Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,976
- 22,419
Nlipomaliza chuo July 2013, niliondoka nkaelekea Tanga kwa ajili ya mapumziko ya mwezi mmoja na pia kwa ajili ya kusambaza bahasha za kaki, ilipofika september nikaamua nielekee mkoa flani nkaenda kumuona meneja wa tawi la bank flani hivi kumuomba nifanye volunteering pale. Akaniruhusu, akaniambia nikifanya vizuri pengine naweza nkaajiriwa. Nikafanya volunteering pale mpaka tarehe 26 Nov nlipoamua kuelekea kwenye graduation. Nlipo rudi kutoka kwenye graduu nkakuta kuna dada kaajiriwa kama marketing officer, hiyo ngoma ikanifanya nione pengine sikuperform kama walivyo tarajia ila kwa upande wa pili na jinsi nilivyojiamini kile kitendo kilinikera sana.
Baada ya fikra za kama wiki moja hivi nliamua kuacha volunteering pale bank na nkaamua nielekee Dar japo kwa wiki moja tu, nkasambaze bahasha zangu na huko halafu nirudi home Tanga. Nakumbuka nlipeleka bahasha BOA, NHIF, NSSF na sehemu nyengine nyingi tu.
Siku hiyo nkaamua kwenda makao makuu ya NBC pale posta bandarini huku najisemea kuwa lazima nkawaone wahusika haswa maana hizi bahasha huwa wanazitupa kwenye dustbin. Kufika pale reception nkawakuta wadada na wakaka marika yangu kabisa (hasira zikanipanda wametusua vipi halafu mimi bado nahangaika). Nkawaomba kumuona HR, haraka haraka nkajibiwa haiwezekani, nkaulizwa unataka nini kwani? nkaona noma kuwaambia nataka kazi. Nkawaambia ni personal issue, nkaomba kumuona head of Marketing, pia wakaniambia hawa Ma-head ndugu yetu huwezi kuwaona kama huna appointment nao, sema unataka nini tuwaambie. Akili zangu za mchana ule zikanituma sawia kabisa. Nkamwambia yule dada, mwambie head of Marketing kuna kijana hapa kasema ana account mia tatu (200) ila hatozitoa mpaka nionane nae ili nijue what is my share out of it.
Kudaadeki wakampigia simu, dakika mbili nyingi nkapewa visitors card nkaambiwa nikapande lift niende ghorofa ya saba. Kufika tu ghorofa ya saba ile lift kufunguka nkamkuta dada mmoja kisu sana aged aroung 35-45 ananisubiri nje ya lift hahahahahah (I turned to be important asset). Akaniambi you must be.......... akataja jina langu. Nkamwambia ndio, akanichukua ofisini kwake. Kufika tu nkamuomba msamaha kwa kudanganya, nkamwambia sina akaunti 200 wala nini nlichotaka ni kuonana nae yeye tu. Nkamueleza lengo langu, ki ukweli yule dada alikuwa impressed sana na mimi ila akanijulisha tu kwa muda ule NBC hawaajiri isipokuwa kama nataka nijitolee atanichukua na hata kesho niripoti pale head office kitu ambacho nlikikataa.
Nkaamua kurudi Tanga nkawa kibarua wa fundi ujenzi mtaani kwetu, washkaji walikuwa wananicheka eti nimehangaika kusoma na sasa nimekuwa kibarua fundi ujenzi, nlipiga moyo konde nkijua ni nini nafanya. Nlifanya kazi ile kwa muda wa kama mwezi tu hivi, yule manager wa bank alinipigia simu tarehe 5 February 2014 akitaka niripoti kazini, nkiwa kwenye basi naelekea Dar siku ile ile akaniambia nipitie Head Office yao pale Dar nikamilishe taratibu zote za ajira halafu nielekee huko mkoani kwa ajili ya ajira.