Niko njia panda! Nikate mzizi wa fitna? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Niko njia panda! Nikate mzizi wa fitna?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eeka Mangi, Jan 23, 2012.

 1. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hi ni kweli kabisa,
  Wana JF! Imenitokea na sasa niko njia panda. Ni hivi! Kuna binti mmoja kaajiriwa hapa ofisini. Wakati anaajiriwa nilikuwa sipo karibu. Niliporudi binti wa watu akawa keshajichanganya na staff. Haikupita mda naye akawa keshanizoea. Kuna safari ya kiofisi kama siku 6 hivi tulisafiri kama team. Niliporudi kukawa na kisukununu kishamwambia mke wangu kuwa namchakachua kuku mgeni. Kiukweli sijawahi kufanya lolote na huyu binti. Mama amekuwa mkali ile mbaya ooooooooooh wewe unamduu yule binti. Siku moja kamvizia akamwambia achana na mume wangu. Binti wa watua akashangaa! Muda ukapita kazi zikasonga mbele. Sasa wafanyakazi nao wameanza huyu anatunguliwa na mkuu wa kitengo! Kisa kila kitu kabla hajaamua ama kupitisha lazima aombe ushauri kwangu. Habari imefika tena kwa waziri wa mambo ya ndani kuwa sasa wamethibitisha kuwa ni kweli! Still sio kweli kuwa nimeshafanya uchafuzi!
  Binti kasikia na kanieleza! Rafiki yangu hapa kazini naye kanieleza yanayojiri department nyingine kuwa naharibu mchumba wa mtu mtarajiwa. Waziri wa mambo ya ndani kashikilia bango kwa mda sasa na kila jioni lazima aje kunipitia tuongozane home hata kama ni saa sita. Hali hii inanikera sana. Natamani nifanye termination ya huyu binti ili akatafute kazi pahala pengine lakini naona ka sitomtendea haki!
  Nimekaa na mke wangu na kumweleza ukweli lakini kaziba maskio. Juzi tu nilijaribu kuwaita rafiki zangu tuongee naye kuhusu hili. Rafiki walishauri naye binti aitwe lakini wife alipomwona tu akakataa kata kata kukaa naye meza moja.

  Shetani wangu sasa nananituma nikate mzizi wa fitna! ETI KWA KUWA NIMEITWA MWIZI NAMI SIO MWIZI BASI NIIBE ILI NIHUKUMIWE KWA NILICHOFANYA NA SIO KUHISIWA TU!

  JE NIMALIZIE WALICHOKITAKA AMA NIACHE TU SHETWANI APITE!
   
 2. h

  hayaka JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mshinde shetani acha fikira mbaya. We fanya kazi yako sawasawa na ipo siku hata huyo mkeo atajua kuwa ulisingiziwa.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Deep down wewe sio mtu mwema..

  ndo maana unazungumza ku terminate kazi ya mtu kirahisi saana

  ili tu ikusaidie wewe na mkeo mwenye wivu

  hivi unajua tabu kiasi gani kupata kazi TZ siku.hizi?????

  halafu kama hakuna baya ululiofanya iweje mkeo

  ambae anakujua vizuri kuliko sisi asikuamini kiasi hiko????

  na wafanyakazi wenzio pia wote wakusingizie???????


  hebu soma sentensi yako ya mwisho....eti umesingiziwa kwa hiyo ufanye kweli

  really??????......

  hapa umekuja kujiosha naona.....
  you are as guilty as any criminal......
   
 4. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Usijaribu hata siku moja kuumaliza ugomvi kwa kuanzisha ugomvi mwingine
  Kumalizana na huyo binti kwa kuwa umeitwa mwizi ni saw ana kumwaga petrol kwenye moto unaowaka ukitegemea utazima
  Na hapo utakuwa umezalisha tatizo la kudumu maana hutaonja asali ile kwa mara moja maana utamu utakaoupata utataka uchonge mzinga kabisa na hapo sasa utakuwa kila safari unayoenda lazima uongozane na huyo binti.
  Busara zaidi zinafaa zitumike katika kulimaliza tatizo lako na kaa vyema na mkeo.
  Kuna kitu kimoja nakushauri
  Usirudi tuu kazini mkeo amechoka na wewe umechoka ukaanza kumpa story au kukana tuhuma anazokuambia
  tafuta muda mko so relax na mkeo na mahali patulivu ambapo akili zenu wote hazina stress za aina yoyote na mweleze mkeo hali halisi
  Kwa mke ambaye ni mstaraabu ataelewa na kama ni mke asiye na busara ataendeleza ugomvi ambao kwako na kwake ni hasara
  Usikubali mwizi aingie nyumbani mwako wakati una zana zote za kumzuia maana kusema kuwa umetuhumiwa na unataka ufanye kweli ni kama kumruhusu mwizi aingine nyumbani kwako wakati una kila sababu za kumzuia
   
 5. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kama mke haelewi ww gonga tu ,hamna shida
   
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Ushauri mwingine ni balaa
  ukiufuata hata shimo utaona kama ni kidimbwi
   
 7. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ni haki yako kusema hivyo. Sina sababu ya kujikosha kote huko! I could have done it without asking my fellows as YOU! So kama na wewe umeungana kunituhumu sina sababu ya kukubishia! Ni wewe umeamua kuwa upande wao! Thanks fella!
   
