Nikipenda sipendwi, nikipendwa sipendi

Nikipenda sipendwi, nikipendwa sipendi

Hapo inatakiwa wewe ndio uanze kumpenda mwanamke na ukishampenda uwe na mbinu za kufanya yule uliyempenda naye akupende sababu sisi wanawake tukishapendwa na kuonyeshwa yale mapenzi ni rahisi sana na sisi kupenda tena saa nyingine tunapenda mpaka tunavuka kiwango yaani hatuoni wala kusikia.

Pia pole sana kwa kukikosa hicho kitu sababu kupendwa unapopenda ni raha sana.
Huu ndo ukweli asante dada Myta
 
Habari waungwana, natumai mu wazima,

Bila kupoteza muda kama mada inavyojieleza hapo juu ni kwamba nimekuwa na tabia ya kuumia saana hasa inapofika suala la mapenzi.

Mimi bado sijaoa na katika kutafuta mchumba nakua na sifa zangu ninazozihitaki, sasa nikianzisha mahusiano na mtu mwenye sifa ninazozihitaji mahusiano yetu huwa hayadumu na kuishia kuumia tu.

Kwa upande wa pili kuna wadada wanaonipenda saana na mpaka wanamua kuniambia tuoaene Ila hawana sifa ninazozihitaji kama nilivyoeleza hapo juu.

Hili tatizo hasa ni nini? Kwanini nisipate anaenipenda na mimi kumpenda? Kwanini huwa inatokea hivi?

Ahsanteni na karibuni kwa usahuri
Ndoa zinasumbua kwa kuwa katika hao wanandoa ni mmoja tuu ndo anampenda mwenzie mwingine unajutia rohoni kuwa ah angenikuwa fulani sasa basi fulani ama ndugu hawamtaki au yeye mwenyewe yaani huyo fulani alimkataa huyo mwanandoa asiyempenda mwenziye.
 
Unafikiri hizi ndoa zote wanaoana walio pendana kama unavyotaka?
 
Ila bora mwanaume akupende we mwanamke...kinyume na hapo ni kilio daily
Hapana huwa mwanamke ndo mwenye uwezo wa kumfanya mwanaume apende. Mwanamke ndo huanza kumpenda mwanaume na kisha kwa strategies zisizo na papara na akiwa na nidham na akiwa mtaratibu na akifanya Yale tunayotamani wanaume basi lazima mwanaume aingie kingi. Fact

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu unaweza kitumia tafsida maana duh lights yako ni Kali saana
hakuna tafsida hapo kaka neno MALAYA lipo hata kwenye kamusi ya kiswahili sio tusi hilo.......kaka wewe unatabia kama zangu ndio maana nmekujibu hvo hujui unachotaka wewe...unayemtaka ungemtengeneza mwenyewe .
 
hakuna tafsida hapo kaka neno MALAYA lipo hata kwenye kamusi ya kiswahili sio tusi hilo.......kaka wewe unatabia kama zangu ndio maana nmekujibu hvo hujui unachotaka wewe...unayemtaka ungemtengeneza mwenyewe .
Nimekusoma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom