Nilichokikuta kwa Mchepuko wangu jana, wanaume tuwe makini

Kilemakyaaro

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
5,050
5,078
Nnawasalim sana wakuu, nnaomba niende kwenye mada moja kwa moja.

Ni hivi mimi ni mwajiriwa na niko mkoa fulani, familia yangu iko Mkoa Mwingine. Sasa baada ya kuja hapa ktk pitapita zangu nikakutana na binti mmoja mzuri tu na mwenye sura ya upole na mtulivu, yeye anafanya kazi sector binafsi.

Basi Wakuu kama kawaida nikaona nisiendelee kuteseka nikajiweka lkn kwa sharti kwamba lazma kupima afya na yeye akakubali. Nlimfahamisha nna familia so akawa anajua na akanambia alikua na mtu sema wameachana.

Basi maisha yakasonga, nikajikuta nnampenda kwa maana aliniwezea sana lkn pia ni mtulivu huwez mdhania.
Basi bwana Weekend ile kabla ya hii ya juzi siku ya jumamosi akawa Hapatikan kabisa ktk sim zake, kutwa nzima isipokua kuna saa ikaita mpaka ikakatika na baada ya hapo hakupatikana tena.

Jion sana akapatikana na nlipomhoji kulikoni akanambia alikua shamba nje ya mji na hakuna mawasiliano. Nikamuuliza toka msimu wa kilimo unaanza mpaka sasa wanavuna sikuwahi kusikia una shamba kulikoni?

Akajibu simple tu kwamba analo na hakunambia, ila kiuwanaume nikaona tayar hapa kuna issue ila nikatulia kukusanya ushahidi na hakika mipango yangu ilikua nimpakie garini nimtake anipeleek huko shamba.

Sasa baada ya huo mkasa nikasafiri na nikamuaga. Siku ya jumatatu nikarejea bila kumwambia na nlipofika nikampigia akanambia yuko saluni, ila baada kama ya saa moja na hivi nikaanza kumpigia hapatikani kabisa, nikaona hapa tayaar.

Basi nikaenda kwake, gonga sana mlango na dirisha lkn hapakua na dalili ya uwepo wa tu zaidi ya viumbe kama panya.
Siku ile nikapanga kuhakikisha nnapata ukweli so nikarejea kwangu then nikatulia (sikulala kabisa) mpaka saa 11 alfajri nikaenda kutega njia anayopitaga kwenda kazini lkn mpaka panapambazuka hakutokea. Muda kidogo simu zake zikawa hewani akanza ngonjjera kua alisahau charger ofisin ndio maana hakupatikana kwakua simu ilizima.

Basi nikajifanya boya, jion nikamuibukia home nikambana akagoma kua hachepuki, basi mwanaume nikalegezwa na nikapewa na mbususu.

Nlipoanza zoez tu nikakuta kitu sio kabisa bas nikakomaa ila nlipomaliza nikamuuliza mbona leo baridi sana akaanza blahblah. Hapo sasa nikasema mimi na yeye na yeye na mimi, nikachukua sim nikataka kusepa nayo aisee akaanza kuweweseka na hilo likanipa sababu ya kukomaa zaidi. Bas bwana baada ya kumbana akakubali kua kweli hakua home alilala kwa jamaake na akakiri aliliwa.

Kwanza nikapata hasira mnoo baada ya kujua alipokojoa muuni bila kinga na mimi nimerejea hapo ktk muda usiozidi masaa 12. Nlichofanya nikamzoa muda kama wa saa saba mpaka dispensary kupima afya tukawa poa then nikampeleka mahala nikamtaka afungue simu hapo ndio balaa lilipoibuka maana aligoma kabisa.

Bas wakati malumbano yanaendelea kama muda wa saa nane usiku akapiga jamaa nikapokea ebwana nikamchana mwana kua jopange hapa huna mtu maana tuko foleni kama ya mbagala na namba yake nikachukua huku dem kaganda kama sanamu.

Baada ya simu ile nikamkaba kwa mbinu za medani akafungua simu, ebwanaeee niakkuta Chart za jamaa aliemla ule usiku( Huyu sio aliepiga simu) wanaelezana mchezo ulivyokua.

