Nilichokiona Shinyanga

MR.NOMA

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
338
502
Wakuu habari zenu,

Nimepita hapa kuwamegea kidogo mambo machache ya kustajabisha niliyoyaona wiki tatu zimepita nikiwa nimetembelea Manispaa ya Shinyanga.

Mambo yenyewe ni:-

1.Mji kuna vumbi na vimbunga vidogovidogo vyenye kasi hupita kila mara.

2.Watoto wa shule ya msingi na sekondari wanaonekana kupita wakirudi shule jioni huku wakiendesha baiskeli kwa umahiri.

3. Nimeona wamama wakiendesha baikeli kwa ustadi.

4.Nimemuona mmama wa karibu miaka 50 na kuendelea akiendesha bodaboda.

5.Baiskeli ni nyingi kuliko bodaboda na zinaitwa daladala kupanda kwa umbali ambao pikpiki itakupeleka kwa buku yenyewe unalipa tsh 300 tu.

6. Waendesha daladala hawakushushi mahala hata kama ni mlima atakukokota tu maana upo kwenye daladala.

7. Nyama ya Mbuzi choma portion ya elfu tano ni kubwa sawa na ya elf 15 huku Dar.

8.Kuna kiwanja kizuri cha kuburudika na kupata chakula jioni,ghorofa la NSSF panaitwa level 4.

9. Ukihitaji huduma ya mambo yetu yale unamwambia mhudumu wa loji/hotel anapiga simu mtu anakuja fasta, ila asubuhi unatakiwa umtoe si chini ya 30.
 
Back
Top Bottom