Unamnyanyasaje dada wa kazi kama wewe sio chizi

kiroka

JF-Expert Member
Feb 28, 2018
355
1,856
Kuna watu nawaona hawana akili au ni malimbukeni hivi unaanzaje mwanamke kumnyanyasa dada anaekuesaidia kazi hapo nyumbani kwako (housegirls) mtu ambaye anaingia nyumbani kwako kila sehemu, mtu unayamwachia hivyo vi akina juniors wako, mtu ambae unamwachia jikoni akupikie chakula na mtu unayempa nguo zako akufulie unamnyanyasa kweli.

Hivi unajua sumu ya panya inauzwa bei rahisi na inaua kibaya zaidi wauzaji wanakuja mpaka majumbani hivi akikasirika siku akapatwa na wazimu kwa mateso yako akanunua sumu ya buku akawawekea hao kina juniors wako utalia na nani kama hukuyatak mwenyewe.

Unaanzaje kumtesa na kumfokea mtu ambaye anaweza kupata nguo yako ya ndani hujui kwao wanaimani gani akiondoka na nguo zako za ndani zikachezewe kishirikina utalia na nani?

Mtu ambae anawapikia chakula unamwona takatak akiamua awawekee uchafu wowote anojua yeye mle utalia na nani acha uchizi

Kwangu mimi dada wa kazi nyumbani namheshimu kuliko hata baadhi ya rafiki na ndugu zangu, Mimi na wife tunashinda kazini tunamwachia watoto na tuna kitoto cha chini ya mwaka mmoja akiamua kukitengeneza atakavo nitalia na nani

Kwangu nmepiga marufuku dada wa kazi kuitwa dada cjui na wife au Mimi tinamwita kwa jina lake na kumheshimu kama mwana familia, acheni uboya wa kuwanyanyasa wadada wa kazi wengi wameahikilia sehemu ya furaha za maisha yetu,akikosea muonye kama mwanao usimuonee
 
Kuna wengine huwa wanawatumikisha kuanzia alfajiri mpaka usiku tena saa 4 au 5
Msichana anafanya kazi za kila aina halafu akiugua hata panadol humpi

Mapumziko mpaka augue, na akiomba ruhusa siku mbili tu, mama mwenye nyumba ananuna kichizi

Kuna binadamu wana roho mbaya sana
Tena sio Bongo ni kila sehemu watu wanatesa sana housemaid

Ila nao wakiamua kujibu mapigo utakula uchafu wa kila aina unaokutoka mwilini na huku akicheka

Tena huyo kakuhurumia sana
Kuna m Philippines mmoja aliuwa mtoto wa muajiri wake Tena visa vingi vimetokea

Umemleta mtoto wa watu akusaidia kazi lakini zingine lazima usaidie pia

Kuna wanawake wapumbavu wanawatuma mpaka kutandika kitanda cha bwana wake
Niliapa nikikuta anatandika kitanda siku hiyo hiyo nafunga nae ndoa
Sina ujinga huo
Msichana wa kazi awe na mipaka na kazi zake sio afue mpaka chupi za baba
Kuna wanawake huwa wanalitafuta la kutafuta
 
Mimi na wife tunashinda kazini tunamwachia watoto na tuna kitoto cha chini ya mwaka mmoja
Ndoa nyingi za wasomi hazina maarifa!

Kwahiyo binti wa watu unayemuachia mtoto wa chini ya mwaka mmoja, yeye ana umri gani? Maarifa ya kulea?

Kwasasa jinsi taasisi hii ya ndoa ilivyotikiswa, UKIMUELIMISHA MWANAMKE, UMEANGAMIZA kizazi kijacho.
 
Haina haja ya kutafuta dada wa kazi waleeni watoto wenu wenyewe
 
Ndoa nyingi za wasomi hazina maarifa!

Kwahiyo binti wa watu unayemuachia mtoto wa chini ya mwaka mmoja, yeye ana umri gani? Maarifa ya kulea?

Kwasasa jinsi taasisi hii ya ndoa ilivyotikiswa, UKIMUELIMISHA MWANAMKE, UMEANGAMIZA kizazi kijacho.
Hujui km mke kaajiriwa unafny nn
 
Hujui km mke kaajiriwa unafny nn
Si ndio hivyo mkuu, maarifa yanapokesana ndo inabidi uhatarishe ustawi wa watoto.

Akiwa na mimba, unajua jinsi ya kufanya...mpaka maternity mnampa.

Tuendelee tu kutegemea beki tatu na walimu kwa malezi ya watoto.
 
Mwisho wa siku tuwasaidie wadada na wamama kutambua kuwa mbususu Ni kiungo Cha uzazi ambacho hakiwezi kumpa utamu mwanamume
Bali kinaweza kumpa utamu mwanamke akikitumia vizuri

Hii Imani potofu ambayo wanawake wametapeliwa na wanaume huenda pia Ina sababisha madhara ya kifikra kwa mwanamke

Haiwezekani mtu mzima kukicha kupambana na kasichana ka kazi!



Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hivi unajua sumu ya panya inauzwa bei rahisi
Kuna za 500, 1000, 2000 na 3000 na zinaua panya ndani ya masaa 24, Ila usichojua zote NI bidhaa za Kenya lakini usichokijua zaidi kwenye ile pakiti pamewekwa ONYO marufuku kuuzwa Kenya

Kuna hio moja inaitwa RatOx hio ni kiboko 1000 TU nyumba nzima inanuka na wanakwambia usivute ile harufu madhara ni kuumwa kichwa & tumbo hapo hujalamba sumu bado
 
Back
Top Bottom