Niko njia panda ushaurii wenu tafadhari

Niko njia panda ushaurii wenu tafadhari

s_faith

Member
Joined
Oct 29, 2014
Posts
9
Reaction score
4
Mimi ni msichana na Miaka 25,Nilikua na mpenzi wangu ambae nampenda saana tumesaidiana mambo mengi sanaa,kwa sasa tuna Miaka saba kwenye mahusiano kwetu mi tuna hali ngumu kidogo alinisomesha Chuo hadi nikamaliza.

Nilipoumwa aliniuguza japo kua ana mapungufu yake ni mtu wa michepuko ila hua anakiri na kuomba msamahaa namsamehe imekua mara nyingi najua anachepuka kama mara kumi hivi,maisha yakaenda tukapta mtoto mmoja wa kiume, na tunaishi wote sasa kwa furaha sana.

Sasa anataka tufunge Ndoa,tatizo linakuja yeye ni Mkristo mimi ni Muislam nilielelewa mazingira ya Dini,nampenda sana yeye pia naipenda dini yangu( uislamu) nifanye nini

Na pia wazaziwangu hawapendi tunavyoishi wanataka nirudi nyumbani mi naona kazi kumuacha nampenda sana na amekua mtu mwema kwangu pia natamani mtoto alelewe na wazazo wote wawili naombeni busara zenu niko njia panda.
 
Mkuu dini sio kiwazo kam akweli mnapendaneni.... unaneni na wazazi wa pande zote mbili muweke sawa.
 
Mapenzi hayaangalii dini so follow your heart
 
Kwanza naomba ujitambue; Pili toka umezaliwa wewe unapenda tu, yaani unapenda Dini yako,unapenda kusoma, unampenda Mwenza japo kuwa mzinzi !! huoni hapo ushakuwa mteja wa nafsi yako?
Sasa jipange kiutu uzima na uyatazame maisha yako kwa upeo na busara na hekima.... jibu utalipata mwenyewe bila kushauriwa humu.
kila la heri dadangu.
 
mwanzo mbaya na maamuzi yasiyo sahihi ni chanzo cha watu wengi kujuta...
 
sometimes sio lazima ufate kila watakachokwambia wazazi, kwa vitu kama hivi angalia moyo wako, hao wazazi hawajali hata utu basi, kaka wa watu hata kama umesema ana michepuko lakin amejua kukujali, hajakusahau katika maisha amejitolea vya kutosha leo ukaangalie wazazi, come on bana, hata laana haitokufikia kwa style hii........ any way choose your destiny
 
Swala La Ye Kuchepuka Ni Mengineyo. Na Hongera Kwa Kutolifatilia Sana. Swala La Ndoa Maamuz Unayo Mwenyewe. Kama We N Binadam Na Una Uta Ndan Bas Waweza Elewa M2 Mwenye Upendo Wa Dhat, Kuthamin Na Kujali, Na Hayo Ndo Muhimu. So Amua We Ulipe Fadhira Na Upendo Mwoneshe , ANAKUPENDA. Usije Kua Wale Wanasomeshwa Na Kuchkichia Mitin. Unaanza Kutafuta Sababu. Bila Shaka Mpaka Unaamua Kuish Nae Na Kuzaa Ulikua Na Malengo Na Ulijua Mbelen Kuna Nin Na Ni Nin Unafanya. Ungetushirikisha Kabla Hata Ya Kuzaa. Fata Dini Yakeee. Mwanamke Hana Din
 
Kama ni muislam unahitaji toba ya kweli kwa sababu hayo uloyafanya kuzaa nje ya ndoa, kuwapinga wazazi wako, na mengine ni makosa makubwa. Kama kweli unaupenda uislam na unauamini kuwa ndio dini sahihi msilimishe na huyo mtu wako kama akupenda kweli atasilimu. Any way ushahidi wa kipi unakipenda Zaidi kati ya dini yako na mwanamme utaonekana katika uamuzi utakaochukua.
Akili kichwani mwako
 
Sijui unampenda sana au unalipa fadhila

Kila mtu abaki na dini yake mkafunge ndoa ya serikali

La sivyo mtatukuu huku hamjaoana kisa wazazi
 
Nendeni kwa mkuu wa wilaya mfunge halafu kika mmoja na dini yake. Lakini mwisho mfuate yesu. Nipm nikupe counselling
 
Nenda kafunnge ndoa kanisani kwakuwa kuruani inamtambua Yesu haina shida
 
Ukisoma katikati ya mistari inaonesha kwamba, linalokufanya uwe nae pamoja ni kulipa fadhila, mwisho wa siku maamuzi ni yako mwenyewe!
 
Ushauri mzuri utaupata kwa wazazi wako, ipo siku utanikumbuka usipozingatia ushauri wa wazazi
 
Dunia ni yako chaguo ni lako fanya vile upendavyo...unaweza funga ndoa ya Serikali pia.
 
Back
Top Bottom