Elections 2010 Nilichokiona kwenye mikutano ya Dr. Slaa

Mubezi

Member
Sep 27, 2010
71
23
NIMEHUDHURIA mikutano ya kampeni za awamu ya pili za mgombea urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa. Kwa nguvu za kampuni ya gazeti hili la Raia Mwema, nimefika katika mikutano ya Ifakara mjini, Lupiro-Mahenge, Songea Mjini, Njombe-Mjini, na Iringa Mjini.

Ni baadhi ya mikutano tu. Kwa kuzingatia mikutano hiyo, nitajadili umuhimu wa nilichokiona ambacho kwa wengine hakionekani au hawataki kukiona na zaidi, hawataki kutoa tafsiri ya kimantiki.

Tangu kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu 2010, vyombo vya habari vimekuwa vikizungumzia wingi au uchache wa watu katika mikutano ya wagombea husika.

Ni kawaida kwa mwandishi wa habari gazetini kuandika mkutano ulihudhuriwa na maelfu au mamia ya wananchi.

Ni kawaida sasa kwa mwandishi wa habari wa televisheni kuonyesha picha za wingi wa watu waliohudhuria. Kwa kadri ya mwenendo wa kampeni, waandishi wamekuwa wakilenga mambo matatu makubwa.

Kwanza ni ujumbe wa mgombea husika kwa watu wanaomsikiliza. Pili, wingi wa watu. Tatu ikibidi vituko au mbwembwe zilizojiri eneo la mkutano.

Ni kweli, yote haya yamekuwa yakijitokeza kwenye mikutano husika. Ni muhimu kuripotiwa.

Binafsi, kwenye mikutano hiyo ya Dk. Slaa, sikushangazwa na wingi wa watu au ujumbe wa mgombea huyo kwa wananchi. Ni mambo yaliyoanza kujitokeza tangu kuanza kwa kampeni zake.

Nilichoshuhudia, pengine ambacho kinaonekana lakini watu hawataki kukiona, ni utulivu na usikivu wa wahudhuriaji kwenye mikutano ya maeneo niliyotaja hapo awali.

Kwa mtu makini, utulivu na usikivu wa asilimia 100 kwa watu zaidi ya 40,000 tena waliokusanyika pamoja kwa hiari yao, ni suala la kushitua.

Katika mikutano hiyo, nimeshuhudia umati mkubwa watu ukiwa katika utulivu na usikivu wa asilimia 100. Ni utulivu na usikivu ninaoweza kuita chemchemu ya fikra mpya kwa viongozi au watawala.

Nizungumzie mkutano mmoja kati ya mingi niliyopita. Huu ni mkutano wa Ifakara mjini. Nikiwa mkutanoni Ifakara mjini nilimwona mama muuza ndizi mbivu alizozipanga kwenye sinia.

Kwa wakati huo, mkutano ulikuwa ukiendelea, Dk. Slaa anazungumza.

Kwa kuwa utulivu na usikivu uwanjani pale ulikuwa kwa asilimia 100, huku sauti ya mtu mmoja tu ikisikika (Dk. Slaa), nilimsogelea yule mama, ambaye macho yake yalijielekeza kwa Slaa na sio sinia lake la ndizi alilokuwa ‘amelibwaga’ chini.

Nilipomsogelea, nikainama kukwanyua ndizi mbivu ili nile kama mnunuzi wake. Hapa, kipaumbele changu hakikuwa ndizi bali kupima utulivu na usikivu wake kwa mtu anayemsikiliza. Je, anaguswa na anachosikia?

Je, amefika uwanjani hapo kwa sababu kipaumbele chake ni kuuza ndizi? Na je, kama kipaumbele chake awali kilikuwa kuuza ndizi, kipaumbele hicho kimetekwa na hoja za Dk. Slaa?

Je, kipaumbele cha mama huyu muuza ndizi mbivu kimegeuka kutoka uuzaji ndizi eneo la mkutano hadi kusikiliza hoja za Dk. Slaa? Kwa nini haya yamtokee mama huyu? Haya ni sehemu ya maswali niliyotaka kuyajibu kichwani mwangu.

