Niko njia panda

Niko njia panda

BILGERT

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2015
Posts
6,533
Reaction score
11,027
Habarini za wekend wadau,

Naombeni mnisaidie kimawazo.umri wang ni miaka 24 ni muajiriwa serikalin huku Dodoma, wilaya ya Mpwapwa,lakini home ni Iringa nina girlfriend wangu ambaye yupo chuo cha RUCO kilichopo iringa, nmedumu naye takribani mwaka mmoja na nusu, ingawa tumepitia changamoto nyingi sana lakini tumeweza kudumu pamoja na hatimaye kusonga mbele.

Siku ya tar 17 alinipigia simu kunijulisha kuwa tarehe 18 ambapo ni siku ya ijumaa ana TEST,,hvo akimaliza hyo test ataangalia utaratibu wa kusafiri ingawa chuo kinafungwa tar 23, aliniambia kuwa atafanya hivo kwa sababu hakutakuwa na mishe yoyote, hivo akiendelea kubaki hapo ataboreka.

Mimi nikaridhia, siku ya jana jioni akanijuza kuwa kesho ambapo ni leo kuwa atasafiri kama alivonijuza mwanzoni na aliniambia kuwa ataondoka na gari ya sa 12, akaniambia kuwa anaenda Dar es salaam kusalimia ndugu ila kwao ni MOSHI mimi nikaridhia, nikamtakia safari njema mida ya saa nne tulifanikiwa kuongea zaidi na kutakiana usiku mwema. PICHA NDO IKAANZA KULIVO KUCHA.

Nlipanga niwah kumuamsha ili awahi hyo gar ya sa 12,lakini nkajikuta nmepitiwa na usingizi.nmekuja kuamka baada ya sa 12 asubuh,ambapo nlishangaa kutokukuta sms wala call ya kunijulisha kama kaondoka ama la.nliamua kumtumia text, kumuomba samahan nanukuu SAMAHANI NMECHELEWA KUAMKA, NLIPITIWA NA USINGIZI HVO KUSHNDWA KUKUAMSHA KWA WAKATI ILI UWAHI GAR, ikapokelewa lakini haikujibiwa nikaamua nitume tena text ya kumtakia safari njema, nayo ikapokelewa lakini haikujibiwa nkaendelea kuvuta subira mpaka mida ya sa tano,lakini bado alikuwa kimya.

Nikaamua nimpigie simu, nimejaribu kama mara 20 kwa kutumia namba yangu ya voda, naambiwa namba busy nikahisi kuwa AMENIBLOCK lakini nikapuuza hilo wazo,nikaamua nitumie tena namba yangu ya Tigo lakini nlipata matokeo yaleyale nliamua kujipa moyo na kuamini kuwa wenda anaongea na simu nyingine nikawa natuma tu sms zinaonyesha deliverd lakini hazijibiwi.

Nimekaa saa moja na nusu nimemtafuta tena lakini matokeo ni yaleyale nikaamua kuingia WHATSAPP nikaangalia namba yake anayotumia humo wasap ambapo mara ya kwanza ilikuwa inaonyesha last seen,status pamoja na profile picture lakini vyote hivo havionekani saivi nikawa bado siamini kuwa AMENIBLOCK ghafla likanijia wazo,la kutaka kufanya confirmation,binafsi wasap natumia namba ya tigo sijawahi badili namba na yeye anafahamu hivo, niliamua kwenda kwenye account yangu ya wasap na kubadili namba, nikaweka namba ya voda halafu nikarefresh nikarudi tena kuangalia ileile namba yake anayotumia wasap maajabu ndugu zangu, nikakuta profile picture ipo kama kawaida na last seen inaonyesha ni saa nane na dkka 50 mchana huu hakika nmejikuta natetemeka,na sijataka kuliamin hili tukio nmekuja kuhakiki kuwa hata namba yangu ya wasap ameiblock pia.

Nisaidieni kimawazo ndugu zanguni, nifanye nini maana kiukweli nashndwa kuamin sijagombana naye zaidi ya changamoto za kawaida katika mahusiano pia sijaelewa kama kasafiri ama laa.

NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWENU NYOTE
 
Kwanza amini kama ashakufanyia hivo. Hawa viumbe hawana bima, kua mwanaume fanya maamizi magumu ya 'kumsahau' ashapenda kwingine huyo
 
Duh pole ndo mapenzi yalivyo kaka.Kuwa mpole atakucheki akiwa free si unajua huu msimu Wa sikukuu una mambo mengi.
 
Duh pole ndo mapenzi yalivyo kaka.Kuwa mpole atakucheki akiwa free si unajua huu msimu Wa sikukuu una mambo mengi.

Nashkuru kwa ushaur sista,lkn sikukuu ndo imepelekea anifanyie hvo?
 
Kwanza amini kama ashakufanyia hivo. Hawa viumbe hawana bima, kua mwanaume fanya maamizi magumu ya 'kumsahau' ashapenda kwingine huyo

Ahsante kwa ushaur mkuu
 
Ukisubiri umkute laivu Na MTU utakesha, ushapata jibu amua. hivi viumbe hatutoki navyo sayari moja wanajifanya wa akili sana
 
mpaka kufikia Hapo nadhani jibu unalo lakini hutaki kuliamini kama hilo ndio jibu.. Cha kufanya ni wewe mwenyewe kukubali kuwa Huyo ameshakuponyoka na Amekwenda kwa anayestahili.
 
Every relationship has a chaser, and the chased. You're the chaser, my friend. Now relax, if you're worth it, she'll get back to you and explain everything.
 
He he heee Umenikumbusha mbali ndugu yangu

#nliamua kwenda kwenye account yang ya wasap na kubadili namba,nkaweka namba ya voda.halafu nkarefresh nkarud tena kuangalia ileile namba yake anayotumia wasap....maajabu ndugu zangu,nkakuta profile picture ipo kama kawaida na last seen inaonyesha#

Mpaka hapo majibu unayo, hataki mawasiliano nawewe kwa wakati huo so, either umsubiri mpaka atakapoamua or umpotezee tu au umtolee uvivu umpe makavu laivu mshenz wa tabia huyo
 
naomba nikuulize maswali: mara ya mwisho kuwakumbuka wazazi wako ilikuwa lini? mara ya mwisho kuwapigia wazazi ilikuwa lini? mara ya mwisho kufikiria uje kuwa na nyumba yako ilikuwa lini? mara ya mwisho kufikiria kuja kuwa unamiliki angalau kampuni yako ni lini? mara ya mwisho kufikiria angalau ukaongeze elimu ili uhame mwanghalanga au mpwapa ttc ilikuwa lini?
 
Bosi bila kumung'unya maneno umegongewa.....hiyo night wlikuwa analiwa............ndo maana hakutaka usumbufu wako kwa jamaa aliyekuzidi mbinu na utaalamu...........ukipenda amini ukiona haiwezekani fanya mtandao ulikuwa unasumbua
 
Duh...Mkuu,wakati unaandika Hii thread ulikuwa unawahi wapi?
Anyway,labda ni Hasira tu,Mwaka ukiisha atarudi.
 
naomba nikuulize maswali: mara ya mwisho kuwakumbuka wazazi wako ilikuwa lini? mara ya mwisho kuwapigia wazazi ilikuwa lini? mara ya mwisho kufikiria uje kuwa na nyumba yako ilikuwa lini? mara ya mwisho kufikiria kuja kuwa unamiliki angalau kampuni yako ni lini? mara ya mwisho kufikiria angalau ukaongeze elimu ili uhame mwanghalanga au mpwapa ttc ilikuwa lini?

nmekusoma mkuu,lkn ingependeza kama ungenipa mawazo...juu ya hili linalo nikabili
 
Ukweli ni kwamba inakera sana. Alitakiwa akujulishe kuwa kafanya maamuzi ya kubadili gia angani.

Ingawa siyo vizuri kuongea naye, nakushauri kama unaweza kumtafuta kwa namba nyingine kabisa, mpigie halafu usikie anajikanyaga nini. Vinginevyo, utakuja kuletewa hadithi za kuibiwa simu na upuuzi mwingine ili uendelee kuwa kwenye waiting list.

Ni vizuri kuhakikisha (kama inawezekan) ili uanze mwaka kwa amani!

Inatia hasira sana aisee
 
Bosi bila kumung'unya maneno umegongewa.....hiyo night wlikuwa analiwa............ndo maana hakutaka usumbufu wako kwa jamaa aliyekuzidi mbinu na utaalamu...........ukipenda amini ukiona haiwezekani fanya mtandao ulikuwa unasumbua

Nmeumia sana mkuu,lkn mpaka saiv asinitafute kweli? maana before hatuna ugomv wowote zaid ya changamoto za hapa na pale
 
Back
Top Bottom