Nilakuta na Chart za mwana aliepiga simu nae ni jamaa yake na ndio waliokua wote ile weekend nliokua simpati, nikakuta na mawasiliano ya muuni mwingine tena anakula lkn na namba kibaoo, yaani nyingi zenye majina na ambazo hazipo ktk phone book zote mapenz matupu.

Ila kwa uhakika kabisa nikajikuta ndani ya Mkoa huu niliopo kuna wana watatu na mimi wa nne tunamkula huyu mtu mmoja na bahati mbaya hakuna kinga hapo.

Kiukweli nilijaa upepo, nlichofanya nikachukua namba za wana na wote nimewapa taarifa juu ya hii chain maana ni hatari mnoo. Bahati mbaya sana nikagundua wote ni vijana na tuna familia, hapa nikajiuliza manaake mmoja kati yetu angekwaa lolote hapa manaake chain yote hii na wake zetu wangekua hatarini.

Pamoja na kwamba nimefupisha hii story, somo kuu nlilopata na ambalo nnawapa ninyi vijana wenzangu ni ACHA MICHEPUKO, KUA MAKINI SANA NA USITHUBUTU KUMWAMINI MTU, nnarudia haswa kwa wanaume tuepuke kua na imani na hawa watu, hata kama umepima aisee usijidanganye ukaenda kihuni utaja lia.

Lingine la Muhimu sana ni kuweka akilini ule msemo kua 'Wanawake malaya wako salama kiafya' kuliko hawa wa mtaani,ofisini naavyuoni, yaan hao ambao bila kinga humgusi ni safe kuliko hawa wa mazoea ambao anawapanga na anaweza maliza Ukoo.

Mwisho japo sio kwa Umuhimu, nimejionea hatari ya kuchepuka kupitia hili tukio, vijana tuache zinaa na tuwe mkini, usipime mtu kwa macho ama hospital na ukamwamini, itakugharimu.

Niwieni radhi kwa hili Bandiko, ukisoma kwa utulivu utapata kitu, utajifunza.
Wassalaam na Nnawatakia kila la kheir
 
Yaani pamoja na kujuana wote zaidi ya watano, bado kuna njemba zenye roho ngumu zitaendelea kutandika Mbususu.

Na huyo mwanamke atadanganya, wote wamenigaya. Ila nimeshindwa kukuacha wewe tu.

Aisee!
 
Lingine la Muhimu sana ni kuweka akilini ule msemo kua 'Wanawake malaya wako salama kiafya' kuliko hawa wa mtaani,ofisini naavyuoni, yaan hao ambao bila kinga humgusi ni safe kuliko hawa wa mazoea ambao anawapanga na anaweza maliza Ukoo.
Mwisho japo sio kwa Umuhimu, nimejionea hatari ya kuchepuka kupitia hili tukio, vijana tuache zinaa na tuwe mkini, usipime mtu kwa macho ama hospital na ukamwamini, itakugharimu.
Dah, pole sana aiseee! Kila la kheri Sheikh
 
Mambo mengne ni ushamba..

Ww una mke wako na unajua kabisa huna future na huyo binti wa watu halafu unambana utafikiri ni mkeo.. Huo ni upunguani. Nenda kambane mkeo asigongwe na bodaboda huko ulikomuacha acha kumbania nafasi mtoto wa watu..

Huo umakini unaouweka kwa mchepuko uweke kwa mkeo. Ww jifanye kujitoa ufahamu utalea watoto wa majirani zako ulikomuacha mkeo shauri yako.
 
Nimekuelewa sana Sheikh, ni ajali tu hizo

images (2).jpeg
 
Uko vizuri kwa sababu hizi;

1. Kuna tabia za wanaume wengine wakigundua issue kama hiyo wanaanza kutukanana na kugombana ilhali wao ndiyo wanachezewa. Ni muhimu sana wanaume kufahamiana na kupeana taarifa baada ya kugundua wanachezewa. Big up sana.

2. Hakuna mwanamke muongo ambaye siye malaya. Umalaya na uongo ni mapacha siku zote, na rafiki yao mkubwa ni wizi. Mtu mwongo ni malaya na mwizi. Maelezo ya mwanamke ambayo hayapo straight maana yake ni uongo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom