Annie Josh
Senior Member
- Nov 17, 2010
- 184
- 67
Habari zenu wanajamvi.mwenzenu nimetokea kupendana na Kijana mmoja mtanashati na uhusiano wetu ina miaka 3. Tumejaliwa mtoto wa kike (12months old). Majuzi nimegundua bwana huyu ana katoto kamwezi sasa na mfanyakazi mwenziye.Kweli nliumia sana na ninatamani kumuacha huyu bwn nashindwa nampenda sana na pia sipendi mwanangu kuwa na baba ambayo siyo biological father! Nikimtazama mtoto naumia sna. Nimemuuliza akawa mkali sna Ila nliposimama kidete alikiri kweli na kuomba sana msamaha. Anasema alipitiwa na hiyo dada kajibebesha hiyo mimba!!! Nahofu tabia ikawa hivyo hadi ndoani kweli niko njia panda!