Twin Tower
JF-Expert Member
- Jan 13, 2023
- 4,903
- 7,193
Nimesafiri na aina zote za train tokea ile ya enzi za mkoloni aka gari moshi hadi hii SGR ile express na Ordinary.
Wastani wa safar zangu kwa sasa ni kama mara 24 nikipanda madaraja ya uchumi (economy) na biashara (Business). Royal class ipo njian pia.
Naipongeza serikali kwa huu mradi, hakika umefanya safari kuwa rahisi kiasi kikubwa sio kwa wakazi wa mikoa ya Dodoma, Moro na Dar. Hata wale wa mikoa kama Iringa, singida,Tabora, Mwanza. Hapa unaanzia safar yako Dodoma.
Upatikanaji wa tiketi.
Mfumo wa tiketi umekuwa bora sana, mara moja tu nilipata changamoto za malipo kwa kutumia benk na simu, lakini kupitia huduma kwa wateja nilihudumiwa vizuri.
Ushauri kwenye hili eneo, nikuangalia uwezekano wa mtu
1. Kukata open ticket/tikit ya wazi aweze kuitumia ama ndani ya mwezi lkn afanye confirmation 48/24hrs kabla ya safari.
2. Kukata tiketi ambayo unaweza kubadili taarifa za msafiri. Hii iwe muda wowote, ilimradi wakati kuchek in kuwe na taarifa sahihi.
Huduma ndani ya treni na vituo.
Hili ni moja ya eneo ambalo Kadogosa na timu yake wanapaswa kulisisitiza. Sio mbaya sana, lkn bado hairidhishi.
1. Sehemu za kulumzikia kukosa viti vya kutosha huku msisitizo watu wafike 2hrs kabla ya muda wa kuondoka. Mnawakawalisha wapi?
2. Ukaguzi wa tiketi kufanywa na maafisa wachache.
3.vizuizi kwa abiria wanaoshuka,rahisheni kuwe na maeneo yasiyo na vizuizi kwa wanaoshuka.
4. Usimamizi na huduma ndani ya mabehewa. Watqnzania bado wanajitafuta sana, wanahitaji usimamizi na uongozaji wa matumizi ya vifaa. Msiwe wavivu nyinyi wahudumu ndani ya train.
5. Wekeni wazi mtu akikata business/royal anapata faida zipi.
Miundombinu.
Mpaka sasa hongereni chuma bado mpya, ingawa mfanye maboresho kidogo kuna vitu vimeharibika.
Ile barabara ya kwenda stesheni ya morogoro ni uchafu na inaharibu hadhi. Ni aibu hadi sasa haipo kwenye viwango.
Nitaendelea.