Mim ni msichana mwenye miaka 25,nilikua na mpenzi wangu ambae nampenda saana tumesaidiana mambo mengiii sanaa,,kwa sasa tuna miaka saba kwenye mahusiano,,kwetu mi tuna hali ngumu kidogo alinisomesha chuo hadi nikamaliza,,nilipoumwa aliniuguza japo kua ana mapungufu yake ni mtu wa michepuko ila hua anakiri na kuomba msamahaa namsamehe imekua mara nyingi najua anachepuka kama mara kumi hivi,,,,maisha yakaenda tukapta mtot mmoja wa kiume, na tunaishi wote sasa kwa furaha sana nasasa anataka tufunge ndoa,, tatizo linakuja ye n mkristo m n muislam nilielelewa mazingira ya dini,nampenda sana yeye pia naipenda dini yangu( uislamu) nifanye nini? Na pia wazaziwangu hawapendi tunavyoishi wanataka nirudi nyumbani mi naona kazi kumuacha nampenda sana na amekua mtu mwema kwangu,,,,pia natamani mtot alelewena wazazo wote wawili naombeni busara zenu niko njia panda.
Wew nawe ni mzigo....na mpaka hapo wew ni mtumwa wa fikra...yaan upo upo tuuu, una elea elea tuu!
Miaka saba mnahusiana, tofauti zenu ulizijua na wazaz wako walizijua, mtoto mmezaa, bado hamjafunga ndoa...kikwazo ni wew na msimamo wako na wazaz wako ni dini...kweli!!! Mwanaume wako ni wa michepuko mara kumi umejua na umevumilia...Kama tatzo ni dini..mbona huondoki????
Mwanaume wako ataoa karibuni...ila hatakuoa wewe. Ww utaolewa na dini yako. Huko anakochepuka mara kumi ndo anaweka mambo yake sawa...na sababu ya nsingi ya kuchepuka...anayo. Nijuavyo mm, mwanamke kwenye suala la mapenz na ndoa...hanaga dini. Yeye hufuata aendako bwana. Ameku*tongo*za, amekuposa,amekuchukua kwake, amekupa mimba....ayo yote umekubali....mizengwe sada yatoka wapi??? UNAPIGWA CHINI.
HABARI KAMA YAKO....INANIHUSU. Ucje ukawa ndo wew afu tena nakoment mm. Mwishoni nataka kukuposa tukafunge ndoa kanisani....wew unaniambia oooh wazaz wangu ni ma-alwatan, mara ooh sisi waislam ni mwiko kubadili dini wazaz watanitenga, kwani sasa utaishi nao milele??? Haya mimba hiyo, umezaa, nakuulza utayari wako kwenda kanisani...unasema kama vp tufunge ndoa serikalini...mim sitaki...na wew hutaki kamisani.
Haya sasa, taka yangu na taka yako...IPI NI TAKATAKA??? Nimesema poa, sikuoi ila nitalea mwanangu, nakuchukua mpaka kwetu, nakutambulisha kwa wazazi wangu..wanamtambua mtoto...wanakushauri ufuate ya mume kama uko radhi...unasema nop! Napata safar kikaz...huko nakosa mawasiliano nawe miaka mitatu. Narudi nakuta umenuna...nakubembeleza...unanielewa. Nakuomba mambo, unanipa, nakuuliza tena twende church wasema nop. Mwanangu unempa jina la kiislamu na la ukoo umempa la babako...kisa miaka mitatu nimekutelekeza....na vile nimesema sifungi ndoa ya kiislam/ kiserikali ndo tafsiri nitamchukua mtoto nikuache na wew umri umesonga.
KWA NINI UNAFANYA MAMBO ASIYOTAKIWA KUFANYA MTU MWENY AKILI TIMAMU KAMA WEWE??? Kwa nn kunizungulusha zungulusha mfano wa pia??? Kwa nn unanitega...wakati wajua mm nategua mitego yote na ndio maana nikakupata na kuwa nawe hadi leo??? Kwa nin huwezi kunifuata tena kama mwanzo.??? Kwa nn unakaa mkao huo wa hatari kwako...mguu mmoja ndani, mmoja nnje???
KAMA SI WEW TULI-SHARE...Fanya fasta mwambie akuoe muishi kwa dhiki na faraja. Fuata dini yake utakuwa salama na mwenye furaha. Mpende moja kwa moja...na siyo nusu nusu na nusu unawaachia wenzako. Unawaita wenzako michepuko....na wew ni mchepuko coz hajakuoa. Hamia airtel dadangu...uinusuru furaha ya maisha yako mafupi yalobaki. ALONIFANYI VISA KAMA VYAKO....MIM NILIPIGA CHINI YEYE NA MWANANGU. Mwenyw alidai ana kazi yake..hashindwi kulea..na kwamba mwanangu atakuja kwangu akiwa na ndevu kama KANUMBA. MM naitwa Halelluya....halafu mwanangu anaitwa Athunani...bila ridhaa yangu.....
SIKUSUBIRI USHAURI...NILIMPIGA CHINI. Na sirudi nyuma. Na wew unaelekea huko...NJIA NI MBILI TUUU, CHAGUA MOJA ILIYO SALAMA NA YA KUKUFAA.