Nikiangalia uso wa Tundu Lissu namsoma namna hii...

Unaweza ukawa na ajenda nzuri na nyeti sana,lakini namna unavyoziwasilisha ikawa si sawa (utaratibu).hii ni mojawapo ya udhaifu wa wanasiasa wetu walio wengi,kwani ni wagumu kushaurika
wepesi kuwasilisha,si team-work oriented personally na kujifanya wajuaji wa kila kitu bila kufanya utafiti.
 
Tundu Lisu ni jasiri sana. wale wanaomsuta wanasemea pembeni lakini wangewekwa kwenye mdahalo na Lisu tungeju aliye dhaifu au jasiri mkweli au asiye mkweli kirahisi zaidi
 
TL namwamwini sana yaani ni kama JKN yaani akiwa rais wa nchi yako unalala usingizi bila wasiwasi ukijua kwamba kuna mtu ikulu kwa niaba yako,akienda kwenye mikutano ya kimataifa au akienda kukutana na marais hata wa nchi kubwa au marais wengine wenye akili kama Obama huna wasiwasi kwamba atanga'ara.ukietembelea nchi ya kigeni ukiwambia unatoka nchi ambayo rais wake ni TL class unapata special treatment na hongera kibao! NATABIRI KUNA SIKU SINGIDA ITATOA RAIS KUPITIA CHADEMA!
 
natamani wawepo kina lisu hata 10 na magazeti aina ya mwanahalisi kama 2, inatosha kuwapigisha magoti watawala legelege! bahati mbaya tulionao wanakosa baadhi ya sifa za Lissu na bahati mbaya hakuna hata gazeti moja baada ya mwanahalidi kutiwa kufuri... hata hivo mungu yupo
 
And he is getting stronger!

I admire Hon. Lissu a lot. Yeah, both his personality and his noble service to this nation.
 
Ni kweli Mhe.Lissu hajisahau kuwawakilisha wananchi wake bungeni kwa vitendo
 
Nikiboko ya WEREMA na majaji vihiyo wengine,Werema hatakaa amshinde kwa hoja asilani atatukana sana sijui fuga nywele matusi ni dalili ya kutokuwa na hoja madhubuti.
 
Mkuu ukiongelea Antipas Lissu unaongea level nyingine kabisa nauona uzalendo wa ndani kabisa wa huyu mtu kwa Tanzania na watanzania walio masikini wanaonyanyaswe kwenye kipande cha ardhi yao yenye madini,maziwa,asali,misitu,wanyama ambao Jangili Kinana anawabeba,anatumia weledi wake vizuri kwa ajili ya Tanzania iliyo mlea hapa rasili mali za nchi zilitumika vizuri kumsomesha.
 
TL namwamwini sana yaani ni kama JKN yaani akiwa rais wa nchi yako unalala usingizi bila wasiwasi ukijua kwamba kuna mtu ikulu kwa niaba yako,akienda kwenye mikutano ya kimataifa au akienda kukutana na marais hata wa nchi kubwa au marais wengine wenye akili kama Obama huna wasiwasi kwamba atanga'ara.ukietembelea nchi ya kigeni ukiwambia unatoka nchi ambayo rais wake ni TL class unapata special treatment na hongera kibao! NATABIRI KUNA SIKU SINGIDA ITATOA RAIS KUPITIA CHADEMA!

Inshallah
 
Nina hakika hata Mh.Rais kikwete na chama chake na serikali nzima toka kwenye mioyo yao wanajua Tundu lissu ni nani! Huyu jamaa kiukweli yupo tofauti sana na viongozi wengine Mungu ambariki sana na azidi kumzidishia nguvu hua anazungumzia mambo ya msingi sana ya Taifa hili!
 
hivi wewe mleta hii mada,mbona umeniibia mawazo yangu?,au kwa nini mawazo yetu yanafanana? pamoja na umaskini wooote huu na taifa langu hili hohehahe lakini huwa naijiwa na faraja kubwa nikisikia jina la Tundu A. M. Lissu.kwa kifupi ni kielelezo cha uzalendo wa taifa na ngao pekee ambayo taifa hili linaweza kuitegemea.Mungu ampe maisha marefu Tundu A.M.Lissu
 
Mbona kama mahaba tu hayo, bora ungetupia wasifu labda ungetupa fursa ya tusiomjua tukamjua vyema. Lakini pamoja na mapambo yote mnayompa bado anatakiwa kujirekebisha ili awe kama mwansiasa wa leo manake jamaa anaonekana kama mbabe wa miaka ya 1980's hivi na jazba ziko mbele mno na zinampeleka kuliko hekima na busara na umakini wake pia ni questionable manake mijadala yake mara nyingi inaishia kuomba radhi anayo nafasi ya kujifunza kutoka kwa Dr. Slaa alivyokuwa bungeni na kina Zitto na jinsi walivyofanikiwa na kupeleka harakati mbele mno kuliko yeye na mijadala yake yenye utata kuliko hoja.

Wasomi wa leo hii wa sheria wanapaswa kutupeleka katika sheria mpya zinazoendana na wakati huu, sio kung'ang'ania majaji hawanasifa kwa miezi sita just once na anakamata data nyingine anasonga. Kwenye halmashauri huko zimeenda pesa mingi na accountability ndio taabu, Dr. Slaa alikuwa mwarobaini katika hilo, sasa hayupo wakina Tundu ndio walitakiwa kutembelea mikono sasa.

Kwa sifa hizi na mapambio mnayowapa akiyamungu mtawaharibu hawa watu manake manake wanaonekana ni kina Dully.
 
tundu mughai lissu ni kiwango...unadhani kwa nini magamba wana unya unya?
 
Back
Top Bottom