Niko njia panda naombeni ushauri wenu.

Niko njia panda naombeni ushauri wenu.

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
7,490
Reaction score
8,305
Salaam. Kama kichwa Cha habari kinavyoeleza.nimejikuta ktk migogoro wa kifamilia kutokana na kijana wangu kumpa mimba mwanamke huko walikokuwa na kisha wakatibuana. Msichana yule kaleta Mtoto kwangu nilee mjukuu!zao la hawala!fotokopi na John mwanangu.
Sasa bibi yake anataka tumchukue eti kwa kuwa kijana hajapata kazi amemaliza digrii mjini huko...mie nimekataa hiyo mambo ya kulea wajukuu nahisi John atazidi kutuletea mizigo mingine ningependa walee mtoto wao wenyewe.lakini bibi sasa anachonga hatari,eti sina upendo kwa John.Hapa nyumbani ni vurugu tupu,eti jamani mnanishauri nini?mtu akizaa si anakuwa keshajiona ni mkubwa,na wala msichana hajalazimisha kuolewa anataka huduma tu.
Nifanye je hapo wananzengo.
 
Shkamoo babu.

Lea tu mjukuu, sasa utafanyaje babu.!!

Kijana wako alipenda ngono lakini hakuwa tayari kukubaliana na matokeo yake.(labda kama angeelekezwa vizuri haya yasingetokea)

Pambaneni na hali zenu tu maana hakuna namna

Ni maoni yangu tu plus akili za usiku
 
[emoji16][emoji16][emoji16]marahaba aka night bureini[emoji3][emoji3]
 
Ukiachana na mamake diamond, we ndo mtu wa pili nakuona kujiweka mbali na mjukuu.....babu acha roho mbaya mtoto ana raha
Ni kweli ana raha sana lakini siyo kihivyo!nikipokea huyu ataleta na wengine nadhani zipu ya John inamatatizo ya kufunguka funguka.
 
Shkamoo mkubwa

Mimi naomba kwanza uvute picha enzi za ujana wako wewe ilikuaje....?

Ni kweli kuletewa mjukuu pasipo ndoa ni kufedheeshwa hasa kwa majirani na umma unaokuzunguka afadhari kwa mtoto wa kiume angekua wa kike sijui ingekuaje

Mzee muite mwanao muweke chini na unwambie kwamba sasa ameshakua mwanaume a ajiangaikie alee mwanawe
 
Yaan huyo john anaenda kugegeda malaya uko tena peku peku afuu anakuletea zygot ulee??? Achaa kulea watoto mayai mayai,,, mpe mzigo wake akapambane mtaan ndo atajua vzur kufunga zipu za mbele,,,
 
Shkamoo mkubwa

Mimi naomba kwanza uvute picha enzi za ujana wako wewe ilikuaje....?

Ni kweli kuletewa mjukuu pasipo ndoa ni kufedheeshwa hasa kwa majirani na umma unaokuzunguka afadhari kwa mtoto wa kiume angekua wa kike sijui ingekuaje

Mzee muite mwanao muweke chini na unwambie kwamba sasa ameshakua mwanaume a ajiangaikie alee mwanawe
Marhaba.Tatizo ni huyu mama yake anajifanya kumtetea sana eti tulee tu mjukuu,kisa J hajapata kazi.wakati wa ujana kwanza ningeanza je kumruhusu mwanamke aende kwa mzee ?
 
Ni kweli ana raha sana lakini siyo kihivyo!nikipokea huyu ataleta na wengine nadhani zipu ya John inamatatizo ya kufunguka funguka.
kutenda kosa sio kosa, bali kurudia kosa. mlee huyo mjukuu wako ila kama John akirudia tena hilo kosa hapo unahaki zote za kukataa kumlea huyo wa pili.
 
Babu ni kweli umekosa ufumbuzi wa hilo jambo mpaka unakuja huku?
Aaaaah babu eeeh,acha hizo wewe lea hata ukiletewa mwingine wewe pokea na lea mpaka huyo John wako akose wa kumzalisha.
 
Aaah wapi!apambane tu hata mie nilipambana kumlea.
 
Babu ni kweli umekosa ufumbuzi wa hilo jambo mpaka unakuja huku?
Aaaaah babu eeeh,acha hizo wewe lea hata ukiletewa mwingine wewe pokea na lea mpaka huyo John wako akose wa kumzalisha.
Huna wazimu kweli!magufuliosis ndiyo ugonjwa mupyaa !!
 
Wee nawee ni Baba mti mzima mwenye kijana alomaliza degree nakuzalisha.

Umeandika ili tujue mwanao kamaliza degree?? Au umeandika tujuenkazalisha?? Au tujue umepata mjukuu??

Ikiwa wee baba kichwa chafamili Viswala vidogo dogo kam ivi vinakushinda kutatua mpaka utuletee sisi huku ,hayo makubwa utahimili???

Kweli nmeamin kadiri mtu anavyozeeka na utendaj kazi wa ubongo unashuka nahapa huwa namlaumu alosema " Mzee ni mwerevu"... Kama nimzee wee niwazee wakisasa
 
Salaam. Kama kichwa Cha habari kinavyoeleza.nimejikuta ktk migogoro wa kifamilia kutokana na kijana wangu kumpa mimba mwanamke huko walikokuwa na kisha wakatibuana. Msichana yule kaleta Mtoto kwangu nilee mjukuu!zao la hawala!fotokopi na John mwanangu.
Sasa bibi yake anataka tumchukue eti kwa kuwa kijana hajapata kazi amemaliza digrii mjini huko...mie nimekataa hiyo mambo ya kulea wajukuu nahisi John atazidi kutuletea mizigo mingine ningependa walee mtoto wao wenyewe.lakini bibi sasa anachonga hatari,eti sina upendo kwa John.Hapa nyumbani ni vurugu tupu,eti jamani mnanishauri nini?mtu akizaa si anakuwa keshajiona ni mkubwa,na wala msichana hajalazimisha kuolewa anataka huduma tu.
Nifanye je hapo wananzengo.
Fanya process mwanao aoe huyo binti kabisa ili aache kuendelea kukuletea wajukuu wa nje ya ndoa. Mtafutie capital aanze kujitegemea. Ajira zimekuwa adimu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom