Nilichokishuhudia Romania Dec/1989

Nilichokishuhudia Romania Dec/1989

Mara chatu mara ng'ombe mara mzungu mara Bucharest mara Moldova mara godoro yaani kila ukiunganisha dots unapata maluelue tu..
Wewe kweli kilaza yaani ktk story yote iyo ndo umeambulia hayo tu??

Pole yako kwa kupakatwa na chogo
 
Nilizaliwa Magu mkoani Mwanza,baadaye wazazi wangu walihamia ktk kijiji kimoja ( jina nahifadhi) kilichopo karibia na mbuga ya wanyama ya Serengeti.
Lengo la kuhamia huko ilikuwa ni kufuata malisho bora ya ng'ombe ambao wazazi wangu walikuwa wakifuga.
Siku moja mwaka 1987 nikiwa darasa la kwanza wakati huo,nakumbuka ilikuwa siku ya jmamosi nikiwa na mdogo wangu na kaka yangu tukichunga ng'ombe majira ya mchana tuliona gari aina ya Land Rover kwa mbali likiwa limesimama na nje ya hilo gari tuliona wazungu wawili na mtu mmoja mweusi.
Tuliamua kusogea karibia na hilo gari na kuwaacha ng'ombe wakichunga peke yao,tulipofika tuliwaona hao wazungu mwanamke na mwanaume wenye umri wa makamo hivi,wakiwa na yule mtu mweusi wakibadili tairi ya gari.
Yule mama wa kizungu muda wote alikuwa akilizunguka gari kama mtu anayetafuta kitu kilichopotea,na yule mtu mweusi nilimwona akiinama mara nyingi kuchungulia kwenye uvungu wa gari.
Baadaye mita kadhaa kutoka kwenye lile gari nilimwona chatu akiwa amelala kwenye kichaka kidogo ambacho yule mama wa kizungu alikuwa anaelekea huko,nilipiga kelele kwa lugha ya kisukuma kumsihi yule mama asiendelee kwenda huko,kelele zangu zilimgutua akasimama,kisha nikamwonyesha kwa ishara yule nyoka.
Alipomwona alikimbia kurudi haraka,alikuwa anajua kiswahili kidogo,akanifuata na kuniuliza jina nikamwambia,kisha akaniuliza kwanini sijavaa viatu halafu natembea porini?
Nikamjibu kuwa Baba hajaninunulia,akamwita kaka yangu na kumwomba amwelekeze kwetu.
Hiyo ni story ndefu mno.

BACK TO THE TOPIC

Baadaye wazungu hao walinipeleka Australia na nikasomea huko,kisha mama akawa anashinda akilia akitaka nirudi nyumbani,na hivyo ikabidi wanikatishe masomo ili nirudi nyumbani.
Siku narudi nyumbani Tanzania walisema twende Bucharest mji mkuu wa Romania tukale Xmas huko kisha ndo nirudi Tanzania.
Tuliwasili Bucharest majira ya jioni sikumbuki tarehe,na tulifikia kwenye Hotel moja iliyokuwepo nje kidogo ya jiji la Bucharest, mimi nilikuwa nikilala chumba cha peke yangu,siku nne tangu tuwasili hapo hali ya jiji ilibadilika ghafla,tukaanza kuona police wenye silaha wakiwa wamezagaa kila kona ya jiji hilo, siku hiyo nakumbuka tulikuwa tukila chakula cha mchana yule mama akasema tuondoke haraka turudi kwanza Australia kabla sijarudi nyumbani maana hali ya usalama ilikuwa imeanza kutoweka kulikuwa na vurugu za kisiasa baada ya waandamanaji wengi kutoweka na wengine kuwekwa jela.
Waliafiki tuanze safari siku hiyo hiyo,wakati tukitoka nje ya Hotel tuliona kundi kubwa la vijana wakiwa wamefungwa pingu na police na wakipigwa kikatili mno (usiombe kuona ni bora usimuliwe) .
Nakumbuka Dada mmoja aliuawa kwa kupigwa rungu kichwani ilihali akiwa kabeba mtoto mchanga kifuani.
Tulirudi ndani ya Hotel, kwa sababu hapakuwa na sehemu ya kupita tena,dakika chache baadaye tulianza kusikia milio ya risasi ikirindima bila kukoma,tulipochungulia dirishani tuliona wanajeshi wamezagaa na watu wakianguka chini na kutoa damu nyingi huku risasi zikilia.
Kilichonishangaza kila sekunde idadi ya watu ndo ilizidi kuwa kubwa, tukaona vifaru vya jeshi vikiwakimbiza watu na kuwagonga kama wanyama.
Dakika chache baadaye ile Hotel tuliyokuwemo ikavamiwa na jeshi na sote tukatolewa nje,alikuwepo padri mmoja mule tukashuhudia akipigwa risasi ya kichwa na damu kutapakaa eneo lote.
Hii kamwe haitanitoka maishani mwangu,tulikimbia kutoka nje tusijue tunakoelekea,na kisha tukarudi tena ndani na kujificha chooni hadi usiku wa manane tuliposikia mlango wa ukigongwa.
Alikuwa ni mwanajeshi akasema nyie wageni kimbieni kwenye balozi zenu na kama ni waandishi msijaribu kupiga picha yoyote mtapigwa risasi.
Akatuingiza kwenye gari la jeshi kisha akaomba Pesa au la atutelekeze katikati ya machafuko ili tuuawe,sikumbuki alipewa kiasi gani maana niliona akihesabiwa dola.
Aliendesha hadi sehemu moja tusiyoijua kisha akasema hiyo ni US Embassy nendeni hapo mtakuwa salama,tulikuwa zaidi ya kumi raia wa mataifa mbalimbali.
Kwa mbali kwenye taa tuliona wanajeshi wakiwa wamezingira jengo la US Embassy, yule mzee akapiga kelele "We need your help American soldiers" taa Kali ghafla ikamulika eneo tulilokuwepo halafu askari mmoja mwenye silaha akatufuata,na kuanza kuhoji maswali,
Nikawaona wakimwonyesha passport zao,akatupatia ishara tumfuate.
Tulinusurika kwa kupewa hifadhi hapo, tulilala chini kwenye magodoro safi na blanket, asubuhi tukapewa chai na tukawa tunaangalia matukio ya mapinduzi kwenye TV.
Dikteta Nicolae Ceausescu alipigwa risasi yeye na mkewe Helen baada ya jeshi kumgeuka.
Hali ilipotulia tuliondoka Romania kupitia Moldova.
Mpumbavu utamjua tu kwa kutunga hadithi za alinacha.
 
Vijana wa "ulipo tupo" bado hamkubari kuwa mlishindwa uchaguzi wa 2015,sasa mnawaza mapinduzi ya kwenye mtandao.
Jipangeni 2019 uchaguzi wa serikali za mitaa 2020 uchaguzi mkuu. Nawakumbusha tu.
Umeletwa na Kagame?? Mbona Kiswahili kinakupa taabu??
 
Nina wasi wasi na hiyo story yako ya kusoma Australia. My son drink(s) water tu imekushinda kuandika sahihi!
Wewe ndiyo una matatizo, Syntax unayotaka kuileta hapa ni kwa mjibu wa uelewa wako. Hajakosea, My Son Drink Water (ni amri), My Son Drinks Water unayoitaka wewe (ni kauli taarifa).
Tofautisha.
 
Ni hatari sana... Mambo kama hayo ndiyo yanaoendelea kwenye nchi nyingi za Africa...


Cc: mahondaw
 
Jana kuna uzi mmoja nilikwambia wewe ni MPUMBAVU,,. na naendelea kukukumbusha kuwa wewe ni MPUMBAVU. Unapoteza muda wako mwingi bure, huko Tanzania ya uhalisia mbali na mitandaoni maisha yanaendelea kama kawaida. Ukija kushtuka kuwa unapoteza muda wako bure kuandika UPUMBAVU wako itakuwa TOO LATE.
Nasimulia nilichokiona Romania na nilivyonusurika kuuawa na hatimaye kurudi nyumbani salama,wewe unakuja hapa na kuniita mimi ni mpumbavu,sasa kwanini unapoteza muda wako kusoma uzi wa mpumbavu?
By the way,unanijua mimi na maisha yangu wewe juha?
Unadhani nina dhiki? Mimi siyo hayawani kama wewe boya,ubongo wako umejaa kamasi tupu,ukila ukashiba ukaweka pocket money mfukoni,unaona nchi ipo pazuri sana,una tofauti gani na mbwa koko wewe? Hujui kuhusu wajane,yatima,wagonjwa,wafungwa na watoto wa mitaani wanaoteseka,juha kabisa wewe achana na mimi.
 
"----itakuwa TOOLATE" kwa kitu gani? Yaani ndio hivyo unamtishia sio?

Watu wote wanaowaonea wenzao hudhani wao ndio kila kitu na kwamba hakuna lolote linaloweza likawatokea wao.
Wanapoona wamezungukwa na kila aina ya ulinzi, hujisahaulisha kabisa na kudhani wao hayawezi yakawapata yanayowapata madikteta wenzao. Usidhani kwamba Charchescu alikuwa hajiamini hivyo hivyo kama unavyoamini wewe na hao wenzako.

Haya yote hatuyaombei yatokee hapa kwetu; lakini kuna kiasi cha uvumilivu. Watu wanaweza wakachoka na uvumilivu ukawaishia.
Kwa nini twende huko kote, na kumbe waonevu wanaweza kuacha njia zao za uonevu? Kwani ni nini watakikosa?
Mkuu huyo jamaa mjinga sana,sasa sijui kilichomuuma kwenye story yangu ni kipi,muda utaongea siku watapofurushwa madarakani
 
Wewe ndiyo una matatizo, Syntax unayotaka kuileta hapa ni kwa mjibu wa uelewa wako. Hajakosea, My Son Drink Water (ni amri), My Son Drinks Water unayoitaka wewe (ni kauli taarifa).
Tofautisha.
Ahsante mkuu kwa kumwelewesha huyo kilaza wa lugha
 
Mpumbavu utamjua tu kwa kutunga hadithi za alinacha.
Kwako ni hadithi kwa sababu you have been deeply destructed by poverty,you're a scrub that astonishes success, si ajabu hata Kenya tu hujawahi kwenda,leo kusikia Australia na Romania wakati unawaza kuzamia meli ni lazima useme hii ni hadithi,pole sana ndugu umaskini mbaya mno.
 
Now i understand why you always swim with the tide of whites.
Magufuli wanyooshe kabisa watuletee stori nyingine nyingi za kujifariji.
Any ufipa member with Julius caeser's story you may have it presented please.
How does my story relate by Ufipa?kwanini mkisikia Dikteta your heart beats move rapidly?
 
Back
Top Bottom