Nikiona mtu anaibiwa nahisi kama naibiwa mimi...

Nikiona mtu anaibiwa nahisi kama naibiwa mimi...

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Posts
20,334
Reaction score
23,945
Nikiona mtu anaibiwa nahisi kama naibiwa mimi..


​
1999, Himo - Kilimanjaro.
images


Nilikuwa nimemaliza Chuo Kikuu cha Mlimani wanavyokiita watoto wa siku hizi. Enzi zetu ilikuwa ‘The University of Dar es salaam’ na heshima zote kijijini mtoto wa mangi, Mentor amemalisa sule sote kapisa!!


Anyway katika harakati za kutafuta kazi nikawa nafanya kazi kwenye gesti/lodge ya baba pale Himo mjini, kama meneja! Ilikuwa gesti nzuri sana kwa standards za kipindi kile. Kulikuwa na simu kila chumba, feni, choo na bafu ndani na huduma ya bar kwa nje..mahitaji muhimu kwa wale kina infii.



Katika muda niliokaa pale nilipata mikasa na raha nyingi sana. Moja nzuri ninayoikumbuka ni interaction yangu ya kwanza na Polisi. Guest yetu ilikuwa nzuri kiasi cha kwamba wakati ule walipofanya kikao cha Maofisa wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro basi walikodi vyumba na ukumbi katika lodge yetu.



Nakumbuka baada ya kikao chao nilipeleka bill kwa OCS pale Himo kudai malipo ya huduma zote walizopata kwa muda wote wa kikao chao. Alinizungusha sana yule OCS. Siku moja nikaamua kusafiri hadi Moshi Mjini kuonana na RPC nakumbuka enzi hizo alikuwa ni Afande Chiko. Nikaingia moja kwa moja nikamweleza mzee sijalipwa.

Akanyanyua simu akapiga kwa OCS sijui waliongea nini akaniambia nirudi kwa OCS. Kufika kwa OCS namkuta anacheka eti mangi pesa umefuata hadi kwa RPC nikamwambia niliona unanizingua. Akanipa nusu yake akanambia nyingine atanipa baadaye. Kusema kweli hadi leo ile nusu nyingine sijawahi kuipata!!



Hiyo ni topic ya siku nyingine..leo nimekumbuka kisa kilichonifanya nishikilie msimamo wangu wa kutokuoa..at least sio kwa sasa.



Unapokuwa gesti unachoangalia ni pesa tu. As long as wateja wanalipa bili wanayofanya humo ndani hayakuhusu..chezea mangi na heleri!!!



Siku moja niko ofisini asubuhi mapema, akaja kaka (kwa makadirio ni 28-30yrs) mmoja akakaa kwenye bar pembeni. Mara akae mara asimame..yani he was so restless. Nikamfuata nikamuuliza shida yake.



Mentor: “Habari kaka, sijui nikusaidieje naona umekaa hapa muda bila msaada”
Bro: “Kuna mshkaji namngoja yupo humo ndani chumba namba 28 kuna biashara tunafanya.”
Mentor: “Oooh sasa si ungesema kaka, basi ngoja nimpigie halafu nimwambie”
Nikamwacha pale nikaenda ofisini na kupiga extension ya chumba namba 28. Akapokea;
Mteja (wa chumba namba 28): “Halooo KakaKiiza hapa”
Mentor: “Hallo ndugu habari za asubuhi”
Mteja ( KakaKiiza): “nzuri nambie”
Mentor: “Kuna ndugu hapa nje anaitwa sosoliso anasema anakungoja muda mrefu sasa. ”
Mara mshkaji akawa kimya ghafla..nikasema nini tena…ikabidi anieleze sasa;
[SIZE=3 [B]KakaKiiza[/B]: “dah, menejaee huyo mshkaji wala hatuna biashara naye wala nini. Tafadhali nisaidie niko na mke wake ndani huku atakuwa ametushtukia.”[/SIZE]


Kichwa kikagonga..nikashtuka sana nikajua leo msala umeifikia gesti yangu lazima damu imwagike. Sasa mchaga ninavyopenda pesa mimi (ila mnisamehe tu..ilikuwa enzi zile) ikabidi niwaambie wahudumu wa pale kuwa namwita Yule mshkaji ( sosoliso) aje ofisini ili aongee na mteja wangu (wa chumba namba 28 a.k.a KakaKiiza ). Akiingia tu ndani basi wamtoe Yule mkewe wampeleke kwenye nyumba nyingine ya kwetu kama viwanja vitatu mbele.


Basi nikamwita sosoliso akaingia ofisini, akanyanyua simu. Ile kusikia tu sauti ya KakaKiiza akaweka simu chini akashindwa kuongea…akaniambia ndugu Mentor naomba unisaidie. Ikabidi aanze na yeye kunihadithia story yote.



Mkewe aliaga anaenda Kibosho akitokea kwa mjombake Tanga. Huku nyuma akasikia kuwa mkewe kaishia Himo kwenye gesti. Nilichompendea huyu jamaa alifanya research yake vizuri hadi chumba walichokuwa wanalala alijua. Akaniomba nimsaidie tu kumpata mke wake amwonyeshe tu kuwa amejua. Ila hakujua huku nyuma mkewe ashatoroshwa.



Nikamwambia siwezi kuwa na uhakika labda twende tukahakikishe chumbani. Tukaongozana wote hadi chumba alimo KakaKiiza. Tukagonga akafungua..yani ile kukutanisha macho hata mimi mwenyewe nilijisikia vibaya. Ila kwa kuwa ushahidi ulishaondolewa sikuwa na wasiwasi. sosoliso akaingia ndani akasachi wee na kweli mkewe hakuwepo. Tukatoka wote nje amechanganyikiwa kabisa.



Haraka haraka KakaKiiza akampigia mshkaji wake ambaye kwenye simu alimuita Kipaji Halisi akaja na mandolini yake. Nakumbuka ilikuwa imejaa maparachichi akamchukua wakaondoka eneo la tukio.



Nikamwambia sosoliso kama vipi akatafute ushahidi zaidi au mkewe yupo sehemu nyingine. Akaondoka, kumbe alienda kituoni Polisi kuripoti kuwa ana uhakika mkewe yupo kwenye gesti yangu na mimi ninamficha.



Huku nyuma ikabidi niwahi home nikamtoroshe Yule mke wa Sosoliso. Katika mahojiano ndo akaniambia anaitwa Paloma na kwamba ni kweli sosoliso ni mumewe na Kaka Kiiza walikutanaga tu kwenye party ya kazini.



Basi nikampakiza kwenye taxi andoke pale.



Wkati narudi gesti nakutana na polisi mlangoni wakaanza kunihoji kana kwamba wana uhakika 100% ninajua mke wa sosoliso alipo. Nikakataa...



Wakasema wanafanya ukaguzi vyumba vyote. Wakaanza kukagua wee. Nakumbuka kwenye chumba namba 12 kulikuwa na mteja mwingine kutokea Dar ambaye naye aliniambia yuko pale kwa likizo na kwamba alikuwa na mkewe na wasingependa kusumbuliwa kabisa hata kwa simu. Hivyo polisi walipofika chumba kile nikawaelezea na kuwaomba wakiruke chumba kile na kuendelea na vingine. sosoliso akang’aka kusema ndo huko mkewe alipo. Niliwaomba sana ila wakakataa ikabidi nimpigie simu kumuomba afungue mlango.



Mentor: “Hallo mteja samahani. Kuna polisi wamekuja hapa wanataka kufanya upekuzi kidogo kuna ndugu anamtafuta mkewe naomba ufungue mlango”
Mshkaji akakubali akafungua mlango.



Swali la kwanza kabla hata polisi hawajaanza kumuhoji akamtupia swali Sosoliso, “Unamtafuta mke guest?” Mara akamwita ‘bebii’ wake aje akamwuliza tena, “Huyu ndo mkeo?”
Kwa kweli lile swali lilinichoma sana na kujihisi msaliti..



Polisi wakakagua wakamaliza ila waliomba vitambulisho vyao pia: KUMBE..na wao si wanandoa…ni wezi wa mapenzi tu kama KakaKiiza...maana mshkaji alikuwa anaitwa Mtambuzi s/o Dark City na Yule dada (ambaye kwa makadirio ni mwanafunzi wa chuo) alikuwa anaitwa KING’asti d/o Asprin. (kutokana na maelezo ya polisi)



Basi baada ya ukaguzi tukaondoka kuelekea kituoni. Wakamchukua na baamedi mmoja pamoja na mimi na sosoliso hao kwenye PT 0047 ya polisi kituoni Himo.
Wakaanza kutuhoji mmoja mmoja...



Zamu yangu ilipofika, Sosoliso aliniuliza swali moja lenye kunifanya nijisikie msaliti hadi leo..
[SIZE=3 [B]sosoliso[/B]: “Mentor, wewe ni dini gani?”[/SIZE]

Mentor: “Mkriii..mkristo kweli”
Sosoliso: “Hivi ndugu yangu kama ungekuwa upo mbele ya padre hapa akakuuliza kama kweli hujui alipo mke wa Sosoliso ungesemaje?”

Mentor: “Hapana, sifahamu alipo!”



