Kiongozi mzuri ni yule anayesikiliza kwa makini watu wake wanasema nini lakini siyo lazima ayafanyie kazi yale yote anayoambiwa na watu wake linapofikia swala la implementation.

Kwa mtaji huu, ninashawishika kusema mnajenga mazingira ambayo yatawafanya wanachama wenu wawaogope hata kuwanyoshea vidole kulingana na Katiba kama ilivyoainishwa katika taratibu, kanuni, itifaki na miongozo ya chama. Kama ushauri kwa chama tu unakumbana na majibu yenye mlengo huu, itakuwaje kama ikiwa ni personal criticism. Kufukuzwa uanachama!

Yangu macho na masikio.

Well said brother...! inawezekana kweli kuna baadhi ya viongozi wakuu CHADEMA,hawapendi kabisa kushauriwa/kukosolewa. Majibu aliyotoa Dr Slaa yana reflect hilo.
 
Ochutz,
Kwa bahati mbaya huna ujasiri wa kuandika jina lako la kweli, hivyo siwezi kujua Kama kweli ulinipa ushauri au umetunga tu. Ebu jiulize katika akili ya kawaida, Mimi na wewe ( au Chadema) nani angelimshauri mwenzake, wake moja Kati ya lengo la OPeration Pamoja Daima ni kuishinikiza Serikali kuboresha Daftari Hilo. Hayo yamesemwa na Mbowe, Lisu na Slaa! Kati yako wewe na Slaa ni nani Hana uelewa au nani ampe ushauri mwenzake. Ni vema tusifanye ushabiki katika mambo mazito.

Kama kweli ukielewa na una nia njema, badala ya kutuma ujumbe kwa Slaa, ungeandika kwenye Gazeti ili uishinikize Serikali kwa kuwa kazi ya kuboresha daftari ni ya Serikali na NEC yake. Aidha ungelikuwa na ujasiri wa kupostiwa kwa ID yako ningelijua Kama tuliongea la, kwa sasa hoja yako haina maana yeyote,

Dr.W.Slaa

Inawezekana wewe unaulewa mkubwa kuzidi pro-Chadema wote lakini ujuaji wako na uelewa wako ndiyo umeipa Chadema viti vitatu vya udiwani.

Kama mnalalamika watu hawajitokezi kupiga kura hata hilo daftari likiboreshwa watu ndiyo watajitokeza.

Majibu yako yamejaa kibri na dharau.
 
Leo nimekubaliana na wewe 100/100. Sidhani kama hawa watu huwa wanaelewana katika vikao vyao vya ndani kama picha tunaoonyeshwa tulio nje ni hiyo...
 
Last edited by a moderator:
Itafika kipindi wapiga kura watakuwa milioni moja tu

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Ochutz,
Kwa bahati mbaya huna ujasiri wa kuandika jina lako la kweli, hivyo siwezi kujua Kama kweli ulinipa ushauri au umetunga tu. Ebu jiulize katika akili ya kawaida, Mimi na wewe ( au Chadema) nani angelimshauri mwenzake, wake moja Kati ya lengo la OPeration Pamoja Daima ni kuishinikiza Serikali kuboresha Daftari Hilo. Hayo yamesemwa na Mbowe, Lisu na Slaa! Kati yako wewe na Slaa ni nani Hana uelewa au nani ampe ushauri mwenzake. Ni vema tusifanye ushabiki katika mambo mazito.

Kama kweli ukielewa na una nia njema, badala ya kutuma ujumbe kwa Slaa, ungeandika kwenye Gazeti ili uishinikize Serikali kwa kuwa kazi ya kuboresha daftari ni ya Serikali na NEC yake. Aidha ungelikuwa na ujasiri wa kupostiwa kwa ID yako ningelijua Kama tuliongea la, kwa sasa hoja yako haina maana yeyote,

Mkuu slaa,
umma unahitaji majibu sahihi ni kwa nini mmeangukia pua kwa kuambulia kata 3 tu? Gharama zote hizo mlizotumia,mlikuwa mnafanya nini? Sasa umeamini kuwa mzimu wa kijana wako zitto unakitesa chama? Soma maneno ya kitila baada ya 23 bila kwamba ccm inastawi, chadema inadidimia huku cuf inapotea yafanyie kazi
 
Ochutz,
Kwa bahati mbaya huna ujasiri wa kuandika jina lako la kweli, hivyo siwezi kujua Kama kweli ulinipa ushauri au umetunga tu. Ebu jiulize katika akili ya kawaida, Mimi na wewe ( au Chadema) nani angelimshauri mwenzake, wake moja Kati ya lengo la OPeration Pamoja Daima ni kuishinikiza Serikali kuboresha Daftari Hilo. Hayo yamesemwa na Mbowe, Lisu na Slaa! Kati yako wewe na Slaa ni nani Hana uelewa au nani ampe ushauri mwenzake. Ni vema tusifanye ushabiki katika mambo mazito.

Kama kweli ukielewa na una nia njema, badala ya kutuma ujumbe kwa Slaa, ungeandika kwenye Gazeti ili uishinikize Serikali kwa kuwa kazi ya kuboresha daftari ni ya Serikali na NEC yake. Aidha ungelikuwa na ujasiri wa kupostiwa kwa ID yako ningelijua Kama tuliongea la, kwa sasa hoja yako haina maana yeyote,
Wakati mwingine huwa nakubaliana na logic yako mzee, pamoja na kwamba haiingozei CDM afya wala shibe!
 
Well said brother...! inawezekana kweli kuna baadhi ya viongozi wakuu CHADEMA,hawapendi kabisa kushauriwa/kukosolewa. Majibu aliyotoa Dr Slaa yana reflect hilo.
Mimi yamenishangaza sana mpaka nikaanza kuisikiliza sauti ya maandishi yake angalau nijihakikishe kama ni yeye aliyeandika hiyo comment.

Bado siamini kama ni yeye pamoja na majibu kutoka kupitia Verfied User ya jina lake.

Inashangaza na kusikitisha sana kwa vile yeye ni kiongozi mkuu wa chama chenye wanachama wenye fikra na mitazamo tofauti katika kuyajongea mambo mbali mbali ya ndani na nje ya chama.
 
Shida ni kwamba, ukutaja chadema unakuwa umetaja watu. Wenye chama wanajua kabisa kuwa ili washinde lzm wao ndo waende kuratibu mambo.

Ccm wanatumia kwa kiasi kikubwa wenyeji wakati chadema hutumia watu toka makao makuu. Kila wanapotangaza kugatua madara yanaishia vikaoni tu kwani wale wawekezaji wanaogopa kuyumba kiuchumi.

Au tuelezane, tangu wagatue madaraka, ni jimbo gani limepata mgao wa pesa kwa ajili ya kujijenga? Kwa nini hizo pesa za chopa zisipelekwe majimboni watu wakafanya kazi? Wala msitafte sababu nyingine wkt za wazi mnazijua na mnaziona.

Mbona ccm viongozi wa kitaifa wanawaamini watu wao mikoani ninyj vp?
 
Back
Top Bottom