Niliacha viatu nje ya daladala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Niliacha viatu nje ya daladala

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by lidoda, Nov 18, 2011.

 1. lidoda

  lidoda JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2011
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 80
  Nimeamini makonda wa daladala tangu wanapoondoka majumbani mwao hadi wanapopanda kitandani, wanakutana na vituko vingi katika shughuli yao hiyo. Wapo abiria waelewa na wapo wasioelewa na kusababisha usumbufu usio wa lazima kwa makonda hao.
  Kuna wakati hukutana na mambo ambayo si rahisi kuyapatia majibu. Kutokana na matukio ya kutwa, wakati mwingine tunawaonea makonda na kuwaona ni wakorofi.
  Hii ilitokea hivi majuzi, nikiwa nimesimama Kituo cha Daladala cha Mabatini, Mwanza. mara daladala toka Igoma kwenda Mjini ilisimama kituoni.

  Aliteremka bibi kizee mmoja wa makamo aliyeonekana kutafuna magunia mengi ya chumvi.

  Umri wake ulikimbilia miaka sabini na ushee kutokana na muonekano hata kutembea kwake alipinda mgongo kidogo.
  Baada ya kuteremka, konda alitaka kuruhusu gari liondoke, yule bibi alimuita konda.
  Bibi: Mjukuu wangu ndala zangu ziko wapi?”
  Konda: Bibi acha kunizingua, hukupanda na ndala ndani ya gari.”
  Bibi: Acha utani, ndala niliziacha nje kabla ya kuingia, nateremka sizioni.”
  Konda: Sasa mimi nifanyeje wakati wewe umeziacha mwenyewe?”
  Bibi: Huondoki mpaka unipe ndala zangu.”
  Bibi alimng’ang’ania shati konda, jambo lililozua kituko pale kituoni.

  Ilibidi bibi apewe fedha za kununua ndala lakini alizikataa akitaka ndala zake za awali.

  Kila konda alivyombembeleza, bado bibi alitaka ndala zake alizonunuliwa na mjukuu wake, tukio lile lililovuta watu na kuonekana kituko ‘live’, lilifanya abiria wachelewe kwenye shughuli zao.

  Ili kumaliza utata, alijitokeza mtu mzima mwenye busara kumshauri konda akanunue ndala amletee, konda alifanya kama alivyoagizwa na yule bwana mwenye busara alimpa bibi ndala zake ambazo alizipokea.
   
Loading...