Niko njia panda mwenzenu

Niko njia panda mwenzenu

Habari zenu wanajamvi.mwenzenu nimetokea kupendana na Kijana mmoja mtanashati na uhusiano wetu ina miaka 3. Tumejaliwa mtoto wa kike (12months old). Majuzi nimegundua bwana huyu ana katoto kamwezi sasa na mfanyakazi mwenziye.Kweli nliumia sana na ninatamani kumuacha huyu bwn nashindwa nampenda sana na pia sipendi mwanangu kuwa na baba ambayo siyo biological father! Nikimtazama mtoto naumia sna. Nimemuuliza akawa mkali sna Ila nliposimama kidete alikiri kweli na kuomba sana msamaha. Anasema alipitiwa na hiyo dada kajibebesha hiyo mimba!!! Nahofu tabia ikawa hivyo hadi ndoani kweli niko njia panda!

Kwanini ukubali kuzini? Ungesubiri kwanza uolewe, nahisi hapo hata ndoa haitakuwepo, ndio tatizo la zinaa hilo
 
Unaweza zimia Kwa ushauri mwingine japo ukweli unauma
 
jifunze ishia hapo yasije kupata makubwa zaidi.inaelekea hata kinga hatumii.kupenda kupo na kila siku wanajitokeza wanachama wapya wa kupenda na kupendana.tulizana lea mtoto huyo sio mumeo na hakuheshimu. be ware of AIDS
 
Back
Top Bottom