kulipa fadhila si ndo kupenda pia? ama?
Mpendwa ee Labda ushauri huu mzuri kwako...Mim ni msichana mwenye miaka 25,nilikua na mpenzi wangu ambae nampenda saana tumesaidiana mambo mengiii sanaa,,kwa sasa tuna miaka saba kwenye mahusiano,,kwetu mi tuna hali ngumu kidogo alinisomesha chuo hadi nikamaliza,,nilipoumwa aliniuguza japo kua ana mapungufu yake ni mtu wa michepuko ila hua anakiri na kuomba msamahaa namsamehe imekua mara nyingi najua anachepuka kama mara kumi hivi,,,,maisha yakaenda tukapta mtot mmoja wa kiume, na tunaishi wote sasa kwa furaha sana nasasa anataka tufunge ndoa,, tatizo linakuja ye n mkristo m n muislam nilielelewa mazingira ya dini,nampenda sana yeye pia naipenda dini yangu( uislamu) nifanye nini? Na pia wazaziwangu hawapendi tunavyoishi wanataka nirudi nyumbani mi naona kazi kumuacha nampenda sana na amekua mtu mwema kwangu,,,,pia natamani mtot alelewena wazazo wote wawili naombeni busara zenu niko njia panda.
Kulipa fadhila sio upendo halisi
Hauna zile cheche za mahaba/mapendo
Ila anawaza alipptoka anashukuru na kushikamana......na ndio.unapozaa upendo wa "siwezi kumuacha alinisaidia sana"
Mapenzi hayaangalii dini so follow your heart
UISLAMU unakataza mwanamke wa kiislamu kuolewq na mkristo HAIFAI muogope MUNGU hata kama huyo mtu n mwema ila hlo jambo ni haramu kila dn ina mipaka yake.
Miafrika kama ww ni buree kabisaa..!! Unashindwa kupata mahusiano bora na maisha ya furaha kisa dini walioleta wangese tu kama wewe..!! Hivi inakuaje unakua na akili kama hii???
Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Kama ni muislam unahitaji toba ya kweli kwa sababu hayo uloyafanya kuzaa nje ya ndoa, kuwapinga wazazi wako, na mengine ni makosa makubwa. Kama kweli unaupenda uislam na unauamini kuwa ndio dini sahihi msilimishe na huyo mtu wako kama akupenda kweli atasilimu. Any way ushahidi wa kipi unakipenda Zaidi kati ya dini yako na mwanamme utaonekana katika uamuzi utakaochukua.
Akili kichwani mwako