Nikipenda sipendwi, nikipendwa sipendi

Ipananga kulwa

JF-Expert Member
Jul 24, 2017
573
290
Habari waungwana, natumai mu wazima,

Bila kupoteza muda kama mada inavyojieleza hapo juu ni kwamba nimekuwa na tabia ya kuumia saana hasa inapofika suala la mapenzi.

Mimi bado sijaoa na katika kutafuta mchumba nakua na sifa zangu ninazozihitaki, sasa nikianzisha mahusiano na mtu mwenye sifa ninazozihitaji mahusiano yetu huwa hayadumu na kuishia kuumia tu.

Kwa upande wa pili kuna wadada wanaonipenda saana na mpaka wanamua kuniambia tuoaene Ila hawana sifa ninazozihitaji kama nilivyoeleza hapo juu.

Hili tatizo hasa ni nini? Kwanini nisipate anaenipenda na mimi kumpenda? Kwanini huwa inatokea hivi?

Ahsanteni na karibuni kwa usahuri
 
Habari waungwana ,,,natumai muu wazima
Bila kupoteza Muda Kama mada inavyojieleza hapo juu ni kwamba nimekuwa na tabia ya kuumia saana hasa inapofika suala la mapenzi ,,mimi Bado cjaoa na katika kutafuta mchumba nakua na sifa zangu ninazozihitaki, Sasa nikianzisha mahusiano na mtu mwenye sifa ninazozihitaji mahusiano yetu huwa hayadumu na kuishia kuumia tu.
Kwa upande wa Pili kuna wadada wanaonipenda saana na mpaka wanamua kuniambia tuoaene Ila hawana sifa ninazozihitaji Kama nilivyoeleza hapo juu
Hili tatizo hasa ni nn? Kwa nn nisipate anaenipenda na mm kumpenda ? Kwa nn huwa inatokea hivi?
Ahsanteni na karibuni kwa usahuri
ndo iko hivyo baba tunapenda tusipopendwa. kwan we wataka sifa gani? au unaangalia chura baba?
 
Hapo inatakiwa wewe ndio uanze kumpenda mwanamke na ukishampenda uwe na mbinu za kufanya yule uliyempenda naye akupende sababu sisi wanawake tukishapendwa na kuonyeshwa yale mapenzi ni rahisi sana na sisi kupenda tena saa nyingine tunapenda mpaka tunavuka kiwango yaani hatuoni wala kusikia.

Pia pole sana kwa kukikosa hicho kitu sababu kupendwa unapopenda ni raha sana.
 
Hii formular ya mapenzi alieileta sijui alimanisha nini,? Inatokea Sana hiyo hata mimi naexperince hiyo hali af unakuta mtu mwenyew wa kawaida tu na ana kasoro nying tu kibinadam lkn we ndo umekufa kwake huambiliki yani, cha msing nikuachana nae japo inauma Sana
 
Umeshindwa kuandika hata kichwa cha habari tu? NIKIPENDA SIPENDWI, NIKIPENDWA SIPENDI. Sasa umeandika kama uko chekechea, na bado unashindwa kukielewa!! Pole sana, sina cha kuchangia maana ni uongo.
 
Ukumbuke binadam hatujakamilika na huwezi kumpata mwenye vigezo vyote unavyotaka muhimu kuangalia vile vya umuhim ambavyo unaona ni muhimu kwako

Hata usikate tamaa sababu riziki yako iko njiani yaja muda na wakati wako bado tu haujafika binadam tunaharaka tu kua mvumilivu huku ukimshirikisha Mungu kila tatizo au ombi unalotaka kwa nia thabiti
 
Wapo walipendana na wakawa pamoja, masuala et sijui unayempenda haku/hatakupenda au vice versa hio sema inatokea lakini sio constant, tatzo tunalazimisha kupenda au kupendwa na watu ambao hatu match nao, najua kuna wataopinga ila ukweli ndo huo kuna level nyingne inabidi uwe mpole, mfano Deo kisandu mwana jf mwenzetu amekufa ameoza kwa mtoto wa obama hata hawajuani au hata wangekua wanajuana hivi unadhan unadhan utaondoa kigezo cha gap la level zao? Na yeye aje kulalamika et ninayempenda hanipendi?
 
Kwaharaka nafkir vigezo vyako ndo hv ndo maana imekua tabu kumpata :-

~ Chura
~ mrembo
~ mwenye kipato (kazi)
~mkarimu mpole mwenye __hofu ya Mungu

NB: Kumpata mwanamke
Wa aina hii ni ngumu
Coz wengi wao huwa na watu wao tokea kitambo ambao wameanza nao from zero hadi kuwafikisha hapo.
Tafuta wako mpange mvishe mtunze nafikir ipo siku atakua kama unavyotaka
 
Hapo inatakiwa wewe ndio uanze kumpenda mwanamke na ukishampenda uwe na mbinu za kufanya yule uliyempenda naye akupende sababu sisi wanawake tukishapendwa na kuonyeshwa yale mapenzi ni rahisi sana na sisi kupenda tena saa nyingine tunapenda mpaka tunavuka kiwango yaani hatuoni wala kusikia.

Pia pole sana kwa kukikosa hicho kitu sababu kupendwa unapopenda ni raha sana.
Yaan nmeshafanya hayo mamba mwishon kabisa matarajio yanatoweka,,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom