Niko njia panda, ushauri tafadhali

Niko njia panda, ushauri tafadhali

Mtoto wa Golden Paste

Senior Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
166
Reaction score
121
Niko kwenye mahusiano na single mother yapata miezi mitatu Sasa, na lengo lilikuwa nimuoe. Huyu mwenzang naona kidogo hajatulia maana nilifuma SMS kwenye simu yake akiwa bado anaendelea kuwasiliana na mpenzi wake wa zamani nikauliza akapoa kidogo na kunambia kuwa jamaa amemtafuta kwa lengo la kumjulia hali. Ana mtoto mmoja mpaka sasa na umri wake ni miaka 20 hivi.

Wiki moja iliyopita sikuweza kuwasiliana nae ndani ya kama siku 5,maana kila nikituma SMS na ata nikimpgia simpati hewani nikashindwa kumuelewa kabisa. Siku ya jumatano alinipigia simu na kunijuza kuwa yuko Moshi kwa dada yake ikabid nimuulze ni kwa nini kaondoka bila kunipa taarifa lakin jibu lilikuwa "nimeondoka ghafla pia nilishindwa kuja kukuaga sababu nilikuw busy,naomba unisamehe" kiukwel iliniuma sana nikaona sina thamani kwake kwa lolote lile. Lakini ikabidi nimsamehe tu baada ya kuzungumza naye.

Tangu niko nae amekuw ni mtu wa kutaka pesa tu kila wakati na jana kanipigia simu nimtumie elfu 80, nikauliza ni kwa ajili ya nini anasema matumizi,nikaona isiwe kesi hiyo pesa ntamtumia jioni. Imefika muda wa saa 10 Alasiri jana nikamjuza kuwa niko nje kidog ya mji na huduma za fedha uku ni ngumu kidogo hivyo anivumilie mpaka leo asubuh ndipo nimtumie. Lakini akajibu kwa jazba"najua hunipendi najipendekeza kwako ndo maana unashindwa nitatulia shida zangu kwa wakati" Wakuu nahisi kichwa kinaanza kuuma kwa mbali nikaona hii sehemu nilipo si sahihi hata kidogo,nikatoa laini ile hewani nikaweka laini mpya hivyo mawasiliano yakaishia jana jioni.

Asubuh kaja rafiki yangu ananijuza kuwa yule binti amempigia na kumuuliza kwa nin sipatikani ama niko na mtu mwingine na tangu yeye kaondoka labda kuna mtu alishawahi kuja kwangu na mambo mengi.

Sasa niko njiapanda nimtafute ama niachane nae,msaada tafadhali
 
Mapenzi yanaumiza sana iwe ni kwa singo mama,singo baba au au mtu mwingine🤯

Unaweza kupewa ushauri lakini kumbe bdo unampenda.

Chukua ushauri mzuri utakaopewa,sikiliza moyo wako,fanya maamuzi sahihi.

Pole sana.
 
Unamjua baba wa mtoto? Ukiona hivyo karudi mwenye mtoto wanataka kulea mtoto wao wewe jiengue hata kama moyo unauma yataisha tu. Pole
 
Singo maza hajitambui na hajui anataka nini. Iwapo umeandika bila kujipendelea, hafai, achana naye

Bazazi
 
Mapenzi yanaumwiza sana iwe ni kwa singo mama,singo baba au au mtu mwingine🤯

Unaweza kupewa ushauri lakini kumbe bdo unampenda.

Chukua ushauri mzuri utakaopewa,sikiliza moyo wako,fanya maamuzi sahihi.

Pole sana.
Kweli aisii ayo mambo ni kusikiza moyo wako unakupangaje
 
pole...sana kwa kifupi wewe ni rimbukeni wa mapenzi...
ukiona mfupa umemshinda fisi ujue hakuna mnyama yeyote porini atakae uweza.

ebu wewe mwenyewe jiulize mwanaume mwenzako kamshindwa hadi amemuacha..
wewe unajidai kidume kumfuata mwanamke alieshindwa na mwanaume mwenzako...utamuweza wapi huyo...?

tumia akili kufikilia....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom