Nilichokitafuta nimekipata!!!!!!!!



umeona eeh yaani hapa mwanamke anaambiwa ajipambe,apendeze nyumba sijui iwe safi mda wote as hayo yote alikuwa hayafanyi kabla ya kuchetiwa, ni kazi kuolewa aisee ni kama unatakiwa kuishi kama katuni ili umfurahishe mme hata akikuuzi
 
Pole mamii, ndio ndoa zetu hizi za kisasa zilivyo, binafsi napata ugumu kwamba hata ukimsamehe, huyo secretary wako ofisi moja, duh hapo sijui kama ni kweli wataachana.

Huu ujinga mi ndo ulishaganishinda, yanini malumbano, yanini maneno, najiweka pembeni naepusha msongamano
 
umeona eeh yaani hapa mwanamke anaambiwa ajipambe,apendeze nyumba sijui iwe safi mda wote as hayo yote alikuwa hayafanyi kabla ya kuchetiwa, ni kazi kuolewa aisee ni kama unatakiwa kuishi kama katuni ili umfurahishe mme hata akikuuzi

Unajua hii hali inawakatisha tamaa mabinti wengi wakitaka kuolewa maana wanaume kwenye ndoa tumekuwa wasumbufu mno.Cha kushangaza utakuta huyu binti wakati anatokewa jamaa lilitoa hadi machozi limpate kwa kweli ifike point tuzikane hizi tabia ili madada zetu wawe na amani ndoani na mahusiano kwa ujumla.
 
Billie bora ma bro umeliona hili manake kule kwenye uzi wangu wa wanaume tupeni majibu wametuzodoa sana wakidai wanawake ndo wabaya ndo maana hawawez kuomba samahani tena wanadai wao ni wababa so samahani sio kabisa ila jiulize kweli ingekuwa ni mimi leo hii Kaizer kanifumania kisha kaleta huu uzi hapa ingekuwaje?

sisi ama mimi kama mwanamke nimempa option ya kukaa kimya na kusamehe kwa kujua kabisa mwanamke anatakiwa kuwa jasiri na hodari pia anatakiwa kuwa mtu mwenye nia ya dhati hasa katika kuitunza familia yake. Tukisema tuondoke pia twaweza ila watoto jamani wanatuumiza, istoshe nini kitakachopima hekima ya mama kama akishindwa kukabili magumu yampatayo? nini kinachomtambulisha mama kama nguzo ya familia asipokuwa jasiri? nini kinachopanda upendo na kueka shina la amani na furaha kama si ujasiri wa mama na uvumilivu wake.?

wanawake wenzangu men are our spouses na sisi tusimamie kwenye misingi ya uanamke tutaveshwa taji siku ya mwisho nawaambia ukweli, wao waacheni wawe kama watakavyo ila mwisho wa siku ataikumbuka hekima yako, uvumilivu na upendo wako na ndipo utakapo jidai kwamba uliyalipa haya yote kwa ajili ya familia yenye umoja na amani na upendo.
 
Last edited by a moderator:
umeona eeh yaani hapa mwanamke anaambiwa ajipambe,apendeze nyumba sijui iwe safi mda wote as hayo yote alikuwa hayafanyi kabla ya kuchetiwa, ni kazi kuolewa aisee ni kama unatakiwa kuishi kama katuni ili umfurahishe mme hata akikuuzi
marrykate haambiwi afanye hayo kwasababu alikuwa hayafanyi hapana, ila anaambiwa kwasababu panapo kosa kama hili mwanaum yyte dunian atatafuta weak point ya mkewe ili aweze kuitumia kama kigezo. kama umeolewa nafikiri utayajua haya niyasemayo.

uliza walio pitia magumu kwenye ndoa mwanaume atakuja atafute hata kitoto cha sisimiz tu ndani aanze kuwaka na wewe mbona wewe mchafu hivi na vile muda wote kunichunguza tu kwanza nenda kwenu kajifunze maisha, yaani this is the true picture ya wanaume wa kiafrika hata kama amesh ulaya miaka 100.

kumbuka pia huyu mama kwa kujikeep busy na kazi za ndani mwake ndipo anapopunguza mawazo na ndipo apatapo relief ila ukisema atoke akaanze kuhangaika na kesi za kijinga atakufa kwa msongo wa mawazo.

asikudanganye mtu ndoa kama ndoa yaani haiana phd wala prof. bali inahekima tu tena ya kimungu. ukileta ubabe mwisho wa siku unaisambaratisha familia nzima na kujenga chuki miongoni mwa watoto.
 
Last edited by a moderator:
Huwezi kufanya investigation yote hiyo bila kua na mpango maalum. I think ulisema: Sichukui uamuzi wowote hadi niwe na uhakika. Ikiwa sio kweli nitashukuru Mungu na ikiwa ni kweli nita.... well, upo katika hiiyo hypothesis where ni ukweli. Chukua hatua.

Some would discuss it with him, make sure it doesn't happen again (I wonder how), forgive and forget. Some would just pack and leave. What is your personnal conviction on cheating? Ni vigumu sana kukuelekeza kipi cha kufanya sababu hatujui kwanini uliolewa, nini mtzamo wako kuhusu cheating, mazingira yenu yamekaaje (watoto/familia etc).

All we can do ni kukupa pole na kukupa mitazamo yetu, but ultimately uamuzi ni wako sababu ukweli wa maisha yenu unaujua wewe peke yako. Try discussing it with somebody who knows your couple well (wazazi, ndugu, family friend, your friends or his etc)
Pole sana.
 
Pole sana kweli ndoa ina mitihani, kwa sisi ambao hatujaingia hadi tunaogopa. We usiendelee kumuuliza asije akachukua maamuzi magumu si unajua mapenzi na huyo secretary wake hujui atampa ushauri gani asije akawa anatamani hata ufe ili aolewe yeye. We endelea na shughuli zako kama kawaida, mpikie, akirudi mpokee like nothing happened ataogopa sana na atashindwa kuelewa msimamo wako itabidi aweke wazi.
pia hiyo simu yako yenye ushahidi uifiche mbali sana na umshirikishe mama yako pia incase of anything ajue anakusaidiaje.
 

Na wewe jaribu wa pembeni kama yeye
 
Kwanza nakupa pole

Pili nakupa pongezi kwa shughuli nzuri ulofanya ya u FBI.

Achana na hao wanaokubeza kuwa uliyataka...wanawake wote makini tunafanya upelelezi whenever needed!
Hilo litakusaidia kuamua mstakabadhi wa maisha yako ya ndoa...wengine kwa kupeleleza kwetu tuliweza rudisha waume zetu kwenye mstari kabla hawajanogewa na kuzaa nje.

Najua huko confused na itachukua muda kwa akili kufanya kazi...ila siri pekee ya situation kama hiyo ni kuamua MWENYEWE bila kushinikizwa na mtu.

Yeye ameuchuna hajasema kitu na wewe kaaa kimya. Najua mumeo anajuta na amekosa maneno ya kukwambia ndio maana yuko kimya. Mpe muda afanye maamuzi na si kukurupuka. Kwa experience yangu mkilianzisha sasa hivi mnaweza kutukanana matusi ambayo mtajajutia maisha yenu yote...sababu hasira haina adabu.

The fact remains...wewe ni MTAMU zaidi ya huyo wa nje ...angekuwa MTAMU angekutoa ndani...hata ukiamua kuondoka bado hawezi kutamba kuwa amekutoa ndani...ni wewe umeamua kuwa you are better without him. Wanaume wana maneno mengi tu ya uongo na si kila wanachosema wana maanisha...wewe ni MTAMU dear...huyo ni wa mapozeo tu.

Narudia hukufanya vibaya kumpeleleza mumeo...Mungu amekunusuru na kitu kwa kuufahamu ukweli...na ukweli utakuweka huru.
 
BHULULU, Umesema sawa, Atakaa pembeni mara ngapi?????Atafute Suluhu kwanza kabla ya kuamua kumkimbia Labda kama atasema hataolewa tena au hatakua na uhusiano na kiumbe yeyote Duniani
 
Last edited by a moderator:
Wanaume kama wewe ni wachache sana Billie.

Yaani mwanaume akichiti ukajua unaambiwa kiherehere...mwanamke akichiti sijuhi azae nje utaona comments zinazomkashifu kuanzia kwa wanaume mpaka wanawake wenzie. Kweli sijuhi lini tutaacha u pori pori.
 

Ewwwh! finaly someone with wisdom and courage talks...MUngu akubariki sana, wengi wameishia kumwambia avumilie, sijui nini... We dada wewe binafsi ndiye mwamuzi, ukiwa moyo wako hauwezi kulivumilia alilotenda au analotenda (maana hujui kama ataacha) ni bora uepuke msongamano. Mwombe Mungu sana akupe amani
 
jamani wanaume si vzr kuwasema wanawake zenu kwa vimada, pole sana bibiye, kwa vile yeye kauchuna na wewe uchune usimuulize kitu siku akitaka kuyaongea yaongeeni ila natumaini utamsamehe kama atakiri ukosa na kutorudia kosa, next time usishike simu ya mumeo, iyone kama sumu ona sasa unajipa ma stress bure.
 

shida iko wapi... umetaka kujua how bad upo kwenye mapenzi ukajua

usiingilie yasiyokuhusu aisee

Mimi nimeoa, ila hat siku moja sintopenda kujua ananipimaje, kwani sikuoa kupimana wala kuchunguzana

ILA NIKIPATA SABABU YA KUMUACHA SITAULIZA MTU JF
 
Ndo maana mimi huwa sipendi kutuma meseji, angepiga hata yasingemkuta haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…