kaka_mkubwa
Member
- Apr 6, 2012
- 37
- 59
Habari wakuu,
Kila nikifikiria hili swala la watumishi hewa huwa sipati majibu labda waungwana mtanisaidia.
Mshahara hewa, nafikiri kama ilivyo mishahara mingine, hupitia makato yote kama PAYE, hifadhi ya jamii (PSPF, NSSF n.k), Bima ya Afya, Vyama vya wafanyakazi, na mengineyo kulingana na mfanyakazi husika. Lakini hayo machache yanamhusu kila mfanyakazi wa Serikali.
Shida yangu inakuja kuwa ina maana TRA walikuwa wanapokea kodi kutoka kwa wafanyakazi hewa, Mifuko ya hifadhi ya jamii ilikuwa inapokea michango kutoka kwa wafanyakazi hewa, Bima ya afya walikuwa wanakata michango ya wafanyakazi hewa na kadhalika. Usikute hiyo mishahara hewa ina hadi mikopo kwenye mabenki na wanakatwa marejesho kila mwezi!
Hii inamaanisha kuwa TRA, Mifuko ya jamii, Bima ya afya n.k hawana mfumo wa uhakiki wa watu wao, kwa hiyo kuna uwezekano dili likabadilishwa kirahisi, sasa hivi ile mishahara halali hayo makato yote yakaliwa na wsigundulike, itakuwa jibu rahisi tu kuwa wale walikuwa hewa maana ni zaidi ya wafanyakazi 5000 Kama walipokea michango hewa na hawakujua kitu gani kitawafanya sasa hivi wageuke?
Mapendekezo yangu, pamoja na hili linaloendelea la kuwaondoa kwenye malipo lakini inabidi kwenda mbali zaidi. Nina wafanyakazi wangu, akitenda na tukisha ongea na kumalizana, kama onyo au adhabu, kinachofuata ni maelezo yanayojitosheleza kuwa amejifunza nini katika lile kosa au hasara hiyo na ni jinsi gani uongozi na yeye wanaweza kuzuia kwa wakati mwingine. Nafikiri uchunguzi wa kina ufanyike katika hili.
Lakini pendekezo langu lingine ni kuwa uangaliwe uwezekano wa kuzirudisha hizo fedha, ikiwemo kuwabana na kuwafilisi wahusika, angalau kurudisha kiasi cha hizo zilizopotea, ikiwa ni pamoja na kuchukua akiba zao katika mifuko ya hifadhi za jamii.
Asante kwa leo