Nilipokwanyua ndizi ile ya kwanza, alinitazama na kisha kuendelea kumtazama na kumsikiliza mzungumzaji (Dk. Slaa). Nahisi aliniamini kwamba ni mteja nitakayemlipa bila matatizo.

Nilikula ndizi nne bila yule mama kunitazama (macho na masikio yake yakitekwa na Dk. Slaa). Bado uwanja ni tulivu na usikivu wa maelfu ya watu ni mkubwa, ukiniondoa mimi ambaye bila shaka nimepunguza kiwango kutoka asilimia 100.

Nilichukua ndizi nyingine. Nikamuuliza hivi unajua nimekula ndizi ngapi? Akajibu, wewe kula nitahesabu maganda; huku akiendelea kumsikiliza Dk. Slaa. Alijinijibu kwa haraka, nadhani alinichukulia kama mtu msumbufu na si mteja anayemtafuta juani kila kukicha.

Hatua yake hiyo ilinifanya niwekeze zaidi fikra zangu kwake na kiasi fulani nihusishe na ujumbe wa Dk. Slaa kwa wakati huo.

Kama ilivyo kawaida, masikio ya mwanahabari na macho yake hulazimika kufanya kazi ya ziada. Wakati nikila ndizi niligawa fikra zangu, nilikuwa nikisikiliza anachosema Dk. Slaa.

Kwa hiyo fikra zangu zilibanwa na matukio matatu kwa wakati mmoja. Kwanza, kuwasiliana kifikra ‘kimya kimya’ na huyu mama kwa kuzingatia utulivu na usikivu wake uliomfanya apuuze biashara yake kwa muda.

Pili, kuunganisha mawasiliano hayo ya kifikra na ujumbe wa Dk. Slaa ili nipate tafsiri sahihi kwa kutazama mwenendo wa nchi, siasa na mchakato wa kidemokrasia.

Tatu, kwa kuzingatia ujumla wa mazingira hayo, nini nafasi ya watawala walioko madarakani? Je, ni kweli kuna mkatiko wa mawasiliano kati ya watawala na walalahoi mfano wa huyu mama?

Naam, mkutano unaendelea. Sasa Dk. Slaa anazungumzia hoja mbili. Kwanza alikuwa akifafanua atapata wapi fedha za kufidia uamuzi wake wa kuondoa kodi kwenye vifaa vya ujenzi.

Uamuzi unaotajwa kulenga kumwezesha mwananchi mwenye uwezo wa kati au wa chini ajenge; tofauti na hali ilivyo sasa.

Lakini pia Dk. Slaa alikuwa akifafanua atapata wapi fedha za kugharimia elimu ya awali hadi chuo kikuu ili kumwondolea mzigo mzazi wa mwanafunzi au wanafunzi.

Masuala haya mawili niliyaunganisha na utulivu ulioshiba na usikivu wa yule mama muuzaji ndizi. Ni mama wa makamu anayeonekana kuwa na familia. Tena ni familia yenye wanafunzi.

Kuna mambo kadhaa niliyabaini kutoka kwa mama yule. Kwanza , licha ya kufanya biashara anaamini biashara husika haikidhi mahitaji lakini hana mbadala.

Katika mazingira hayo, ni dhahiri mbadala pekee anaohitaji yule mama ni kuchagua kiongozi bora. Kiongozi atakayelinda maslahi yake, familia yake, jirani zake, wana-Ifaraka wenzake, wakazi wenzake wa Morogoro na Watanzania wenzake nchini.

Nguvu ya usikivu na utulivu kutoka kwa mama yule na maelfu ya wakazi wengine uwanjani pale ilinielekeza niibue tafsiri mpya.

Tafsiri hiyo ilizingatia masuala ya msingi, ikiwa ni pamoja na ukweli kuwa, wananchi walifika eneo la mkutano kwa utashi binafsi na si kwa ushawishi wa lifti au kingine chochote.

Na kubwa zaidi, hata waliofika kwa ajili ya kufanya biashara ndogo ndogo walisahau biashara zao. Kwa kuzingatia mazingira haya, tafsiri niliyoipata ni kwamba viongozi walioko madarakani hawako salama hata kama watashinda uchaguzi kwa haki au mizengwe!

Haina maana kwamba hawako salama kwa maana ya uhai wao, la hasha. Hawako salama kwa kuzingatia mfumo wao wa kiuongozi. Mfumo wa uongozi unaomtenga mama yule na wenzake kutia mkono ili naye anufaike na raslimali za Tanzania.

Mfumo wa uongozi unaotanguliza kujuana katika mgawanyo wa raslimali na kulindana katika makosa ya ufisadi wa mali za umma. Hakika, kama mfumo huo hautavunjwa baada ya uchaguzi mkuu, mama yule na wenzake wakaendelea kusahaulika, viongozi hawatabaki salama. Siku zao zitaanza kuhesabika.

Nguvu ya utulivu na usikivu ya mkusanyiko wa watu zaidi ya 40,000 niliyoshuhudia Ifakara ndiyo iliyojitokeza Lupiro-Mahenge, Njombe, Songea na Iringa.

Kwa heshima zote, nawasilisha ujumbe kwa watawala kwamba; utulivu na usikivu ule wa hoja ni shinikizo kwenu kubadilika; kinyume chake siku zetu zitaanza kuhesabika.

Ukweli ni kwamba, yeyote atakayeshinda Uchaguzi Mkuu 2010 na kuingia Ikulu, awe Dk. Willibrod Slaa wa CHADEMA, Jakaya Kikwete wa CCM au Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, usikivu na utulivu ule katika mkusanyiko wa maelfu ya walalahoi ni changamoto mpya kwao.

Kama leo mkusanyiko wa walalahoi zaidi ya 40,000 katika kila mkutano wanakua watulivu, ipo siku utulivu na usikivu ule utafanyiwa kazi na walalahoi hao hao. Siku hiyo itafika kama watawala watazidi kujenga wananchi wa mfano wa mama muuza ndizi.

Siku hiyo ikifika, watoto wa mama muuza ndizi na watoto wa majirani zake na wengine nchi nzima wataungana kutaka kujiondoa kwenye lindi la umasikini kwa kutumia nguvu na akili zao kwa taratibu zao. Atakayeshinda asiruhusu hilo.

Hii ni changamoto inayoshinikiza kufumuliwa kwa mfumo wa uongozi wa kulindana katika ufisadi, kuenzi urafiki katika kugawana madaraka. Ni changamoto inayohitaji kufumua mfumo wa chama kwanza, Taifa baadaye.
Sidhani kama yule mama ni mwana-CCM lakini nina hakina ni Mtanzania.

Kuendeleza kauli za chama kwanza mtu baadaye, ni kuzidi kuwatenga katika ufalme watu mfano wa yule mama anayeshinda juani kusaka tonge.
Nihitimishe kwa kumnukuu mwanzilishi wa taasisi ya kudhibiti uzito kwa watu (Weight Watchers Organization), Jean Nidetch, aliyewahi kusema: “It's choice -not chance - that determines your destiny.” Kwamba ni uamuzi na si fursa inayoangaza hatima yako.

Kazi kwako. Nikipata nauli nitahudhuria mikutano ya wagombea wengine na nitakueleza nitakachoona bila wao kuona.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
 
Yu wapi maggid aisome hii?

Hii haijapata tokea tangu enzi za baba wa taifa.
taifa linajua nini linataka. waache wenye wivu wahangahike na fedha zao
 
Mubezi umeongea vizuri sana... nashukuru kwamba umeenda mbali zaidi ya uwingi wa watu na tisheti na kofia na ze komedi

Umeenda kwenye quality ya mhadhara... hapa ndipo nipapendapo mimi... ziku zote ukiongea pumba, haifiki hata dk 10 utaona watu wanaangalia saa, wanaongea wenyewe au hata kukupigia makofi uondoke.

