Nilichokishuhudia mume wangu akifanya siamini

Nilichokishuhudia mume wangu akifanya siamini

davina

Senior Member
Joined
Jan 21, 2012
Posts
113
Reaction score
87
Naamini kwa uwezo wa Mungu mko wazima.

Napenda kuwashukuru sana kwa michango yenu ambayo huwa mnatoa humu mm ni mdau japo huwa siyo mchangiaji sana lakini siyo mara ya kwanza kuleta matatizo yangu hapa na mkanisaidia.

Kama utaweza kupitia topic zangu za nyuma utanielewa vizuri ila leo nimekuja na lingine.
Nimeolewa nina mtoto mmoja ana miaka 5 nimeolewa miaka 7 iliyopita, kipindi chote cha maisha yangu ya ndoa nimepitia mambo magumu sana kutokana na tabia ya ufataki aliyonayo mume wangu lakini mungu amenisaidia mpaka hapa nilipo.

Kama wiki 3 zilizopita kuna mtoto wa kike wa shangazi yake na mume wangu alikuja nyumbani kama kawaida huwa anakuja kutusalimia then anaondoka ila safari hii akawa amekaa sana nkamuuliza vpi unarudi au umekuja mjini kwa lengo gani akaniambia amechoka kukaa kijijini bora akae nyumbani anisaidie kazi za nyumbani nikamwambia sawa.

Tumekaa nikaona tuna shida ya mfanyakazi katika biashara yetu na yeye kwa elimu yake ndogo hiyo kazi anaiweza, basi nikamweleza mume nae akakubali tukaona kuliko akae nyumbani na kuna msichana wa kazi haina sababu, basi jana kaanza kazi na hiyo kazi anafanya hadi saa nne usiku then wanarudi na mjombaake ( yaani mume wangu).

Jana usiku saa nne nikiwa ndo nataka nijilaze kitandani nilisikia gari la mume wangu akiwa anarudi coz najua mlio wake, basi nikakaa kama dk 10 gari ipo nje nikajiuliza mbona hafungui geti aingize gari akili ikanijia labda anaongea na simu, nikalala zangu kama dk 20 mbele bado gari ipo silent nje, nikaamka nikatoka nje nikafungua geti taratibu nilishuhudia mume wangu akikisiana na huyo mtoto wa shangazi yake.

Niliishiwa nguvu nikamsogelea kuwaangalia vizuri binti akashtuka sana akataka kukimbia akashuka kwenye gari, nikamuuliza mnafanya nini hapa akaniambia wanafanya mahesabu nikamwambia mbona giza ebu leta hilo daftari la mahesabu mnalofanyia, akababaika akamuita yule binti akamwambia leta daftari akakimbia ndani chumbani kwake akajifungia akalala, nilistaajabu sana sikuamini nilichokiona, mume wangu akaingiza gari ndani akaja chumbani jasho linamtoka sikumsemesha wala kumuuliza chochote nikalala.

Leo asubuhi nilipoamka nikamwamsha yule binti nikamwambia ajiandae arudi kwao kajiandaa nikampa nauli nikamwambia asije tena nyumbani kwangu.

Wapendwa kichwa kinaniuma na kinachoniuma siyo kuwakuta katika hali ile ila roho inaniuma mume wangu alipofikia ukiangalia yule binti ni ndugu yake wa damu kabisa ana miaka 17 tu, mume wangu ana miaka 47 mtu mzima.

Nimefikiria cha kufanya nakosa sina wa kumueleza naogopa mume wangu ni kiongozi nikisema kwa watu ni aibu natamani nifungashe niende kwanza nyumbani kwetu kwani naishi mbali na wazazi labda huyu mume atabadilika nikiondoka au nifanye nini msaada wenu jamani.
 
Amezidisha mno hadi kwa ndugu anyway jaribu kuwashirikisha ndugu wa upande wa mumeo mkae muangalie coz ukishirikisha upande wako itaonekana ni kesi. Tunajifaham
 
davina

na wasiwasi na huyo mtoto wa shangazi yake na kitu chengine kama mnawatoto wakubwa asije akawaliyumba bure mkapata aibu cha kufanya mwambie ampeleke huyo mtoto bweni uone nini kitakachojiri na ukisema uende nyumban ndio itakuwa uhuru wa manyani bora umeshamjua mgoni wako..
 
Last edited by a moderator:
Mh pole dad, umeolewa na cd la kiume,

kabila gani hao
kama warabu binamu ni mke.
Mh mimi nakushauri usiondoke zungumza naye na umkanye na sasa umwangalie kwa karibu zaidi.
 
Mh pole dad, umeolewa na cd la kiume,

kabila gani hao
kama warabu binamu ni mke.
Mh mimi nakushauri usiondoke zungumza naye na umkanye na sasa umwangalie kwa karibu zaidi.

siyo mwarabu
 
pole sana sikushauri uondoke lazima uipiganie ndoa yako! lara1 huwa anaushauri ila tabu mkali sana
ngoja ni pm ili niwe huru zaidi kukushauri kwa vizuri.
 
safi sana huyo mumewe kweli wakajanga....wee ameona umechoka wacha ale nyama fresh!!!
na ukiondoka jua umemfungulia mwenzio ataendelea gegeda kwa raha zake
 
Mshirikishe na Mungu,,, naamini ni ndoa takatifu, zungumza nae ktk maombi ya kweli kutoka kumoyo wako, maadam huyo mpwa keshaondoka tuliza moyo... Usijaribu kuondoka hapo nyumbani... utakuta mwenzio kahamia..... usikome kusali.... then tafuta muda muafaka zungumza nae.... usiite vikao kwanza.....ni yako lazima uyashinde...
 
Back
Top Bottom