Kitombise
JF-Expert Member
- Sep 24, 2013
- 8,652
- 25,849
- Thread starter
- #21
hahaaa!! kipindi hicho tulikuwa tunamwogopa mwanafunzi mbabe kuliko hata mwalimuMimi nakumbuka siku hiyo ambayo tulikuwa darasa la kwanza karibia watoto 84, na kati ya hao ni wanne tu wanajua kuongea kiswahili, wengine wote wanazungumza kinyumbani tu....! Halafu alikuwepo kaka mmoja mkubwa kahamia shuleni kwetu akitokea darasa la tatu, na ndio mmojawapo wanaoweza kuongea kiswahili...! Sisi ndio tulikuwa waanzilishi wa shule ile....! Ghafla mkaka yule aliingia kwa kuchelewa na kumkuta mwalimu akifundisha...! Wote tulisimama kumsalimia "shikamoo kaka", viniginevyo tungekoma mwalimu akitoka....! Kumbe mezani mwalimu alikuwa na soda yake imefunguliwa na andazi...! Halafu wakati tunaandika yaliyoandikwa ubaoni, mwalimu akatoka nje (nafikiri alienda uani)...! Then, jamaa akainuka na kwenda mezani, akaling'ata lile andazi na kumezea soda ile pia...! Akarudi kukaa kule nyuma ya darasa...!
Kidogo mwalimu akarudi na kukuta andazi lake limemegwa....! Aliongea hadi kimeru (kikwao)...! Wale watoto wanne wanaojua kuongea kiswahili; akiwemo jamaa, walijitetea na kupewa kazi maalum kila mmoja...! Jamaa alipewa kazi ya kuhakikisha kila atakayechapwa atarudi kuunga mstari tena na kusubiri kuchapwa tena, wengine walipewa kazi ya kukata fimbo....! Nakumbuka siku hiyo tulichapwa hadi saa ya kwenda nyumbani....! Hakuna hata mmoja aliyedhubutu kumnyooshea jamaa kidole, kisa ungepita njia gani baadaye....!
😀😀