Sam82
JF-Expert Member
- Feb 11, 2013
- 295
- 193
Dada pole sana ila wapaswa kuwa mwangalifu sana, ndoa sio maigizo bali ni maisha halisi ya kufa na kuzikana hivyo usifanye maamuzi kwa hisia tu. Mwanaume uliyenae humpendi kwa kuwa kishakupenda na kakuonyesha anakupenda sana na pia humpendi kwa sababu bado unasikiliza drama za mlevi wako unayemwita rafiki. Mlevi humpendi ndo maana ulimkataa alipokutongoza awali ila kwakua wanaume tu wajanja huyo kakubali kuwa rafiki akiamini adhima yake itatimia na wewe kwa ujinga wako utamtimizia tu. Mlevi anajitahidi sana kufanya mbwembwe kwakua anajua kuna mpinzani hivyo anataka akuvutie but the first guy anafanya anachokufanyia kwakua anajua yuko peke yake.
Ushauri: Kupenda siyo tabu ila kupendwa mama ni shughuli nzito, ndoa mara nyingi hulindwa na mambo mema anayokutendea mwenzi wako na hivyo huweza jenga hisia hatimae ila ukiendekeza hisia kwa sasa zitakuja kupotea siku ambapo mlevi ataanza drama na madada poa.