Nilichokikuta baada ya kupekua chumbani kwa dada wa kazi

jail

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
458
250
Habari wanaJF,

Leo jumamosi nimeshinda home kwangu wife na binti wangu wa kazi wakatoka kidogo nikajisikia leo nipekue chumbani kwa dada wa kazi cheki mabegi nk .
Mpaka chini ya kitanda hii inaitwa intelijensia ya nyumbani du nikakuta dada ameficha soksi zangu nzuri chini ya kitanda chake tena ndani ya mkeka matambala machafu ya hedhi yaliyotumika kafundika mavunguni tena ya mda mrefu.

Da kazi kweli kweli ila swala la soksi zangu tena nzuri kuficha chini ya kitanda ndio sikuelewa ni imani fulani au bahati mbaya nawaza nimshirikishe wife amsaidie huyu binti usafi wake ila najiuliza wife atanishushua nini kuwua nimeanzaje tabia ya kupekua pekua mawazo yenu wandugu.
 

strong ruler

JF-Expert Member
Nov 2, 2013
4,905
2,000
Hahahaha aisee acha nicheke manake hii ni bonge moja la mtihani, manake hapo ulipo mwenyewe kwanza..unawaza soksi zako kwanini ziko pale!! Pili..ukimwambia mama Chanja lazima atamind kwanza utaanza anzaje?, tatu..huyo dada wa kazi lazima Atakuona wack hatokuwa na Imani tena na wewe boss wake!!
 

tofali

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
4,012
2,000
Aaah kaka bora ukae kimya usiseme km umepekua ila ongea tu kiutu uzima ili wife ashawishike kukagua...ila si tabia nzuri kumkagua mdada hiyo ni kazi ya mama..unaweza singiziwa ulimtaka
 

Deo Corleone

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
15,830
2,000
Andika barua uiache mezani ili wife aione. Mitihani mingine ni zaidi ya kumpa mtihani wa kihaya aufanye mngoni.
 

jail

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
458
250
Hahahaha aisee acha nicheke manake hii ni bonge moja la mtihani, manake hapo ulipo mwenyewe kwanza..unawaza soksi zako kwanini ziko pale!! Pili..ukimwambia mama Chanja lazima atamind kwanza utaanza anzaje?, tatu..huyo dada wa kazi lazima Atakuona wack hatokuwa na Imani tena na wewe boss wake!!

yani na kalivyo kapole hadi nakahurumia yani inashangaza nje kanajipenda mke wangu anampa hela mpaka bonus anagewa kwa utendaji mzuri sasa anashindwa kununua pedi mpaka atumie matambali mengine uvunguni chini ya kitanda da najiuliza au soksi zangu alifanya pedi nazo kwa nini kazificha ndani ya mkeka uliokunjwa kitandani kwake
 

Acha Ushamba

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
202
0
habari wana jf
leo jmos nimeshinda home kwangu wife na binti wangu wa kazi wakatoka kidogo nikajisikia leo nipekue chumbani kwa dada wa kazi cheki mabegi nk mpaka chini ya kitanda hii inaitwa intelijensia ya nyumbani du nikakuta dada ameficha soksi zangu nzuri chini ya kitanda chake tena ndani ya mkeka matambala machafu ya hedhi yaliyotumika kafundika mavunguni tena ya mda mrefu da kazi kweli kweli ila swala la soksi zangu tena nzuri kuficha chini ya kitanda ndo sikuelewa ni imani fulani au bahati mbaya nawaza nimshirikishe wife amsaidie huyu binti usafi wake ila najiuliza wife atanishushua nini kuwua nimeanzaje tabia ya kupekua pekua mawazo yenu wandugu

You are very intelligent, i like that! Very excellent, sio mwanaume unakaa kiduanziduanzi tu. Kazi kutoa hela ya matumizi ya nyumbani na kwenda kutafuta zingine! You must maxmize your security! Wanaume chukueni hii msiache!
 

jail

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
458
250
Ukome kupekua pekua

siwezi kukoma upekuz unasaidia kujua mengi dunia imebadilika mkuu mi si waamin hawa wadada anaweza kuwa mwanga ukiona ndumba baada ya kupekuwa unachukuwa hatua binadam wa leo wanatisha hawaaminiki sio uje uone matekeo ndo uchukue hatua mfano leo nimeona soksi zangu chini ya kitanda chake kaweka za nini lazima nifuatilie hii filamu mpaka mwisho
 

Hornet

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
21,667
2,000
Jaribu kuongea na mama watoto mazungumzo ya kiutu uzima usimwambie direct utazua mengine..
Hilo la kutumia matambara na kuweka uvunguni hata msichana wangu alikua nalo..inabidi mama watoto akae nae amfundishe matumizi ya pedi..
..kuhusu soksi labda alizipenda tuu na amezihifadhi tuu
 

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,962
2,000
siwezi kukoma upekuz unasaidia kujua mengi dunia imebadilika mkuu mi si waamin hawa wadada anaweza kuwa mwanga ukiona ndumba baada ya kupekuwa unachukuwa hatua binadam wa leo wanatisha hawaaminiki sio uje uone matekeo ndo uchukue hatua
na mkeo nae huwa unampekuwa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom