Naombeni ushauri Wenu katika Nimefika Njia Panda

Status
Not open for further replies.

mdau mpya

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
471
636
Naweza kuwa sio mwandishi mzuri ila kwa minajiri ya kusaiidiwa kimawazo nitajitahidi kuelezea kisa hiki kadiri niwezavyo.
Direct to the Point:
Mnamo mwaka 2016 mwezi wa 5 tulisafiri kikazi kwenda huko nyanda za kazikazini kwa shughuli za kikazi. Kutokana na nature ya kazi yetu ilibidi tupige kambi kijiji fulani kwa muda wa mwezi mmoja na nusu kabla ya kuelekea Dodoma. Mimi najamaa zangu tukakubaliana kutafuta nyumba tupange kwa muda huo wote kama mjuavyo kijijini hakuna nyumba za kupanga ila kwa hisani ya mwenyekiti wa kijiji akafanikiwa kuongea na mama mmoja atupe upande wa nyumba yake tukae kwa muda akakubali tukamlipa chake tukaendelea na shughuli zetu.
Kupika kwetu ilikuwa ni changamoto tukakubaliana kuchangiana na kumtafuta mfanyakazi atakaye tupikia na kufanya shughuli za usafi pale home..baada ya majadirano na mama mwenye nyumba akakubali bintie aliekuwa katoka kumaliza kidato cha 4 atusaidie kazi ile na tulikubaliana tutamlipa laki 5 kwa shughuli zile kwa mwezi. Kwenye kundi lile mimi nilikuwa ndiye mwenye umri mdogo kulinganisha na wengine so majukumu mengi ya kuhakikisha binti anafanya kazi vizuri mimi nilipewa. Ishu ilikuja kuwa yule binti pale nyumbani kazi zilimlemea sana kwani alikuwa akikamua maziwa na kuhakiksha ng'ombe wao wanapata chakula mrwa ukiachana na shughuli alizopewa za wageni wake ikiwa ni sisi.
Tulikuwa tukirudi toka kazini kama sa 9/10 jioni hivi..ila jamaa zangu walikuwa wakifika wanaoga na kwenda kupiga monde mimi si mshiriki wa hizo mambo. pamoja na uchovu nilikuwa nikifika ku-buy time namsaidia yule manzi kulisha ng'ombe na kukamua maziwa (kwani shughuli ambayo nilimefanya sana nikiwa nyumbani so nilikuwa nakumbushia enzi zangu). Yule dada alikuwa hana simu mm nilikuwa na visimu viwili vya tochi nikampa kimoja awe anakitumia. Yule dada na mama mtu walinikubali sana sijui kwa msaada wangu wa kazi au ni nini..sasa kwa kipindi kifupi tukaanza mahusiano na yule dada na kwa kweli alikuwa zaidi ya mke kwangu sikutamani hata kuondoka pale. Ifahamike kuwa pale tulipata vyumba viwili so jamaa zangu baada ya kuona linaloendelea wao wakawa wanalala chumba cha nje ili wakirudi night wanaingia bila kusumbua mana yule mama alikuwa mstaarabu sana.
Yule dada kila siku muda wa kulala anakuja direct gheto kwangu. Infact nilimzoea sana yule binti na tulipendana sana mpaka tukawa tunaenda kukata majani ya ng'ombe pamoja. Frankly speaking huyu dada aliupamba moyo wangu mpaka nikatani niachane na purukushani za Dar nikapige kambi pale kijijini na mtoto mzuri.
Siku ya siku ikabidi kuondoka gari ilikuja kutuchukua pale huwezi amini yule mtoto alilia kilio cha haja kama mtoto mdogo mbele ya dereva wetu na mama yake. Niliona aibu sana siku io. Mpaka mama ake akaanza kuuliza kulikoni tena ila kwa ile company nilikuwa nampa mama alizani labda ni sababu. Dereva amepiga kick kruza ianze kuondoka mtoto analia amenishikilia mkono jamaa nusu waniache nikamwambia nikimaliza ile kazi ntarudi. Cha ajabu baada ya siku kama 5 mama ake akanipigia akisema yule mtoto anaumwa na hajawahi toka hata nje na mama ake ndiye anafanya kazi zote zimemlemea na toka niondoke yule mtoto analia daily.
Nikimpigia anakuwa na furaha na asema ananisubiri maana nilimuahidi kurudi tena. Ikabidi nianze kutafuta namna ya kumbembeleza akae sawa nikamtumia kama laki aende hospitali kama hajisikii vizuri na mama ake ndo alienda kumtolea na nasikia siku hyo alisoma text zote za mimi na yule binti na akaconect dot akaelewa mchezo.
Sasa utata ukaanza kwangu maana nina mke na watoto ikabidi nimchane live ila hata hakuonyesha kushituka tukapanga aje Dar nilichofanya nikatafuta chumba na sebule mitaa tofauti na home nikaweka furniture zote mhimu nikamnunulia na TV kabisa. Mtoto alikuja Dar nikawa nakaa nae pale kimachale huku my lovely wife haelewi mchezo uliofanyika. Mpaka kuna kipindi niliaga naenda Morogoro kwa muda wa wiki 3 kumbe niko mtaa wa pili.
Shughuli ilikuwa kwa mama ake kila siku anapiga simu arudi tulichoaamua kufanya ni kumtafuta mtu amsaidie kazi za home na nilikuwa nikimlipa. Na huyu jamaa nifahamiana ofcourse nilipokuwa kule akaniambia kuna ng'ombe wanauzwa kuna mtu anashida na hela. Huyu dada akaongea nae tukanunua tukamwambia apeleke kwa mama ake pale walikuwa wawili na sasa tuna ng'ombe saba na huyu binti ila mama mwenye nyumba (bibi mkubwa) haelewi linaloendelea. Nimekaa na huyu binti hapa mjini sasa karibia mwaka na miezi kazaa na anaheshima balaa. Yaani mtoto akileta chakula anapiga magoti kabisa utasikia napenda ukiwa na furaha muda wote mme wangu. Nilijaribu kumshawishi nimuachie kila kitu tulivyonavyo aolewe aendelee na shughuli zake amegoma na inafika kipindi anaugua kabisa inabidi nianze kumbembeleza tena.
Sasa juzi hapa ameenda kwao ameongea na mama yake kinaga ubaga kwamba mimi ndie mme wake na nina mke mwingine ila anataka kuolewa na mimi. Ikumbukwe kuwa haya mambo hatukuyapanga. Mama ake akanipigia simu ananiuliza kweli kama sita mtesa bintia ake mana nasikia nina mke mwingine. Na akasisitiza nikatoe mahari kwania ametupa baraka zote kama tumependana. Hapa ndo kidedea kimeanza nawaza mbaka sijui naanzia wapi na andika huyu binti anaujauzito na tunatarajia mtoto soon.
Sasa shida ni kuwa mimi ni mkristo siruhusiwi kuwa na ndoa mbili na nitaanzaje kuwaambia ndugu na mke wangu. Ikumbukwe kuwa niko na upendo na wote wawili sijawahi gombana nao. strictly speaking sitamani kumuumiza kati ya mmoja wao hawa they are my soul. Jamani nipeni ushauri nifanyaje hapa napenda wote wafahamiane na wapendane kama mimi navyowapenda ila kila nikimuangalia bibi mkubwa anavojitoa na kunithamini na kunijali na anavyojitolea kulea watoto wetu kumuumiza nitakuwa nimefanya si jambo la heri. Na huyu binti hana shida kabisa anasema yuko tayari kwa lolote ili awe na mimi kipenda roho chake na atamheshimu mwenzie akimkubalia mana yeye ndo ni kama ana makosa.
Msaada tutani naona nipo kwenye wakati mgumu kuamua hatima ya hili jambo
NB: Watu wataouliza nafanyaje kuwa na wote kwa wakati mmoja suala na balance tu muda na sometime inabidi nimwambie bibi mkubwa naenda kibaha kwenye vimradi vyangu nitalala huko so anakuwa hana kipingamizi.
 
Ni kweli mkuu,lakini nadhani kwa imani yetu wakristu huwezi kuoa wote. Bora abaki kuwa mke mdogo bila ndoa
Aisee kuna haja ya kureview hizi sheria za kanisa mana zitasababisha kutenda dhambi muda wote ulipopo duniani
 
Nimeona ndugu. Cha ajabu nimekosa cha kushauri. Japo ni lazima atafute mbinu amwambie baby mama wake kuwa amesababisha somewhere
Asee sitaeleweka kirahisi na isotoshe nimejijengea uaminifu kwa muda mrefu vile namhafahamu anaweza hata kuzimia
 
Wanaume bhana tuna kazi sana. Pole akina mama na akina dada. Ndio majogoo yenyewe haya yakiona mtetea tu mshipa umepanda...bila kujali nyumbani yuko nani.

Nashukuru Mungu kutuumba tulivyo ila angeweka option ya kufunga na kufungua hizi ndude ili wanaume wawe wanaziacha nyumbani.

Uumbaji wa Mungu siku zote hauna kasoro
 
Nitaumia sana. Naweza kulia sana. Lakini mwisho wa siku lazima nikubali kuwa kuna mtoto wa nje. Siwezi mchukia mtoto wa nje. Ila mume kuendelea na bi mdogo nitaona nadhulumiwa. Nadhani sitampenda "mke mwenza"
Sasa hicho ndio nadhani kitatokea, kwa sababu jamaa anatakaa wake zake wapendane na wajuane.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom