My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,930
- 13,333
Nilizaliwa Magu mkoani Mwanza,baadaye wazazi wangu walihamia ktk kijiji kimoja ( jina nahifadhi) kilichopo karibia na mbuga ya wanyama ya Serengeti.
Lengo la kuhamia huko ilikuwa ni kufuata malisho bora ya ng'ombe ambao wazazi wangu walikuwa wakifuga.
Siku moja mwaka 1987 nikiwa darasa la kwanza wakati huo,nakumbuka ilikuwa siku ya jmamosi nikiwa na mdogo wangu na kaka yangu tukichunga ng'ombe majira ya mchana tuliona gari aina ya Land Rover kwa mbali likiwa limesimama na nje ya hilo gari tuliona wazungu wawili na mtu mmoja mweusi.
Tuliamua kusogea karibia na hilo gari na kuwaacha ng'ombe wakichunga peke yao,tulipofika tuliwaona hao wazungu mwanamke na mwanaume wenye umri wa makamo hivi,wakiwa na yule mtu mweusi wakibadili tairi ya gari.
Yule mama wa kizungu muda wote alikuwa akilizunguka gari kama mtu anayetafuta kitu kilichopotea,na yule mtu mweusi nilimwona akiinama mara nyingi kuchungulia kwenye uvungu wa gari.
Baadaye mita kadhaa kutoka kwenye lile gari nilimwona chatu akiwa amelala kwenye kichaka kidogo ambacho yule mama wa kizungu alikuwa anaelekea huko,nilipiga kelele kwa lugha ya kisukuma kumsihi yule mama asiendelee kwenda huko,kelele zangu zilimgutua akasimama,kisha nikamwonyesha kwa ishara yule nyoka.
Alipomwona alikimbia kurudi haraka,alikuwa anajua kiswahili kidogo,akanifuata na kuniuliza jina nikamwambia,kisha akaniuliza kwanini sijavaa viatu halafu natembea porini?
Nikamjibu kuwa Baba hajaninunulia,akamwita kaka yangu na kumwomba amwelekeze kwetu.
Hiyo ni story ndefu mno.
BACK TO THE TOPIC
Baadaye wazungu hao walinipeleka Australia na nikasomea huko,kisha mama akawa anashinda akilia akitaka nirudi nyumbani,na hivyo ikabidi wanikatishe masomo ili nirudi nyumbani.
Siku narudi nyumbani Tanzania walisema twende Bucharest mji mkuu wa Romania tukale Xmas huko kisha ndo nirudi Tanzania.
Tuliwasili Bucharest majira ya jioni sikumbuki tarehe,na tulifikia kwenye Hotel moja iliyokuwepo nje kidogo ya jiji la Bucharest, mimi nilikuwa nikilala chumba cha peke yangu,siku nne tangu tuwasili hapo hali ya jiji ilibadilika ghafla,tukaanza kuona police wenye silaha wakiwa wamezagaa kila kona ya jiji hilo, siku hiyo nakumbuka tulikuwa tukila chakula cha mchana yule mama akasema tuondoke haraka turudi kwanza Australia kabla sijarudi nyumbani maana hali ya usalama ilikuwa imeanza kutoweka kulikuwa na vurugu za kisiasa baada ya waandamanaji wengi kutoweka na wengine kuwekwa jela.
Waliafiki tuanze safari siku hiyo hiyo,wakati tukitoka nje ya Hotel tuliona kundi kubwa la vijana wakiwa wamefungwa pingu na police na wakipigwa kikatili mno (usiombe kuona ni bora usimuliwe) .
Nakumbuka Dada mmoja aliuawa kwa kupigwa rungu kichwani ilihali akiwa kabeba mtoto mchanga kifuani.
Tulirudi ndani ya Hotel, kwa sababu hapakuwa na sehemu ya kupita tena,dakika chache baadaye tulianza kusikia milio ya risasi ikirindima bila kukoma,tulipochungulia dirishani tuliona wanajeshi wamezagaa na watu wakianguka chini na kutoa damu nyingi huku risasi zikilia.
Kilichonishangaza kila sekunde idadi ya watu ndo ilizidi kuwa kubwa, tukaona vifaru vya jeshi vikiwakimbiza watu na kuwagonga kama wanyama.
Dakika chache baadaye ile Hotel tuliyokuwemo ikavamiwa na jeshi na sote tukatolewa nje,alikuwepo padri mmoja mule tukashuhudia akipigwa risasi ya kichwa na damu kutapakaa eneo lote.
Hii kamwe haitanitoka maishani mwangu,tulikimbia kutoka nje tusijue tunakoelekea,na kisha tukarudi tena ndani na kujificha chooni hadi usiku wa manane tuliposikia mlango wa ukigongwa.
Alikuwa ni mwanajeshi akasema nyie wageni kimbieni kwenye balozi zenu na kama ni waandishi msijaribu kupiga picha yoyote mtapigwa risasi.
Akatuingiza kwenye gari la jeshi kisha akaomba Pesa au la atutelekeze katikati ya machafuko ili tuuawe,sikumbuki alipewa kiasi gani maana niliona akihesabiwa dola.
Aliendesha hadi sehemu moja tusiyoijua kisha akasema hiyo ni US Embassy nendeni hapo mtakuwa salama,tulikuwa zaidi ya kumi raia wa mataifa mbalimbali.
Kwa mbali kwenye taa tuliona wanajeshi wakiwa wamezingira jengo la US Embassy, yule mzee akapiga kelele "We need your help American soldiers" taa Kali ghafla ikamulika eneo tulilokuwepo halafu askari mmoja mwenye silaha akatufuata,na kuanza kuhoji maswali,
Nikawaona wakimwonyesha passport zao,akatupatia ishara tumfuate.
Tulinusurika kwa kupewa hifadhi hapo, tulilala chini kwenye magodoro safi na blanket, asubuhi tukapewa chai na tukawa tunaangalia matukio ya mapinduzi kwenye TV.
Dikteta Nicolae Ceausescu alipigwa risasi yeye na mkewe Helen baada ya jeshi kumgeuka.
Hali ilipotulia tuliondoka Romania kupitia Moldova.