Nikiota naongea ongea,nini tatizo wakuu?

Kijana kijana

JF-Expert Member
Mar 11, 2018
2,546
2,616
Wakuu nimekuwa na tatizo hasa wakati wa usiku wife huniambia karibia kila ssiku kwamba kuna maneno huwa nayaongea muda ungine yako yanaeleweka tu ila mm nakua sijielewi.

Sasa isije nikaota nachepuka nikaongea maneno maneno akajua ni kweli akaanzisha varangati.

Huu ni ugonjwa wakuu au tatizo nini hasa??
 
Kuongea usingizini kisayansi tatizo linaitwa SOMNILOQUY, si tatizo lenye madhara (kama sio mtu wa michepuko, ila kama unachepuka jiandae muda wowote kinanuka na wife wako).

Ni jambo lisilo la kawaida kwa mtu mzima, na sio tatizo la kuhitaji tiba ya hospitali, mara nyingi hutokea kwa muda usiozidi sekunde 30, ila linaweza kutoa mara nyingi ndani ya usiku mmoja (kwa episod tofauti).

Hua linasababishwa na;

1) Baadhi ya madawa ya hospitali.

2) Stress

3) Homa (zinazokimbilia kichwani, kama vile Malaria ya kichwani).

4) Matatizo ya akili.

5) Matumizi ya vilevi.

Unaweza ukaenda kuonana na mtaalamu wa maswala ya usingizi, ila tatizo la kuongea usingizini halina vipimo vya hospitali. (Atakushauri akigundua kama una hizo sababu juu).
 
mimi nilikuwa napiga stori na kucheka..
siku zingine natangaza football kama live..
lakini asubuhi sikumbuki chochote wadau tu wananimbia
 
Acha umbea ndiyo maana unaongeaongea hovyohovyo usiku kutunga maneno
 
Kuongea usingizini kisayansi tatizo linaitwa SOMNILOQUY, si tatizo lenye madhara (kama sio mtu wa michepuko, ila kama unachepuka jiandae muda wowote kinanuka na wife wako).

Ni jambo lisilo la kawaida kwa mtu mzima, na sio tatizo la kuhitaji tiba ya hospitali, mara nyingi hutokea kwa muda usiozidi sekunde 30, ila linaweza kutoa mara nyingi ndani ya usiku mmoja (kwa episod tofauti).

Hua linasababishwa na;

1) Baadhi ya madawa ya hospitali.

2) Stress

3) Homa (zinazokimbilia kichwani, kama vile Malaria ya kichwani).

4) Matatizo ya akili.

5) Matumizi ya vilevi.

Unaweza ukaenda kuonana na mtaalamu wa maswala ya usingizi, ila tatizo la kuongea usingizini halina vipimo vya hospitali. (Atakushauri akigundua kama una hizo sababu juu).
Nilkua na ndugu yang alkua na tatizo la ivo kuzungmza lugha isiyo eleweka wakati akiwa usingizini hii ime kaaje?
 
Wakuu nimekuwa na tatizo hasa wakati wa usiku wife huniambia karibia kila ssiku kwamba kuna maneno huwa nayaongea muda ungine yako yanaeleweka tu ila mm nakua sijielewi.

Sasa isije nikaota nachepuka nikaongea maneno maneno akajua ni kweli akaanzisha varangati.

Huu ni ugonjwa wakuu au tatizo nini hasa??
Soon utakuwa kama Jiwe.....fanya maombi Mungu akuepushe...la sivyo jiandae kuropoka mambo bila mpangilio
 
Nilkua na ndugu yang alkua na tatizo la ivo kuzungmza lugha isiyo eleweka wakati akiwa usingizini hii ime kaaje?
Khaa yani na wewe unaanzisha uzi ndani ya uzi?

Si ungesubiri majibuu tuu mku ya huu uzi wangu?
 
Wakuu nimekuwa na tatizo hasa wakati wa usiku wife huniambia karibia kila ssiku kwamba kuna maneno huwa nayaongea muda ungine yako yanaeleweka tu ila mm nakua sijielewi.

Sasa isije nikaota nachepuka nikaongea maneno maneno akajua ni kweli akaanzisha varangati.

Huu ni ugonjwa wakuu au tatizo nini hasa??
acha mawazo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom