Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,157
- 31,334
Wakuu salaam
Sijawahi post kitu katika jukwaa hili hii ni mara yangu ya kwanza penye wengi hapakosi kitu.
Wakuu kisa changu ni hiki.
Katika pita pita zangu nilikutana na binti flani ambaye sikuwa na mpenda ila ilikuwa ni hit and run na mahusiano yetu hayakuwa more than a month.
Baada ya hapo nikaanza kumpotezea kwakuwa sikuwahi kumpenda na pia mtazamo wangu na wa kwake juu ya mambo mengi hatukuwa sawa.
Kumbe katika hicho kipindi alipata ujauzito jambo ambalo hakuniambia baada ya kuona nimekata mawasiliano naye akawa ananitumia msgs kuniuliza kwanini nimempotezea mimi nikawa ninamdanfanya kwasababu mbalimbali.
Ilipita kama miezi mitatu bila kumuona ila kuna siku nikiwa nimelala asubuhi ikaingia msg kutoka kwake ikisema kuwa nikipgiwa kwa namba mpya nisipokee. Mimi nilipuuzia tu ila baadae nikapgiwa na rafiki yangu kuwa yule binti ana mimba na inasemekana ya kwangu kwa hiyo shemeji yake hamtaki pale nyumbani.
Usingizi ulikata ghafla nikawaza nifanye nini nikawashirikisha rafiki zangu wa karibu wote wakanishauri nikae kimya nimpotezee, ila mimi nikaona hapana siwezi fanya hivyo.
Nikampgia mchana nikamuuliza una mimba, akajibu ndiyo nikamuuliza ina miez mingapi akasema anahisi mitatu na week hivi kwa hesabu zangu nkaona kweli inaweza kuwa yangu. Nikamuuliza uko wapi akasema dada yake kampeleka sehemu maana shemeji yake hataki kumuona nyumbani pale.
Mimi nikamwambia nipe namba ya dada yako, nikampigia nikaongea naye akanishauri niwe naenda mtembelea tukaongea fresh tu. So nikawa natuma ela na naenda mtembelea.
Wakati ujauzito una kama miezi saba wakaanza niambia nimchukue nimuoe, mimi sikuwa tayari nikaona tension imezidi nikapotea mazima na namba nikabadili.
Nikawa ninaenda kwa wakala nampa ela naomba utume ela kwenda namba hii anapokea anajia imetumwa na mimi lakini hana jinsi ya kunipata.
Nikaja mtafta after 2 months akaniambia alisharudi kwa dada yake akafurahi tukaongea Mungu mkubwa siku nimemtafta usiku wake akajifungua.
Baada ya siku mbili nikaenda kumuona mtoto na mama yake nikapeleka vitu nikamkuta dada yake na ndugu zake wakanikaribisha vizuri tu.
Kesho yake wakaniita wakaniuliza mdogo wao ntamuoa lini, mimi nikawambia kwa muda huo sikiwa tayari kuoa ila tu ntamhudumia mama na mtoto kwa kila kitu. Hawakuridhika lakini wakawa kimya.
Nikawa napeleka kila kitu hata mama akiugua mimi ndiye nahangaika kuanzia nguo na mambo mengine. Kwakweli nilikuwa nampenda sana yule mtoto na ikabidi tu niwe namhudumia na mama yake kila mtu alinisifia sana na mtoto alikuwa ananipenda sana.
Mtoto akiwa na miezi kama 6 hivi yakaanza maneno kuwa hawatakiwi pale kwahiyo wakawa wanafanya mpango wawarudishe moshi. Mimi nikasema nitawapangia, mama yake mzazi akanopgia simu akasema katoa ruhusa niwapangie hakuna haja ya wao kwenda moshi basi nikatafta chumba self nikanunua kila kitu cha muhimu ili aishi kwa furaha na mtoto nikaweka kila kitu nikawahamishia hapo.
Mwenyewe akafurahu hata ndugu zake wakanisifia sana kwa kumjali mdogo wao.
Matatizo ya kaanza sasa alipoanza kuishi peke yake matumizi yake yalikuwa makubwa.
Anaishi yeye na mtoto, mafta ya kupikia lita 5 week 3 yameisha gas ule mtungi saizi ya kati hata mwezi haumalizi sukari kwa mwezi anaweza tumia hata kilo 8, na mambo mengine mengi.
Nikawa nashangaa inakuwaje na kila siku nilikuwa lazima nipite kuwaangalia yeye na mtoto.
Sasa kuna siku nimepita pale nikamuuliza wewe matumizi yako vipi mbona sielewi maana nitashindwa kwa mwendo huu, akanijibu kama hutaki kununua acha tu. Nilipandwa hasira nikajikuta nampa tusi nikambeba mtoto nikaondokan naye.
Niliporudi jionu nikagonga mlango haitikii nikafungua nikamkuta kalala kitandani analia, sikumsemesha nikamweka mtoto kitandani nikaondoka.
Sikumpgia hakunipgia siku tatu mfululizo siku ya tatu nikahisi vitu ndani vitakuwa vimekaribia kuisha ngoja tu nijishushe niende huwezi amini nmefika nakuta nyumba tupu ameondoka kabeba kila kitu kasoro mti wa antena.
Mwenye nyumba akashangaa kuniona nimepigwa butwaa akaniita akaniambia alikuja mwanaume na mwanamke na gari wakapakia kila kitu wakaacha funguo za chumba.
Moja kwa moja nikajua ni shemeji yake na dada yake.
Nilikasirika sana kwa kitendo hicho nikaenda kwenda kwa dada yake kufika nakuta vitu vingine viko nje, nakuta jiko na mtungi wa guess ndivyo wanatumia kupikka friji wameweka wanatumia dada yake aliponiona akabeba ndoo ya maji akanimwagia eti akaruka kunipiga mimi nikamdaka nikamwambia mmewe mshike mkeo sijaja kupigana mmewe akanitandika ngumi basi ukazuka ugomvi mkubwa tukapigana mpaka watu wakaja amulia.
Dada yake akaanza nipa maneno ya shombo matusi akasema nilikuwa namnyanyasa mdogo wao simpi chakula sijui nini. Roho iliniuma sana maana huyo anayenitusi alikuwa kasimamishwa kazi na mmewe hana kazi anamtegemea mke mimi nilikuwa nampiga tafu hapa na pale kupitia kwa mama mtoto anamwambia mwamvie baba flani anisaidie hiki anisaidie kile namimi natoa tu.
Basi kumbe mzazi mwenzangu alikuwa chumbani kusikia ugomvi akatoka na mtoto mimi nikawambia naondoka mtoto watajua wenyewe na vitu sina shida navyo, dada yake akajibi nenda kwani watoto yatima hawakui.
Mimi nikaondoka nafika kwangu nakuta mzazi mwenzangu kapiga zaidi ya mara hamsini katuma sms zaidi ya 30 anasema amekatiwa tiketi anarudi moshi sijui nisikasirike mtoto atateseka hawawezi muhudumia kama nlivyokuwa namhudmia sijui nini.
Nikampgia simu mama yake naye ananiambia kuwa kapata taarifa namnyanyasa mwanae. Nikahisi kichwa kuzunguka nikasema potelea mbali.
Kesho yake mama yao ananipgia simu oh nimeongea na mzazi mwenzako anasema kuwa kumbe dada yake kakupakazia mimi nilivyokuwa na hasira nikasema sitaki kusikia kuhusu lolote.
Walipoenda moshi after a week wakaanza sumbua ela ya mtoto sijui nini mimi nikawajibu nilishawambia hayanihusu. Mama yangu mzazi akaniambia hasira hasara mtoto hana kosa nikaanza tuma ela ndogo ndogo ya matumizi.
Sasa wakaanza eti niwafuate niwarudishe dar mimi nikagoma mtoto hali ya kule kwa madai yao imemkataa anaumwa kila uchwao.
Ilifika kipindi nikataka warudisha niishi nao kwasababu ya mtoto lakini tatizo msg za mama yake haonyeshi kuregret halafu mostly anatuma msg za kuni blame mimi mara aseme kama siishi naye bora hata mtoto afe tu.
Hizo msgs ndiyo zinazidi nifanya nione siyo mtu sahihi wakuishi naye, mtoto now ana mwaka na miezi nane kwakwel kadhoofika siyo kama alivyoondoka kila mtu alikuwa anamtamani.
Kunipa mtoto wanasema mpaka nimchukue na mama yake jambo ambalo moyo wangu unakataa.
Mtoto aliacha mnyonyesha akiwa na moezo mitatu pasipo mimi kujua nimekuja gundua ana miezi mitano kisa maziwa yalikuwa hayatosho dr akashauri nimnunulie maziwa ya watoto yale ya kopo lakini akatusisitiza aisache kumnyonyesha kumbe mwenzangu nilipoanza nunua tu akaacha kumnyonyesha.
Wakuu niko dilema sijui hata nifanye nini maana namuonea huruma mtoto kuisha na mama yake napata hofu pia yani niko njia panda.