Niko njia panda ushaurii wenu tafadhari

akaishi kaburini huko hatachanganyikana na dini zingine pambafff

Aisee ni kweli mkuu maana kuna watu wana akili fupi sana hapa duniani.. Unawezaje acha mtoto wako wa kumzaa ateseke akose baba ake au mama ake kisa kitu kinachoitwa dini wakati mwingine wapuuzi tu tena wazinzi kama sisi au kuliko sisi wanatuongoza.. Shit..!!! Mm naona muhimu zaidi ukamuamini Mungu yupo na kufanye yale yaliyo mema..

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Nilitegemea umshauri binti afuate dini ya mmewe....

Mwanaume kufuata matakwa ya mwanamke ni uhayawani na upumbavu.

Bora kila mmoja abaki na dini yake na kama laa haiwezekani.... ndoa na ifariki dunia.

Nimemshauri kutokana na alivyojieleza, amesema yeye ni muislam na anapenda dini yake. Kumshauri abadili dini ni kosa katika dini yake. Any way huu ulikuwa ni ushauri kwa mtoa mada tu si kwa watu wote.
 
Mim ni msichana mwenye miaka 25,nilikua na mpenzi wangu ambae nampenda saana tumesaidiana mambo mengiii sanaa,,kwa sasa tuna miaka saba kwenye mahusiano,,kwetu mi tuna hali ngumu kidogo alinisomesha chuo hadi nikamaliza,,nilipoumwa aliniuguza japo kua ana mapungufu yake ni mtu wa michepuko ila hua anakiri na kuomba msamahaa namsamehe imekua mara nyingi najua anachepuka kama mara kumi hivi,,,,maisha yakaenda tukapta mtot mmoja wa kiume, na tunaishi wote sasa kwa furaha sana nasasa anataka tufunge ndoa,, tatizo linakuja ye n mkristo m n muislam nilielelewa mazingira ya dini,nampenda sana yeye pia naipenda dini yangu( uislamu) nifanye nini? Na pia wazaziwangu hawapendi tunavyoishi wanataka nirudi nyumbani mi naona kazi kumuacha nampenda sana na amekua mtu mwema kwangu,,,,pia natamani mtot alelewena wazazo wote wawili naombeni busara zenu niko njia panda.

hivi kwani nowday's dini ndo utofautisha ndoa au wapenzi?!mkuu elimu yako haijakusaidia wala kukukomboa.
 
Hakuna ungese ktk dn kama umekata tamaa na dn yk bac n ww dunia n mapito ikikuuma pasuka ila hlo n haramu halipo pole sn fuata mafundsho ya dn yk
 
Huenda wengne n wapagan uzungu unawapoteza ndo maana hata ushoga c ttz,suala ni miongozo ya dn uksukumwa na utash kila jambo utaona sawa anal sex;oral sex,polandry,wanafamilia kufanya ngono wao kwa wao,haya yote n kudharau dn na kusahau life after death,halafu huyo mtu kaomba ushaur sasa akil za kuambiwa changanya na zako uctake usemalo ww liwe ndo suluhsho ameomba ushaur dnt b egoist
 
Hii ni ajabu,kwa hiyo wakati jamaa anakukamua hadi kukuzalisha wazazi walikua hawaoni? Au dini yako inaruhusu kukamuliwa hadi kuzalizwa na mtu yoyote ila sio ndoa?

Kwenye kuolewa na asie muislam ni dhambi,ila kukulala na kukuzalisha sio dhambi.

Mbona wazazi wako hawakukukataza wakati umeanza nae au kwa kua alikua anakupa pesa unawapelekea,anakusomesha,analisha familia hawakuona kama ni mkristo,sasa baada ya kuona umemaliza masomo na wao kula hela ya jamaa vya kutosha ndio wanagundua sio muislam.

Huu ni ujinga wa hali ya juu sana.
 
UISLAMU unakataza mwanamke wa kiislamu kuolewq na mkristo HAIFAI muogope MUNGU hata kama huyo mtu n mwema ila hlo jambo ni haramu kila dn ina mipaka yake.

Sawa,nilikua sijui,kumbe kuolewa tu ndio kumekatazwa ila kuzalishwa,kulalwa ni halal,safi sana.
 
