Amicus Curiae
JF-Expert Member
- Sep 12, 2012
- 5,352
- 7,668
- Thread starter
-
- #21
Hakuna mahali nimesema mimi ni mkopeshaji niliyekidhi vigezo (niliyesajiliwa), sijasema gari ni langu na sijasema nina mkataba wa mauziano, hizo facts ni zako wewe binafsi na sijui umezitoa wapi!Hapo hujakopesha, bali umetoa msaada. Huna sifa za kukopesha, kwa sababu hujakidhi vigezo vya kuwa mkopeshaj...
Asante sana kwa ushauri mzuri mkuu.Weka tamaa nyuma mkuu, inua macho yako mbele zaidi.
Kujimilikisha naweza kwasababu nina makubaliano (mkataba) ambao niliandikishiana nao kwa Wakili. Kitaalamu, kule TRA wakati wa transfer of ownership, badala ya mkataba wa mauziano, unawekwa huu mkataba wangu wa kukopeshana fedha kwa dhamana.
Mimi kukamatwa haiwezekani kwani nina mkataba ambao unaonyesha mmiliki halali ndio amenikabidhi gari lake kama dhamana yeye mwenyewe kwa hiari yake.
Kwa maneno mengine unanishauri niwavumilie? Wakija mwakani je? Au wasipokuja kabisa? Na vipi kuhusu amana yangu ambayo inatakiwa irudi kwenye mzunguko?sio lazima kujimilikisha kitu ambacho sio chako, cha msingi baki kwenye makubaliano makuu mliyoandikishana
Nakushauri wape muda kidogo, though uvumilivu una kikomoKwa maneno mengine unanishauri niwavumilie? Wakija mwakani je? Au wasipokuja kabisa? Na vipi kuhusu amana yangu ambayo inatakiwa irudi kwenye mzunguko?
Chai hii, tena haina hata maziwa.Wakuu, kwanza poleni kwa mihangaiko ya kutwa nzima ya leo. Ndugu yenu nataka kufanya maamuzi ila sitaki nionekane nimedhulumu haki ya mtu.
Miezi 3 iliyopita kuna jamaa ambao sifahamiani nao; walikuwa wanasafirisha magendo kwa gari binafsi kutoka point "X" kwenda point "Y". Wakakamatwa na polisi njiani wakawekwa ndani. Gari nayo (Spacio) ikazuiliwa kama kielelezo.
Sijui walielewana nini na askari, wakawa wana shida na mill 3. Nikapigiwa simu na mwanangu mmoja ambaye ndio anafahamiana na hao watuhumiwa, akaniomba niwakopeshe hiyo hela kwasababu anawafahamu, ila akakataa kuwadhamini.
Na mimi nikashtuka. Ili kuepuka kugombana na jamaa yangu nikakataa kutoa pesa kwa mali kauli. Mmoja wa watuhumiwa akaomba aagize gari yake itoke mkoani ije iwekwe bond kwangu ili niwape pesa. Gari ikaja.
Nikatoa pesa, jamaa wakatoka mahabusu, tukaandika makubaliano, nikakabidhiwa gari (Toyota crown athlete mpya kabisa) na kadi yake. Mwisho wa wao kunirudishia pesa yangu ilikuwa ni juzi tar 12/08/2023. Makubaliano yanasema wakishindwa kurudisha hiyo pesa kwa wakati bila taarifa yoyote rasmi, basi gari itakuwa mali yangu. Cha ajabu ni kwamba, hadi hiyo tarehe 12 inakaribia hakuna hata mmoja kati ya wale watuhumiwa amenipigia simu! Wote wako kimya na hawapatikani! Ninayewasiliana nae ni huyu jamaa yangu tu ambaye naishi nae huku niliko, na yeye hajui kilichowasibu!
Sasa ningeweza kuwasikilizia ila hela yangu iko kwenye mzunguko, natakiwa niitumbukize mahali niongeze faida. Hapa nafanyaje wakuu? Nikijihamishia umiliki wa hii gari sitaonekana nimedhulumu? Manake wanadamu kwa nongwa hatujambo!
Naombeni ushauri.
Kwani giyo gari inatumia maji? Vipi kuhusu service, watakuwa wanafanya hao maharamia?Kwani gari imekaa ndani kama picha?
Anza kuizungukia na kuifanyia biashara. Bebea hata matofali.
In case wakija hela watakupa, wasipokuja unakua umerudisha hela yako
Polisi sijaenda kwa ukaguzi ila TRA nimeshahakiki taarifa za gari na iko salama. Hili lilifanyika kabla sijatoa pesa.
- Kubadili umiliki inatakiwa mwenye mali akupe picha zake ndogo, na nakala ya kitambulisho, je vyote unavyo?
- Je,mkataba unasema baada ya kushindwa kurejesha gari wewe ndiye utakuwa mmiliki halali?
- Je umeenda TRA kwa ukaguzi na kuthibitisha jina linalosoma kwenye kadi ndio mmiliki i.e wapo wanaofoji hizo document
- Je hilo gari umepeleka polisi kwa ukaguzi ili kugundua kama lina makosa yoyote i.e uuaji, makosa mengine n.k
Asante kwa ushauri mzuri mkuu. Ngoja tuone.Nakushauri wape muda kidogo, though uvumilivu una kikomo
[emoji28][emoji28]Kwani giyo gari inatumia maji? Vipi kuhusu service, watakuwa wanafanya hao maharamia?
Ndugu za hao jamaa, wakisema wewe ndio umewapoteza ili ujimilikishe gari?Polisi sijaenda kwa ukaguzi ila TRA nimeshahakiki taarifa za gari na iko salama. Hili lilifanyika kabla sijatoa pesa.
Kwenye mkataba kuna clause iko wazi inasema kabisa kwamba wakishindwa kulipa pesa kwa wakati bila taarifa rasmi gari itakuwa mali yangu.
Kuhusu picha na kitambulisho naandika KIAPO CHA KUTOKUJUA ALIPO MKOPAJI AU AN AFFIDAVIT REGARDING UNKNOWN WHEREABOUTS OF THE BORROWER. It is that simple.
Daaaaa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Jiulize swali la Muhimu. Angekuwa Yesu angefanya nini?
POA CHIEFAsante kwa ushauri mzuri mkuu. Ngoja tuone.
Hawa nao ipo namna ya kuwakabili mkuu.Ndugu za hao jamaa, wakisema wewe ndio umewapoteza ili ujimilikishe gari?