Niliaibika sana, sitakaa nisahau

Niliaibika sana, sitakaa nisahau

Duh, yaani wewe umesoma primary Wakati EATV ishaanzishwa??? Ha ha ha haaa... Kweli humu kuna watoto wengi sikuhizi. Halafu unaonekana unaendekeza mapenzi kuliko shule, no wonder kuna uzi umeandika "Number is don't lie"... ELIMU, ELIMU, ELIMU.
mtoto mwenye miaka 26?
au wewe ni ajuza nini?
 
mmmmmmmmmmm,mie sikuizi sijui nikoje sijui majukumu na ulezi nakua sikumbuki vya zamani kabisaaaaaaaaaaaaaa...
kwani hiii ni yazamani? inaonyesha huyu bado ni kijana mdogo sana, mana channel 5 siyamuda mrefu, na alikuwa la 3...mtoto tu huyu lazima akumbuke jana yake
 
Dah....!! EATV imeanza lini? Mi naikumbuka ITV2 hapo kitambo..

Ila we utakuwa bwana mdogo sana.
 
Umetisha baab,imefanana na moja ilitokea mahakamani mshtaki katukanwa wakiwa kwenye chumba cha mahakamu hakimu akamuuliza mshtaki unaweza sema mshtakiwa alikutukanaje...Mshtaki akasema hapana hakimu siwezi taja alivyonitukana labda niandike halafu wazee wa mahakama wanisaidie kusoma hakimu akamkubalia, akandika kuwa mshtakiwa alimuambia "Twende tukadu" aliandika bila tafsida hapo nimepyunguza ukali wa maneno...Basi kikaratsi kile akapewa mzee wa mahakama mwanamke asome yule mzee akaona soo...Akampa mzee wa mahakama aliekuwa pembeni yake kumbe yule mzee wa pembeni alikuwa amelala...Yule mama mzee wa mahakama akamgusa kwa taratibu yule mzee alivyoamka akamsogezea hicho kikaratasi..kilichaondikwa ''TWENDE TUKADU" yule mzee bila kujua mahakam yote inamuangalia akamuuliza yule mama mzee wa mahakam aliempa hicho kikaratasi''EEH MAMA TWENDE SASA HIVI? Hakimu akaingilia kati kuwa we saidia mahakama kusoma maneno ya mshtaki si wewe umeulizwa...Mzee akaona soo mbaya.
Hahahahahaaaa
 
Mimi nakumbuka siku hiyo ambayo tulikuwa darasa la kwanza karibia watoto 84, na kati ya hao ni wanne tu wanajua kuongea kiswahili, wengine wote wanazungumza kinyumbani tu....! Halafu alikuwepo kaka mmoja mkubwa kahamia shuleni kwetu akitokea darasa la tatu, na ndio mmojawapo wanaoweza kuongea kiswahili...! Sisi ndio tulikuwa waanzilishi wa shule ile....! Ghafla mkaka yule aliingia kwa kuchelewa na kumkuta mwalimu akifundisha...! Wote tulisimama kumsalimia "shikamoo kaka", viniginevyo tungekoma mwalimu akitoka....! Kumbe mezani mwalimu alikuwa na soda yake imefunguliwa na andazi...! Halafu wakati tunaandika yaliyoandikwa ubaoni, mwalimu akatoka nje (nafikiri alienda uani)...! Then, jamaa akainuka na kwenda mezani, akaling'ata lile andazi na kumezea soda ile pia...! Akarudi kukaa kule nyuma ya darasa...!
Kidogo mwalimu akarudi na kukuta andazi lake limemegwa....! Aliongea hadi kimeru (kikwao)...! Wale watoto wanne wanaojua kuongea kiswahili; akiwemo jamaa, walijitetea na kupewa kazi maalum kila mmoja...! Jamaa alipewa kazi ya kuhakikisha kila atakayechapwa atarudi kuunga mstari tena na kusubiri kuchapwa tena, wengine walipewa kazi ya kukata fimbo....! Nakumbuka siku hiyo tulichapwa hadi saa ya kwenda nyumbani....! Hakuna hata mmoja aliyedhubutu kumnyooshea jamaa kidole, kisa ungepita njia gani baadaye....!
Hahahahahaaaaaa nimecheka mpaka sio vzuriiii aliongea hadiii kimeruu hahahahaaa mweeeee haxra zilimkaba koo akajikuta ghafla nayeye anaongea kilugha
 
mmmh hili tangazo la tugeza tunawakilisha si la juzi juzi tu hapo...kwa hiyo wewe uko form one au form two?!
 
Muda huu wenzio wako shule wewe unaleta story za class 3....
 
Primary school, kwenu mlikuwa mna Tv tayari?! Mzee wangu kanunua Tv mimi nikiwa A-Level. Kweli wewe utakuwa kizazi cha BRN.
 
Ulizaliwa awamu ya 4???? Girlfriend darasa la 3??? Una umri gani?? Ukitaka kudanganya jipange
 
Back
Top Bottom