Nilichokiona ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza leo

Nilichokiona ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza leo

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Posts
27,972
Reaction score
35,197
Leo nimeona maajabu, kituko, jambo la kusikitisha ambalo sikutegemea kuliona katika ofisi ya Serikali Kuu, ofisi ambayo ndio "ikulu" yetu ya Mwanza, ofisi ambayo inamwakilisha Rais.

Nimefika ofisi hiyo leo muda wa saa 5.00 asubuhi kufuatilia mambo fulani yanayohusiana na ofisi yangu ninapopatia riziki ya kila siku.

Nilipofika kwenye korido la jengo la zamani nikasikia sauti kubwa, sauti kali, matusi ya nguoni yakitokea ofisi ya masjala ya wazi/bayana (open registry), nikashuhudia watu wengi wamesimama kwenye korido hilo wanasikiliza matusi yale ambayo ama kwa hakika hayakuwa hata na "skin tight" yalikuwa makavu yakiporomoshwa kutokea ofisi hiyo ya Masjala kwa sauti kubwa.

Baadhi ya matusi hayo yalikuwa "MB.WA WEWE, MSEN.GE, YAANI WEWE NDIE UNANIFANYA NIITWE KWA MKUU WA MKOA," na matusi mengine mengi mengi machafu machafu.

Nikawapita watu waliokuwa wanasikilizia huo mziki wa matusi, nikaenda moja kwa moja hadi ofisi ya masjala kushuhudia kuna nini!!!

Oooooooooooooooops! nikakuta dada ambaye nimesikia wakimuita ASHA, ni Office Supervisor, anamtolea matusi hayo kaka ambaye ni mfungwa wa kifungo cha nje.

Mimi kama mtumishi wa umma, pia kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ya mwaka 2005, nilijisikia vibaya sana. Sikutarajia ofisi kubwa kama ile kukuta mtumishi anamtukana mwenzie matusi ya nguoni kwa sauti kubwa kama vile amapandisha mashetani!

Nikawauliza baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo, huyu Asha anaumwa au ni tabia yake? wakasema Asha ndivyo alivyo na uongozi unajua tabia zake, lakini WANAOGOPA KULOGWA!

Sasa mimi siogopi kulogwa na huyo Asha wenu, nawaomba viongozi wa mkoa, kaka Mongela, Mtweve, Rubanzibwa fuatilieni utendaji wa huyo Asha hapo Masijala sio kwa matusi hayo!

Mwisho wanaJF msiponiona hapa JF kwa muda mrefu basi mjue labda Asha kaniloga nimekufa.

Nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko
 
hilo watu wa mwanza yote wakishasikia mtu ana sifa hizo, aisee anaogopwa mpaka na watawala wa eneo hilo, niliweza shuhudia kisiwa ki1 mtu kagongwa na gari na kufa lakini sikuona ufatiliaji wowote kisa jamaa aliyemgonga na kumuua ni mganga wa kienyeji, hakuna askari wana nani aliyekwenda kisa anajulikana kuwa jamaa ni mlozi, hii tabia kanda ya ziwa wanayo sana na hasa wakishajua una sifa hizo
 
Yaani ndugu yangu, ungekuwepo ungejiuliza swali hili, "hivi ni ofisi ya serikali au nimefika bandarini kwa wabeba mizigo" mbaya zaidi alikuwa anatukana kwa sauti kubwa kiasi kwamba ofisi nyingi walikuwa wanamsikia, du! nilimhurumia yule kaka ambaye niliambiwa ni mfungwa wa kifungo cha nje.
 
Aisee hatari. Kumtukana binadamu mwenzio hivyo kisa kukumbishwa wajibu haifai
Wanasema Asha anaogopwa na staff wote, hahahhahaha, ni kama Fulani kembamba sana, vimishipa vimechomoza kila mahali. hahahahhahahah.
NIkauliza huyu Asha ni nani humu, wakasema ni office supervisor, amesoma Chuo cha Utumishi wa Umma ana Diploma ya Record Management. Jamani Asha ni hatari. shost usiponiona badi ujue Asha atakuwa kanidungua,hahahahahahah
 
ahahaaa asha ngedere kazua balaa hadi jf
naomba namba zake kuna mtu nataka nimloge
 
Hahhaha jaman shosti nakuombea ili tusipate hasara ya kukosa ubuyu zaidi. Akituma makombora yamrudie mwenyewe
Wanasema Asha anaogopwa na staff wote, hahahhahaha, ni kama Fulani kembamba sana, vimishipa vimechomoza kila mahali. hahahahhahahah.
NIkauliza huyu Asha ni nani humu, wakasema ni office supervisor, amesoma Chuo cha Utumishi wa Umma ana Diploma ya Record Management. Jamani Asha ni hatari. shost usiponiona badi ujue Asha atakuwa kanidungua,hahahahahahah
 
Wanawake wembamba ndo walivyo labda kuna mtu anampa kiburi

usisahau vya kusahau kabla kusahau hAkujakusahau wewe uliye sahau
 
Labda hatabosi wake anamwogopa
Hapo ndio nimeshangaa kwamba hivi hizi ofisi za umma kumbe bado wana abudu mambo ya utamaduni, yaani wanaogopa kumrekebisha mtumishi anayekosea eti kisa ATAWALOGA!
 
Wanawake wembamba ndo walivyo labda kuna mtu anampa kiburi

usisahau vya kusahau kabla kusahau hAkujakusahau wewe uliye sahau
mh! Asha huyu sio kabisa aisee! Sijui anajiamini nini huyu Asha
 
Sasa kwanini usiombe kumuona huyo mkuu wa mkoa ukamwambia haya mambo unayokuja kuyazungumza huku JF, kweli haya ndiyo maadili ya utumishi wa Umma?
 
Back
Top Bottom