Niko njia panda nahitaji msaada wenu..

Madamem

Member
Feb 15, 2019
19
5
Salam kwenu wana JF ,

Leo nina tatizo ambalo naomba msaada wenu kimaombi na kimawazo pia.

Nimeolewa miaka 7 iliyopita mwenyezi mungu katujaalia twins wa kike na wa kiume.

Muda wote wa mahusiano yetu tulikuwa tunakaa mbali mbali sababu ya mazingiraya kazi , lakini kila baada ya miezi miwili au mwezi tulikuwa tunaonana na kutembelea familia zetu.

Tatizo langu lilianza miaka mitatu baada ya ndoa yetu , mwanzo sikuwahi kujua kabisa mwenzangu ana imani kubwa sana ya ushirikina ambayo ni chimbuko na imani katika familia yao,tunaenda kanisani pia kusali pamoja kama familia nyumbani.

Ghafla nikaanza kuona vitu vya ajabu ajabu ndani ambayo vilikuwa vimeandikwa maneno ya nisiyojua lugha yake ambavyo kumbe alikuwa anaweka kwenye maji na maandishi yakiyeyuka anakunywa yale maji.

Pia anatembea na vitu visivyojulikana kwenye wallet yake .

Pia malalamiko kuwa anarogwa na baadhi ya ndugu na marafiki ili asifanikiwe yakaanza .

Story za ajabu ajabu kama kuna ndugu yake alifariki miaka sita iliyopita eti alirogwa na mke wake na sasa amepatika kuna mganga alimsaidia kurudi katika hali ya kawaida.

Anasema kijijini kwao bila kujikinga huwezi kuishi maana 85% wote wanajihusisha na uchawi.

Kilichoniogopesha sasa anasema anataka watoto waende kijijini ili wakajue mila za kwao.

Nimekuwa nafunga na kuiombea familia yangu ili mwenyezi mungu aweze kumfungua hiki kifungo,ukimsema kuhusu haya mambo yake ananuna na kuondoka nyumbani.

Sasa nimeanza hali ya kumuogopa mme wangu naweza kushituka usiku na kubaki namtizama tu siamaini matendo yake na hizo story zake. Pia ni msomi wa hali ya juu

Nimeongea na familia yangu wananiambia niendelee kumuombea ,

Nisaidieni mwenzenu
 
Maombi huchukua muda kujibiwa hasa haya ya kwako unayo pigana na shetani direct. Usikate tamaa endelea kufunga na kusali maana Mungu wa Jacob na Elia ndiye Alpha na Omega.

Inaweza kuchukua hata miaka mitano lakini usikate tamaa. Shetani ni laghai sana, utapitia majaribu mengi.
 
Ghafla nikaanza kuona vitu vya ajabu ajabu ndani ambayo vilikuwa vimeandikwa maneno ya Quran ambavyo kumbe alikuwa anaweka kwenye maji na maandishi yakiyeyuka anakunywa yale maji.

Ulijuaje hayo maneno ni ya Quran?
Au kila maandishi ya kiarabu ni Quran? Au uarabu ndiyo uislam wenyewe? Ni Quran aya gani?
Na yakikutwa ya kingereza au ya kiswahili yaitwe maneno ya Bible?
Badili mtazamo wako upate ushauri vizuri.
 
sawa Baby Doll done
 
Maombi huchukua muda kujibiwa hasa haya ya kwako unayo pigana na shetani direct. Usikate tamaa endelea kufunga na kusali maana Mungu wa Jacob na Elia ndiye Alpha na Omega.

Inaweza kuchukua hata miaka mitano lakini usikate tamaa. Shetani ni laghai sana, utapitia majaribu mengi.
amshirikishe na mchungaji wake pia ikiwezekana ibada za nyumba kwa nyumba azihmishie kwake
 
Mmekutana watu wawili tofauti. Either ukitaka amani ufuate ushirikina na kama hutaki jiandae na vita inayokuja. Ukiweza kusimama imara utavuka na mambo yanaweza kunyooka. Ukishindwa kuwa imara unaweza poteza hata ndoa na amani yote nyumbani. Ila nakushauri mtafute mtu mzima hasa wa kiroho, anaweza kuwa mchungaji. Ukamweleza yote kisha yeye akajua mnafanyeje.
 
Asee pole sana. Nuru na Giza haviendani ukiteteleka tu unakula mzinga bora kujitenga Naye huku ukizidi kumsihi kubadilika na huku ukiomba pia huyo ni adui yako ata kama ni mmeo kwa alivyo sasa
 
Maombi huchukua muda kujibiwa hasa haya ya kwako unayo pigana na shetani direct. Usikate tamaa endelea kufunga na kusali maana Mungu wa Jacob na Elia ndiye Alpha na Omega.

Inaweza kuchukua hata miaka mitano lakini usikate tamaa. Shetani ni laghai sana, utapitia majaribu mengi.

Amina asante sana
 
Jaribu kuwa naye karibu,utajua chanzo ni nini na utapata suluhisho la hilo tatizo.Wewe ndio mwokozi wake,na usikimbie; hayo mambo yapo na yanawakuta watu pia,cha muhimu ni wewe na yeye mnaamini nini.
 
Ni kumuomba tu Mungu akusaidie kwa akili zako na nguvu zako mwenyewe hutaiweza hiyo vita.
 
Back
Top Bottom