Hakuna njia panda kama hio dada yangu ni vigum sana mtu kuibadili imani yake kisa mapenzi kwa mwanadamu ni kama umemsaliti mugu unae mwamini!
Kwetu sisis wakristo tunaweza kuwa na ndoa na mtu asie mkristo isipokua ni lazima ndoa hio ifungwe kanisani na kwa shart la watoto kuwa wakristo, kama mna liweza hilo jaribuni kuliko kukaa bila ya ndoa kwani ni dhambi hata imani yako na dhani inajua hilo. Lakini dada ushauri tu dada kwa nini usiichague njia sahihi ya kufikia Mungu ambayo na Ukristo? Jaribu kuujua Ukristo jinsi ulivyo rahisi na rafiki wa mwanadamu na hata tatizo kama hilo lisinge kua mtihani kwako.
 
Wewe ni mpuuzi kwelikweli yaani miaka yote saba hukujua kama ni Mkrito tena na mtoto juu???? Huna hata haya fata dini ya mumeo na mfunge ndoa vinginevo ulikuwa una lako jambo ulilofata si mapenzi hata chembe
 
Kama ndoa baina ya dn mbil imekatazwa uzinifu ndo ukabaliwe kaka km?umekuwa acha utoto kaka.
 
Hii ni ajabu,kwa hiyo wakati jamaa anakukamua hadi kukuzalisha wazazi walikua hawaoni? Au dini yako inaruhusu kukamuliwa hadi kuzalizwa na mtu yoyote ila sio ndoa?

Kwenye kuolewa na asie muislam ni dhambi,ila kukulala na kukuzalisha sio dhambi.

Mbona wazazi wako hawakukukataza wakati umeanza nae au kwa kua alikua anakupa pesa unawapelekea,anakusomesha,analisha familia hawakuona kama ni mkristo,sasa baada ya kuona umemaliza masomo na wao kula hela ya jamaa vya kutosha ndio wanagundua sio muislam.

Huu ni ujinga wa hali ya juu sana.

Hebu shangaa na wewe mambo mengine bana hata kuelezea unaweza ona aibu
 
Hapa ndo inapokuaga taabu mtu anaposema anaipenda sana dini yake ili hali keshaiasi kwa kufanya alichofanya anyway ngoja nisifike huko. Mkuu hapo fanyeni maamuzi yenye busara kama kweli mnapendana basi fungeni ndoa lkn jiulize je dini yako inaitambua ndoa ya serikalini.
 
Nendeni kanisani mkafunge ndoa ya mseto.mimi rafiki yangu akifunga ndoa kanisani yeye mkristu mkatoliki mumewe muislam na hakuna akiyebadilisha dini sasa ni miaka 20 wako vizuri tu!hii kitu watu wengi hawajui ila ni ruksa kabisa
 
Nendeni kanisani mkafunge ndoa ya mseto.mimi rafiki yangu alifunga ndoa kanisani yeye mkristu mkatoliki mumewe muislam na hakuna akiyebadilisha dini sasa ni miaka 20 wako vizuri tu!hii kitu watu wengi hawajui ila ni ruksa kabisa
 
Mapenzi hayachagui dini wala kabila sasa nikushauri kitu kimoja mdada mnachotakiwa kwanza mfunge ndoa selikarini ili uishi kihalali kabisa na mpenzi wako sasa baada ya hapo mtakua na maamuzi yenu nyie wenyewe kama familia yaan mtajiongoza wenyewe ktk mambo yenu binfsi
 
Tuna utofauti wajina wangu faith.Kuhusu hilo swala la michepuko hiyo tabia unayomlea yakuendelea kumsamehe kuna siku utaletewa mwanamke ndani.Mfanye atulie na wewe tu na kuhusu ndoa fata moyo unachokwambia maana huyo ndio utakayespend nae maisha yako so uamuzi uufanye mwenyewe kwa kina
 
Kama ni muislam unahitaji toba ya kweli kwa sababu hayo uloyafanya kuzaa nje ya ndoa, kuwapinga wazazi wako, na mengine ni makosa makubwa. Kama kweli unaupenda uislam na unauamini kuwa ndio dini sahihi msilimishe na huyo mtu wako kama akupenda kweli atasilimu. Any way ushahidi wa kipi unakipenda Zaidi kati ya dini yako na mwanamme utaonekana katika uamuzi utakaochukua.
Akili kichwani mwako

Hapa ndo nashindwa kuwaelewa ndugu zangu wa upande wa pili.. Mimi nakuoa wewe alafu nisilimu?! kwan wasichana wameisha?!.. wakristo ni rahisi sana kubadilisha kuliko waislamu najiuliza sana hili swali sijawahi pata jibu..
 
Back
Top Bottom