Baamedi akaja naye akashindilia msumari wa mwisho kwa kusema kuwa ni kweli aliona mtu akitoka kwa haraka lakini hakujua kama ndo mke wa sosoliso.

Kwa hali hiyo kesi ikaishia hapo…ila mpaka leo nikikaa nikakumbuka ile siku huwa naogopa sana kuoa.

Wasalaam Wapendwa,
Mentor.




PICTURE UPDATES (Courtesy of kaka Mtambuzi)

Ndugu sosoliso alitarajia kumfuma mkewe Paloma akiwa na KakaKiiza hivi..
images


Au hivi...
images



Matokeo yake akakuta chumba empty na KakaKiiza katulia utadhani alikuwa peke yake kama hivi...
images



Kumbe Paloma aliruka ukuta na kukimbilia nyumba ya jirani style za Jackie Joyner Kersee...
images


KakaKiiza akaja kuchukuliwa na Kipaji Halisi ndani ya mandolini...

images



Huku nyuma sosoliso akabaki analia..mwanaume mtu mzima..
images


Polisi nao hawakuweza kusuluhisha jambo lolote...
images


Huku nyuma King'asti na Asprin wanatumbua maraha..
images


Baba yake King'asti, mzee Mtambuzi anajua mwanaye ameenda field work Moshi..
images


Mke wa Asprin anajua mumewe kaenda kuwasalimia wazazi kijijini...

images





NA HAYO NDO MAISHA YA MJINI.....
 
Last edited by a moderator:
::
Hujampata tu wa kukuweka sawa,,mbona hayo yote utafumba macho? Usicheze na mwanamke Mentor!
::
Ukweli unaosikitisha ni kuwa kizuri huli peke yako.
=
 
Last edited by a moderator:
Usiingie kwenye Ndoa na Mizani ya Adam" ninamaanisha aliyofanyiwa Adam na Eva sidhani kama nawe yatakukuta hayo, maana ni binadamu tofauti. Wewe kama unataka kuoa Omba Mungu akupe mke mtiifu, mwenye adabu na heshima na kukufanya wewe uheshimike na ukoo.
 
::
Hujampata tu wa kukuweka sawa,,mbona hayo yote utafumba macho? Usicheze na mwanamke Mentor!
::
Ukweli unaosikitisha ni kuwa kizuri huli peke yako.
=
Hahahaahahahaaha!!!! Tetraaaaaaaaaa Unamtishia mwenzio wewe vipi bwana, unatakiwa kumtia Moyo!!!!
 
NB: Based on a very true story....majina ya wahusika yamebadilishwa ili kuwapa privacy!!!
 
::
Hujampata tu wa kukuweka sawa,,mbona hayo yote utafumba macho? Usicheze na mwanamke Mentor!
::
Ukweli unaosikitisha ni kuwa kizuri huli peke yako.
=

For sure, USICHEZE NA MWANAMKE!!!!:-*
 
NB: Based on a very true story....majina ya wahusika yamebadilishwa ili kuwapa privacy!!!

What? Mentor! Based on a true story? And the setting is Himo. a place I know so well. Which guest house are you talking about? Silent Inn? King Size? Which?
 
Last edited by a moderator:
Lol. Yaani wewe dingi Mtambuzi akiona hili soo si nimekwisha mimi jamani?

Ila mentor, mimi cousin wangu ana gesti na iko next to his house. So wageni wake wote huwa tunalala gest. Niliyoyaona nimechoka kuwaza mapenzi. Na ndo maana i am so relaxed kuhusu mapenzi. Najua kuibiwa kumo na nina hakika nikimfuma Paw wala sitopata wazimu na kuhangaika hivyo. Huwezi kumfanya mwenza kama project uanze kuhusisha na polisi na sijui mkiti wa mtaa. Ninkama ukinunua gari unajua kuna wezi wa sight mirror na power window, afu kuna kina bob sambeke wanaolichukua zima zima. Kirrruuuuu, kusakana huko umemzaa wewe?
 
Last edited by a moderator:
ha ha ha.. babe Paloma hebu njoo uone huyu shigongo Mentor anavyotaka kutengeneza pesa kupitia kwetu.. hii ni kashfa hii..
ninatafuta lawyer.. Arushaone[/MENTION]




Mwanasheria wa kuaminika ni Lawyer Ruttashobolwa tu humu
 
Last edited by a moderator:
Kahaaa!! Mentor, kama sio king size ni seven stars hiyo.
Ingekuwa Mtambuzi yupo the other side, lazima mtu angechezea kalma kwanza ndio mahojiano yaanze na mikwara kibaao!!.
 
Back
Top Bottom