Pure_sapiens
JF-Expert Member
- Dec 25, 2016
- 2,202
- 2,035
Natumaini wengi wetu ni wazima wa afya na waliowagonjwa tuzidi kuwaombea kwa Mungu atawafanyia wapesi. Leo ni Ijumaa kwa sisi waislam twendeni Masjid kumwabudu Allah. Nipo safarini kwenda vocation Mtwara kwa ajiri ya weekend, safari yangu ilianza Temeke mwisho lakini kabla sijakata ticket nilipata mgongano wa mawazo kuhusu basi gani lingefaa kwa safari yangu.
Nikakata shauri nikapanda BUTI LA ZUNGU (Hyutong)ikumbukwe.Basi safari ikaanza nilibahatika kupata siti ya dirishani, muda mwingi niliutumia kuangalia mandhari ya nje huku nikisikiliza good music, tulipofika Rufiji jirani yangu akaniambia "kabla ya daraja hili tulikuwa tunatumia siku9 kuvuka kuja Dar es Salama, tunamshukuru sana mh Mkapa kwa daraja hili". Mida ya saa 6:45 tuliingia Lindi stand, Msema kweli ni mpenzi wa Mungu kusema kweli Lindi si nzuri kama wanavyodai baadhi yetu humu jukwaani. Yaani ni mji wa kizamani sana nimeshangaa sana hawana cha kujivunia may be bahari tu. Tuache hayo gari likasimama kama 9minutes tukaendelea na safari mimi nilikuwa na hamu ya kufika Mtwara kwa Dangote tu.
Tukaanza kuingia Mtwara kwa kufika mnazi mmoja na vijiji kadhaa vya Mtwara. Tulipofika madangwa nilianza kuona jengo refu ndipo nikaambiwa ni kiwanda cha cement cha Dangote. Haikuchukua muda mrefu tulifika Dangote yaani! kusema kweli ni kiwanda kikubwa sana kwa ukanda wa E/A na hata Africa, kuna raia wa nchi mbalimbali. Mida ya saa8 hivi tulifika Mtwara stand, Mtwara ipo vizuri sana pia kuna miradi mikubwa inaendelea kama vile ujenzi wa bandari kubwa ya kisasa.
Kuna maeneo mengi ya uwekezaji naona Wahindi, Wakenya Wachina wanayagombania sana, nimeshuhudia fursa mbalimbali huku Mtwara. Wachaga wazee wa fursa hawapo nyuma naona wamejazana sana utazani Ushirombo.
My take Nyinyi wamakonde msikimbilie Dar es Salaam na kuacha fursa zilizopo mkoani kwenu wenzenu wanazikimbilia mkija kushtuka kumebaki bahari tu.
Karibuni tuwashauri wenzetu wa Mtwara kuhusu mkoa wao.