ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,368
- 50,737
Nataka niwe na mwili mkubwa yaani mrefu halafu mnene kama wacheza basketball, tayari urefu wa kutosha ninao Ila bado mwili kimbau mbau, nishauriwe nifanyeje ili kupata mwili naohitaji. Kuna mtu aliwahi kuniambia viko vyakula huko masuper market vyenye nutrients za kujenga mwili haraka. Kwa anayejua Tafadhali anaisaidie Jina la chakula hicho na nyongeza ya hivi vya asili sio mbaya, pia vitu vya kuzingatia kama ni hela ya kupata meals hata TANO Kwa siku sio tatizo ratiba ya kufuata . Nawasilisha Kwa shukrani