Dr. ana kipawa cha msisitizo, ana nguvu za ushawishi na pia anafanya homework nyingi... he may not be perfect lakini surely huwezi linganisha na kakangu JK... hata lipumba anajitahidi sana na kwa ubora wa mihadhara yake
 
Kiukweli ndugu na marafiki zangu huyu mtu(dr slaa) ana kitu cha ajabu anakuvuta,anateka mawazo yako yote yanakuwa kwake,simfananishi na simlinganisi ila ni kama yule baba yao au babu yetu ambae hatupo nae duniani.
 
This iz another good and best article!! nikihisi kumwaga chozi wakati naisoma thread yako...imeni'touch' sana hasa kisa cha huyo mama muuza ndizi na mustakabali nzima wa nchi yetu....mi nadhanii itafika kipindi watu watajiridhisha kwa siku yao kuisha vizuri kwa ku''spit'' au kutemea ''kohozi zito'' picha ya JK....kaharibu sana hii nchi
 
Mkuu mubezi,
karibu sana
Ni ukweli usiofichika, huu mtiririko wako wa uandishi nimeukubali.
Endelea kutuhabarisha
 
Kama leo mkusanyiko wa walalahoi zaidi ya 40,000 katika kila mkutano wanakua watulivu, ipo siku utulivu na usikivu ule utafanyiwa kazi na walalahoi hao hao. Siku hiyo itafika kama watawala watazidi kujenga wananchi wa mfano wa mama muuza ndizi.

Key message thanks!!!

Kuna kitu kimoja tu niwaongezee, kwamba although watu hawapendi changes/mageuzi kwenye mambo mbalimbali kiasili. Watu hao hao wanapenda mageuzi kwenye siasa sana!

Mfano ukiangalia jina la chama kinaitwa CCM litakueleza kwamba always in politics people like changes.... but they need realiable change ... not change b'se it is change!!!

Dr. Slaa ni tumaini katika kuona hizo changes, and people listen carefully to ensure reliability of change promised!!! Of course washabiki wanaenda mbali zaidi kuamini tayari wasikilizani wameshakubali!!! well a certain percentage yes, but still majority will need be assured whether promised changes will is reliable and credible.

Mfano wa kuonyesha wananchi wanapenda mageuzi ni wazee walikuwa wamefanya makubwa kwenye majimbo yao kama Mzee SJM, lakini akaondolewa na kijana... walifanya hivyo tu pale walipogundua kijana ana uwezo, na walifanya hivyo sio kwa sababa Mzee SJM hakuwa ana-uwezo no, it was b'se changes in politics is inenvitable.

My take
---> Kukubali kwamba watu wanapenda mabadiliko it is obvious
---> Kuelewa kwamba CHADEMA isipopata 30% ya kura za urais kwamba sio udhaifu wa Dr. Slaa bali ni kwamba people needs to process and assess credibility of changes they want to make.
---> Personally I won't give CHADEMA presidencial vote, b'se they were not serious in picking up the running mate, also they will not able to form government even if Dr. Slaa be a president per our current constitution zaidi ya kwamba watakwamishwa na chama kitakachokuwa na wabunge wengi which is obvious CCM.
--->Kura ya Mbunge na Diwani yes nitawapa wapinzani b'se I need them to build that credibility to be given vote for change.
--->Indeed kuipa CHADEMA urais sasa ni kuamini only one person can run a country... bila kuwa na nguzo nyuma!
 
Nimeisoma hii makala kuhusu utulivu, kwa utulivu wa asilimia 100

Hongera sana, Maggid .... read that 'piece' so you build your capacity...
 
Key message thanks!!!

Kuna kitu kimoja tu niwaongezee, kwamba although watu hawapendi changes/mageuzi kwenye mambo mbalimbali kiasili. Watu hao hao wanapenda mageuzi kwenye siasa sana!

Mfano ukiangalia jina la chama kinaitwa CCM litakueleza kwamba always in politics people like changes.... but they need realiable change ... not change b'se it is change!!!

