Nikiondoka sirudi tena Dar

Baby Doll

JF-Expert Member
Aug 9, 2017
4,716
21,521
Ndugu zangu kilichonikuta Leo !!!!!
Nilikuja Dar ijumaa.(siishi dar huwa nakuja matembezi)
Kumbe mji una wenyewe!!!
Leo si nikatoka nataka kwenda kutembea tembea,
Nikaambiwa nichukue pikipiki nikawa bahili.
Nikapita mitaani huko. Nikaingia kibanda cha Tigo pesa nikatoa hela.
Ile naondoka ghafla kuna watu wa 3 wananifuata nyuma, halafu kuna uchochoro ,
Moyo ukaanza kudunda, nikiongeza mwendo na hao wanaongeza.
Nikaona wapita njia nikasema bora nimepona .nikaanza kutembea kawaida .
Wale watu walinikuta wakanizuia na wale wapita njia wakawa wameshapita.
Kuwaangalia wana kisu na sijui ni misumari ile.!!!
Nikasikia TULIA halafu na tusi juu. Nikasimama, wakaniambia kwa usalama nitoe kila kitu niwape niondoke.(ni saa ,10 jioni) nikawaambia nawaitia mwizi.
Wakaniambia nisijisumbue ule mtaa ni wao na wao ni maraisi hamna wa kuwatishia daah!!!
Mara watu wanapita nikaanza kusema "nyie niachieni kwa nini mnaniibia" nikijua wapita njia watanisaidia . khaa wanashangaa wanapita tuu.
Nikifikiria kasimu werevaa kangu hakana hata miezi mi 2.
Nikawa mwekundu ghafla ndani ya dakika 2 nimelia machozi hadi make up imeisha. Nikaanza kuomba msamaha "kaka zangu nisameheni mama yangu anaumwa yupo hospital ndiyo nimekuja kumuuguza"
Akaja mmoja nahisi ni mwenzao akawaambia mwacheni huyo akaniambia nifuatee, nikasema Mungu wangu ndiyo nimfuate wapi tena hapo ndipo nilipojikojolea (sio utani)
Hiyo ikawa pona yangu akaniambia nimpe namba zangu atanitafuta na niwe makini.
Nikaondoka nikarudi nyumbani ( nilipofikia) nikaingia ndani nikafunga milango na madirisha yote na nimeshusha mapazia ,
Nikalala nikajifunika hadi usoni nahisi watakuja.
Nilijawa hofu sana.
Khaaaaa pakuche tuu niondoke .
MTU UNAVAMIWA NA VISU WATU WANAANGALIA TUU.
Kweli nilizaliwa mwenyew nitakufa mwenyewe.
Nyie KAKA JAMBAZI kama mpo huku nawaambia SIWAOGOPI. Na nimewablock
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom