Nilichokiona jana mkutano wa ACT-Wazalendo

Nilichokiona jana mkutano wa ACT-Wazalendo

Yaani walikuwa na poor planning sana, yaani jana wamenadi sera na itikadi yao ambayo ni nzuri kwa kweli lakini hawakuwa hata na kadi za chama pale kwa ambao wangeshawishika kukiunga nao. Walikuwa busy kuuza t-shirts zao.
 
Hata Chadema ni chama cha kaskazini..Bila mbowe hakuna kinachofanikiwa[emoji23]
 
1. Kila chama kina base lakini hakihubiri the so called " Chama Chetu" meaning ni cha watu wa ile base. Hili nililishuhudia kwenye mijadala muda wa mapumziko.
2. Huu ulikuwa ni mkutano wa ndani, hakukuwa na sababu ya kuchelewa, wajumbe wanafika wanakuta ukumbi ndio kwanza unaandaliwa.
3. Hiyo clip ya huyo dada sina hapa, but ninachoongea ni kweli kama mjumbe alikuwepo jana atathibitisha hili. Alikuwa dada mmoja mweusi kajaaliwa kidogo.
Mtu anapozungumza chama chetu unatambuaje kama "niukabila"?.CCM,CDM,Chauma si mali yawanachama?,mwanachama akizungumza hiki nichama chetu tatizo linatoka wapi?.

2.Unataka kutanabaisha wajumbe walio wengi walifika muda husika?.Au wengi wao walichelewa.

3.Kama clip huna tutaamini vipi maneno yako,na nikitafuta mtu aliekuwepo akadai ayo maneno hayakusemwa utawaambia moderator wafute uzi wako?.
 
Mwanaume ukiwa mbea haipendezi,kilichokupeleka huko ni umbea,acha hiyo tabia utakuja ombwa 0713
 
Ni sawa na chadema bila dj mbowe hakuna chadema bila huyo mkwepa kodi ndo sawa na act bila zito
 
Mtu anapozungumza chama chetu unatambuaje kama "niukabila"?.CCM,CDM,Chauma si mali yawanachama?,mwanachama akizungumza hiki nichama chetu tatizo linatoka wapi?.

2.Unataka kutanabaisha wajumbe walio wengi walifika muda husika?.Au wengi wao walichelewa.

3.Kama clip huna tutaamini vipi maneno yako,na nikitafuta mtu aliekuwepo akadai ayo maneno hayakusemwa utawaambia moderator wafute uzi wako?.
Mkuu endelea kutoa povu but ukweli ndio huo
 
Ni kweli huyo Dada alivaa gauni yeupe ,tuliokaa juu tulimuona alikuwa maeneo ya katikati yule Dada alikosea alitakiwa aiwakilishe ile hoja kwa maandishi ,IPO siku Mama ataondoka ACT kwa mtamshi Yale kila siku anasema hakujiandaa
 
Samahani kamanda. Tuwe wakweli tu, ukiacha Zitto, ni kiongozi gani ACT anaweza kuitisha nkutano wa hadhara akapata watu? Ni kitila? Mchange? Anna? Hawa unaeeza kuwafananisha na Lissu, Lema, Sugu, Prof J, Mnyika, Mwalimu, Mdee et al? Let us be sincere!
Ni sawa na chadema bila dj mbowe hakuna chadema bila huyo mkwepa kodi ndo sawa na act bila zito
 
Ukijibu masuali haya utapata majibu.

Hakuna chama ambacho hakina base?.

Ulijuaje kama wanachama wengi waliohudhuria Jana ni wakigoma?.

Umejuaje wanaotoka mikoa mingine kama niwashkaji zake Zitto?.

Huyo alive muatack mama Anna alimuatack wapi?,unaweza kutuwekea vidio tuone hayo maneno?.

By the way Chadema,Nccr,Cuf,Chauma na CCM wanachama wake wengi wanotka wapi?.Bila shaka utakuwa unafahamu kwa kuwa wanachama wa ACT umefahamu wanapotokea(wengi).

Chama kipi ambacho huwa kinaanza mkutano muda kilio utangaza utaanza?.



mi sielewi hapa kwani ccm base yake ipo wapi mana huwa wanashambulia sana vyama vyetu vya upinzani kuwa ni vya kikanda hii hoja huasiipendi mana Tanzania ni moja ubaguz huo ni mbaya.
 
Kila chama cha siasa huanza hivyo hata TAA na baadae TANU ilianza hivyo, wazee wa Dar akina Abdulwaheed Sykes kwa kutaka kuungwa mkono bara walimfuata Chief Makwaiya Kidaha wa Shinyanga ili aongoze Chama dhidi ya mkoloni akakataa, ndipo walimfuata JK nyerere, kwanza alisita kdg baadae akakubali, na leo hii baba wa Taifa ni JK nyerere na nani anamjua chief Makwaiya? Historia ina maajabu yake na ajali zake tuwekeni akiba ya maneno.
 
Chadema top leader wake wanatoka kaskazini hususani kilimanjaro na pia base yake ipo huko huko kilimanjaro na ndio maana hata wabunge wengi wa viti maalum niwachaga... Pole sana zito anaijua siasa na chadema kinawauma hicho sababu hamna mjenga hoja kama yeye waliobaki ni waropokaji wasiojua mbele wala nyuma......
 
Kumbuka ccc ilivyoanza miaka 20 tulikuwa tunamwimbia Mwalimu wetu Nyerere tu na fikra za mwenyekiti wa ccm zikadumu kwa miaka yote hiyo acha na ile miaka ya kuanzisha chama labda jumla ilifikia hata zaidi ya 30 ukijumlisha ni hiyo miaka ya kuijenga chama.
Leo ccm wanataka kuaminisha watu kuwa wao ndio wanademocrasia tu kwa kuwa wanabadili uongozi kila baada ya miaka 10.

Kumbuka South Africa. Mandela amekuwa ikon kwa miaka mingapi?
Miaka yote mpaka kufa kwake.
Kulea chama siyo mchezo mdogo kama unavyofikiri.
Inahitaji moyo, uaminifu, uwezo, ujasiri, hekima na pesa.
Ni wachache sana wenye yote hayo.
Huwezi kuendesha chama kwa michango ya watu. Full stop!
Lazima kuna kujitolea sana katika kujenga chama.
Hivyo wanachama wa ACT, chadema,NCCR, ETC,ETC msidanganyike na kibaraka anayetaka kuwaaminisha kuwa vyama vinaanza vinavyoanza vinaweza kubadilisha viongozi kwa muda mfupi.
Msiruhusu hiyo katika katiba zenu. Ni uwongo na hamtafika.
Anayeanza chama ana vision fulani ambayo ni yeye na wachache wanayo.
Siyo kila kiongozi ana vision.

You ca see the difference between Nyerere and his followers-it is like heaven and earth!!!
 
Yaani walikuwa na poor planning sana, yaani jana wamenadi sera na itikadi yao ambayo ni nzuri kwa kweli lakini hawakuwa hata na kadi za chama pale kwa ambao wangeshawishika kukiunga nao. Walikuwa busy kuuza t-shirts zao.
Hata Chadema miaka 1995 mpka 2005 base yake kuu ilikuwa kigoma na mbunge wake wa kwanza alitokea kigoma fuatilia hilo utajua then uje tuongee sio kuropoka kama mvuta bangi... Chadema hamna mjenga hoja waliopo ni waropokaji na sasa chama kimekuwa cha wachaga
 
Mkuu uko sawa kabsa, act ni chama cha watu wa kigoma, hilo halina ubishi 100% na wakat mwingne namuoneaga huruma sana huyo mama Anna, kingne zito ana mvuto zaid kigoma
endeleeni kugawana vyama kikanda au kikabila mkidhani ndo njia ya kuitoa ccm!! ccm ina coverage kwenye kila kabila huo ndo utakua mwanya wa ccm kusalia madarakani
 
Back
Top Bottom