Dr. Slaa ni tumaini katika kuona hizo changes, and people listen carefully to ensure reliability of change promised!!! Of course washabiki wanaenda mbali zaidi kuamini tayari wasikilizani wameshakubali!!! well a certain percentage yes, but still majority will need be assured whether promised changes will is reliable and credible.

Mfano wa kuonyesha wananchi wanapenda mageuzi ni wazee walikuwa wamefanya makubwa kwenye majimbo yao kama Mzee SJM, lakini akaondolewa na kijana... walifanya hivyo tu pale walipogundua kijana ana uwezo, na walifanya hivyo sio kwa sababa Mzee SJM hakuwa ana-uwezo no, it was b'se changes in politics is inenvitable.

My take
---> Kukubali kwamba watu wanapenda mabadiliko it is obvious
---> Kuelewa kwamba CHADEMA isipopata 30% ya kura za urais kwamba sio udhaifu wa Dr. Slaa bali ni kwamba people needs to process and assess credibility of changes they want to make.
---> Personally I won't give CHADEMA presidencial vote, b'se they were not serious in picking up the running mate, also they will not able to form government even if Dr. Slaa be a president per our current constitution zaidi ya kwamba watakwamishwa na chama kitakachokuwa na wabunge wengi which is obvious CCM.
--->Kura ya Mbunge na Diwani yes nitawapa wapinzani b'se I need them to build that credibility to be given vote for change.
--->Indeed kuipa CHADEMA urais sasa ni kuamini only one person can run a country... bila kuwa na nguzo nyuma!
Hapa ndio naamini kuwa lile suala la mgombea binafsi kwanini lilipingwa na kuamuliwa kwa mizengwe.

 
Kuna tofauti kubwa kati ya mwandishi huyu na Majjid kuhusu articles zinazofanana. This is what i call "Journalism with a purpose".
 
Ndg yangu, mimi nimekuwa nikiwaasa wenzangu waone tofauti iliyopo kati ya hotuba na usikivu wa watu kwa mgombea wa Urasi CHADEMA na wagombea wengine. Kusema kweli, hata kwa OBama watu walikuwa wanasemshana mkutanoni na ungeona wananong'onezana. Kwa Dr. Slaa ni kimya bin utulivu. Ukimya huu si bure.

Kusema kweli hata wakati nasoma ujumbe wako NILIKUWA KIMYA utafikiri namsikiliza Dr. Slaa. Sijahudhuria mkutano wake, lakini i can read from the state of the crowd.....

Dr. Slaa ni MKOMBOZI, tukiliamini sawa, tukilipuuza, TIME WILL TELL.

Mungu Ibariki Africa yetu yote. Mlinde Slaa, Kikwete, Lipumba na wagombea wengine, ili sauti hizi zitakapoongea baada ya utulivu huu sote tuseme VIVA!
 
Naomba MUNGU amwezeshe na na Dr. Benson Bana wa REDET asome maelezo yako makini ili ajue hisia halisi za mtanzania wa leo hii.
 
kasheshe said:
Personally I won't give CHADEMA presidencial vote, b'se they were not serious in picking up the running mate, also they will not able to form government even if Dr. Slaa be a president per our current constitution zaidi ya kwamba watakwamishwa na chama kitakachokuwa na wabunge wengi which is obvious CCM.

Kasheshe,

..call me crazy, but I have been dreaming of the day when our President would come frm a party that does not have a majority in the parliament.

..mwanzo nilikuwa naomba CCM wa-lose majority of the seats, lakini inavyoelekea ni rahisi zaidi, in the near future, kwa vyama vya upinzani kupata Raisi, kuliko majority ya bunge la muungano.

..naamini mfumo wetu wa utawala na bunge utafanya kazi vizuri zaidi ikiwa Raisi atatoka kwenye chama kisicho na majority bungeni, au tukiwa na situation ambapo the majority is very slim in the parliament.

..uchaguzi huu kura yangu ya Uraisi ni kwa Dr.Wilbroad Slaa.
 
jokakuu umeongea POINT MUHIMU SANA,mana wabunge wetu wanatumikia vyama vyao kuliko wananchi waliowachagua,bigUP KUBWA
 
Back
Top Bottom