 8. Shagiguku

  Shagiguku JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 400
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  kaka unasubiri nini sasa kumalizia mchezo...!!??

  hapo unachotakiwa kufanya ni kuuweka mpira kimiani na refa atarudisha kati, wakati huo wife wako ndo atajifunza kuwa wivu ni mubaya ati.....! kula maini mkuu, na kwa taarifa yako huyo binti unayefanya naye kazi keshavutiwa na wewe siku nyiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiingi wewe tu ndo unachelewesha gemu, hebu mbidue acha kuuliza maswali ambayo majibu yake unayo wewe mwenyewe, kula vitu ili uliwe na wewe vya kwako....!!!

  teheeeee teheeeeee teheee.......!!
   
 9. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  We Mangi,

  Nachukulia kwamba ni muajiriwa wa sekta ya umma , uki "terminate" bila sababu za msingi anaweza kudai fidia hiyo ofisi yako ,sasa hiyo fidia haitoki kwenye mfuko wako ni pesa zetu za kodi ambazo kila tukipata pay slip huwa zinatuuma sana tunavyokatwa wakati nchi huduma mbovu. Nakushauri ujifunze kum handle mke wako anaonesha yupo out of control.

  Au kama ni sekta binafsi basi mfikirie huyo muajiri wako ambaye amekupa ujiko wa kuweza ku terminate watu...
   
 10. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Itakua mkeo hakuamini na sio maisha hayo Kama hamuaminiani, jengine achilia mbali kumfukuza kazi Huyo bint hata kufikiri sio sawa, Huyo mkeo asijidai anakupenda Sanaa bure Hana lolote babu jinga inama ufikiri......
   
 11. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wewe unaonyesha unatawaliwa sana na mke wako...Pole sana.
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Haya mkuu
  Ushauri wako huu ni balaa
   
 13. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Funika kombe mwanaharamu apite kaka. Mambo hayo makazini yapo sana, wengine wanasingiziwa makubwa kuliko hayo.
  Huna haja ya kufanya cho chote na huyo binti, haitakusaidia chochote na pengine kukuletea balaa zaidi.

  Cha msingi ongeza upendo kwa mkeo, jipe muda na mpe mda mkeo nae kufanya uchunguzi wake, maana kwa vyovoyte atakuwa anafanya hivyo.
  Na mwisho punguza ukaribu na huyo binti, kuepuka matatizo zaidi, mweleze kuwa you need space kwa ajili ya ndoa yako. Kwake ibak mambo ya kazi tu.

  Usijaribu kuduuu naye wala usijaribu kuterminate ajira yake. It is not good idea at all.
   
 14. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Mmmmh ndugu, mbona unataka kumtumbukiza mwenzio shimoni jamani? Unamfundisha cheating hivi hivi lol
   
 15. BRO LEE

  BRO LEE JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Kama wa2 wanakusema vibaya kwa jambo ambalo hujafanya waache wasema ni suala la muda 2, ukweli utadhihirika. We wapuuze wote na endelea na taratibu zako za kazi na usibadilishe mawasiliano na huyo mfanyakazi unayetuhumiwa naye.
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kama unaelewa maana ya ubinadamu hutafanya kilicho nje ya ubinadamu! Tafakari kabla ya kutenda, binadamu tumejaliwa kuwa na utashi.
   
 17. Asnam

  Asnam JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 4,268
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  kwa ushauri huu nahisi we ni balaa
   
 18. Asnam

  Asnam JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 4,268
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  kila kitu ni taratibu mambo yatakwenda sawa i believe so ongea na mkeo taratibu wimbo utamuingia masikioni usiharakie maisha
   
 19. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #19
  Jan 23, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,454
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Kwanini usingiziwe wewe na sio mwingine, Ingekuwa utotoni sawa lakin kwa umri wenu,acha kutudanganya/kujidanganya mwenyewe na kutaka sababu ya ku justify Ufuska wako
   
 20. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,046
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  Kaka tubu kwa mkeo make hayo maelezo hata kama hamjavuana nguo tayari kuna tuhisia kwa mbali ambatwo tayari tulijengeka baina yenu wawili na yawezekana labda ulimpiga hata matachi unconsciouslly na wadau wakausoma mchezo,achana na huyo chick kabla ndoa yako haijawa ngumu,ni easy sana,kubali tu kwamba ulichelewa kumake na tayari dili limesanuka sasa inakuuma

  Ondoa timu uwanjani kaka dakk90 zimekugomea,unatakiwa kujifunza kuwa na speed of essence na very timed katika issue kama hizi make mwisho mambo hujulikana brother

  Jihadhari wakati unapanga kuukata huo mzizi usije angukiwa na tawi na likakuponda kichwa.
   
Loading...